Walimu Sekondari ya Aga Khan wagoma kisa Ubaguzi wa Rangi

Walimu Sekondari ya Aga Khan wagoma kisa Ubaguzi wa Rangi

Misingi ya kikoloni ilishaweka hiyo mizizi, jitihada za ziada zinahitaji kupindua meza kwa kweli

Uko sawa cha ajabu tumerithi haya mambo bila ya kuelewa maana yake mfano mpaka leo hii tunaita maeneo Uzunguni, Uhindini na Uswahili bila ya kujua ni Wazungu waliweka hiyo apartheid wakati wa Ukoloni ilikuwa hivyo maeneo bora ni kwa Wazungu Uzunguni kama O‘bey, ya daraja la pili Uhindini kama Upanga na daraja la tatu na la mwisho uswahilini kama Magomeni na mpaka leo hii hata kwenye mji mipya sehemu nzuri tunaita uzunguni au Uhindini sehemu mbaya na chafu tunaita uswahilini lakini chanzo cha huo mgawanyiko ni ubaguzi dhidi yetu na sisi tunaendeleza bila ya kujua, …
 
Hili suala sio la kuvumilia kabisa..yani ndani ya nchi yako bado unanyanyasika utoke uende kwenye nchi zao nako unyanyasike...hii si sawa.

Kama serikali imeshindwa kusimama na kukemea wazi wqzi vitendo hivyi vya ubaguzi ifike hatua wananchi tuanze kuwanyoosha hawa ma gabachori.


#MaendeleoHayanaChama
Mfumo ni uleule toka ukoloni,unaona hapo HR ni muafrika mwenzetu ila anatetea,hana tofauti na akida au liwali wa enzi ya mkoloni[emoji1787][emoji1787]
 
Yaani mpaka wamefikia Kugoma, basi tujue ukweli kwamba hali ni mbaya sana. Huyo HR Msaidizi ni Mtanzania na kwa kauli yake hiyo inaonyesha wazi anawatetea Wahindi.

Jiwe mwenyewe alishindwa kwa Mr. Aga Khan pamoja na kukutana Uso kwa Uso; kuhusu Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) kupokelewa katika Hospitali zake na wananchi waliliongelea sana hili suala mpaka aibu lakini mpaka kesho bado 'Ngoma Ngumu'.

Sembuse hili la Unyanyasaji wa Walimu Wazawa? Serikali ile ile tuitegemee tena!!?

Nawatakieni Kila la Kheri.
NHIF inqtumika aghkhan ila inategemea na thaman ya kadi,hizi za walalahoi ndo haziingii ila zile za juu kama wanazotumia TRA,BOT au NHIF zinatumika vzr tu
 
Wahindi ndivyo walivyo NCHI mzima na kibaya zaidi, utateseka kisaikolojia tu na hutakuwa na Msingi wowote wa hoja za kisheria wa kusimamia.

Kitakachokuweka hapo kwenye Ajira Ni njaa Kali na Hakuna kitu utakacho badili.

Hakuna shule, kampuni au taasisi za Kihindi au kiislam zikakosa ubaguzi.

Ubaguzi kwao Ni SUNNA.
Uislam umeingiaje sasa hapa?? Kina taasisi gani ya kiislamu au unazungumzia bakwata??
 
ZAIDI ya walimu 50 wenye asili ya Kiafrika kwenye shule ya Sekondari ya The Agha Khan Mzizima wamegoma kuingia darasani kufundisha wanafunzi kwa kile walichodai kuwa uongozi wa shule hiyo umekuwa ukiwanyanyasa na kuwabagua kwa rangi.

MwanaHALISI kupitia chanzo cha kuaminika kilipata taarifa hizo na kufika shule hapo kushuhudia mgomo huo ulianza leo tarehe 24 Mei 2022 asubuhi.

Mwandishi wetu alipofika shule hapo aliwakuta wanafunzi wakirandaranda nje ya madarasa huku walimu wenye asili ya kitanzania wakiwa hawaonekani eneo hilo.

Mwandishi alifika mapokezi kwa ajili ya taratibu za kupata taarifa hizo na chanzo cha mgomo huo alimsikia mwanafunzi mmoja akimuomba mwalimu wa kike ruhusa “madam kama hatusomi mturuhusu turejee nyumbani mapema”

Hata hivyo uongozi wa shule hiyo haukuwa tayari kuzungumzia suala hilo lakini Mwana HALISI ilipata nafasi ya kuzungumza na walimu wa shule ambao walikuwa wamejikusanya pamoja kwenye jengo la nyuma wakisisitiza kuwa wamegoma kwa kile walichokidai kukithiri kwa ubaguzi na unyanyasaji.

Mwalimu Mohammed Haji mwalimu anayefundisha somo la Baiyolojia kwenye shule hiyo amesema kuwa shule hiyo ina waalimu wa kiafrika na walimu wanaotoka bara la Asia ambao wengi ni wahindi.

‘’Likifika suala la uamuzi, rangi inakuwa kigezo na wahanga wakubwa ni sisi watanzania, mpaka inafika kipindi tunakuwa hatuna imani na kesho yetu kwa sababu hapa unaweza kuzushiwa chochote kuchafuria CV zako mfano wale wenzentu waliosingiziwa kuvujisha mitihani.

“Mwaka jana kulitokea suala la kuvuja mitihani ambapo sisi tuna mashaka na kuvuja kwa mitihani hiyo lakini bila sababu yoyote walimu wa Kitanzania watatu waliangushiwa jumba bovu na kufukuzwa kazi, sisi ni watu wazima mambo yote yanayotokea hapa tunayaona,”amesema Haji.

Haji amesema kuwa ubaguzi huo umekwenda mbali mpaka kwenye masuala ya malipo kwa kuwa walimu wa kigeni wanalipwa kiwango cha juu mara nne zaidi ya kiasi cha Mtanzania ikiwa kiwango cha utendaji kazi ni sawa, “Tena walimu wa kitanzania wanafanya kazi zaidi”.

Anasema kuwa walimu wa Kitanzania hawaheshimiki, “ sisi walimu wa Kiafrika unaweza ukakemewa mbele ya wanafunzi na ukienda kulalamika unapewa onyo kali lakini hata kwenye ajira akiondolewa Mtanzania ataletwa raia wa kigeni na atapewa kiwango kikubwa cha mshahara.

“Tunanyanyaswa mpaka na walimu wenzetu wale wahindi wanatuona kama watu wa Second Class kwenye taasisi hii”

Issa Sumbi Mwalimu wa shule hiyo amesema kuwa ubaguzi huo unawaathiri na kwamba hivi karibu wameondolewa kazini walimu takribani watano bila kuwepo kwa sababu yoyote na waliojaza nafasi zao ni walimu wa kihindi.

Pamera Mboya Mwalimu wa TEHEMA katika shule hiyo amesema kuwa chanzo cha kuondolewa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ambaye alikuwa akisimama kutetea haki za walimu wa Kitanzania shuleni hapo kinaukakasi na kwamba wanahisi kuwa kuna shinikizo.

Samweli Kameme ni mmoja wa walimu wa The Agha Khan Mzizima amekiri kuwa uongozi wa shule huo unawabagua walimu hao wenye asili ya kiafrika.

“Unyanyasaji huu unafanyika kwa wazi kwetu sisi walimu kwa kubaguliwa na uongozi wa shule hususani Mkurugenzi wa shule anajua anachotenda hasa sisi walimu weusi , tunanyanyasika kwenye nchi yetu kwa kweli inauma”

“Mikataba inasitishwa bila sababu za msingi, wakiondolewa kazini walimu wa kiafrika wanaletwa walimu wenye asili ya kihindi tunaamini Rais Samia ataliona hili tunabaguliwa kwenye ardhi yetu,’ ameongeza.

John Kayoa Ofisa Rasilimali watu (HR) Msaidisi wa shule hiyo ambaye alimtaka mwandishi wa habari hizi aache maswali yake yote kwake ili siku inayofuata apate majibu.

Kayoa amesema kuwa kuhusu tuhuma za ubaguzi anaweza kuzisemea kidogo kuwa si za kweli.

“Unajua Mwandishi hapa kuna watu wanaotoka nchi tofauti tofauti na kila mtu anautamaduni wake hayo mambo hayana ukweli na kuhusu ajira kwa walimu wa kigeni sisi tunawaalimu zaidi ya 103 kwenye hao walimu raia wa kigeni ni walimu 13 tu,” amesema.

MWANAHALISI
Trust me.
This regime hakuna lolote litafanyika na sana sana, waalimu wataombwa kuvumilia changamoto hizo huku serikali ikichunguza.

Ripoti hiyo itatoka baada ya ile ya kuungua Soko la Kariakoo
 
Africa tumekuwa wakulalamika sana,,, unabaguliwa na still bado unataka kuendelea kukomaa hapohapo...

Unampangiaje mtu aliyewekeza pesa zake namna ya kuzitumia..?? ukiona mshahara mdogo acha kazi nenda kapambane.... kwanini uishi kitumwa kwenye taifa lako....
 
Kwangu mimi Ubaguzi ni muhimu, bila ya ubaguzi utabaguliwa, ubaguzi siyo mbaya na hapa sisi kama Watanzania weusi ni lazima tujifunze kujiweka mbele kwanza ya kila asiye mweusi kama sisi kwani wengine wote wanafanya hivyo na ndio maana hakuna Muhindi yoyote au Mwarabu ambao mnawatetea kuwa ni“Watanzania“ wana uhusiano wowote ule na wewe au mimi ukiondoa business na hata hiyo yenyewe ni lazima utakuwa na cheo Serikalini au kwenye Shirika la Umma ambapo anajua atakutumia na kukudanganya afaidike lkn linapokuja swala la Familia au urafiki wa maana na wa kudumu wako wao kwa wao wanaoana wao kwa wao wanaishi kwenye maeneo yao na hata wako loyal kule walipotoka na ndo maana kaita Kampuni yake Caspian, ulishawahi kujiuliza Wahindi waliojazana sasa hivi kwenye Viwanda wanatokea wapi na nani anawaleta ? Siongelei waliozaliwa hapa naongelea wanaotokea India leo na kuja kufanya kazi viwandani, nani anawaleta kama hawa akina Mo ni Watanzania wenzenu kama mnajilazimisha kuamini?
Sijui unazungumzia uhusiano gani, Mimi Mbantu, wewe pengine Nilotic kuna mwingine Cushites unazungumzia kipi. Mimi sitetei Mwarabu au yeyote yule, nachokataa ni kutumia card ya ubaguzi kubagua. Ukibagua wewe akibagua Mwarabu, Muhindi kosa ni lille lile.
Sijui kama ulishawahi kufika Nchi kama Rwanda au Cameroon ukaona ubaguzi ulipowafikisha.

Caspian ina uhusiano gani na asili ya Mtu? Vipi TAIFA GAS? Vipi IPP?
 
Sijui unazungumzia uhusiano gani, Mimi Mbantu, wewe pengine Nilotic kuna mwingine Cushites unazungumzia kipi. Mimi sitetei Mwarabu au yeyote yule, nachokataa ni kutumia card ya ubaguzi kubagua. Ukibagua wewe akibagua Mwarabu, Muhindi kosa ni lille lile.
Sijui kama ulishawahi kufika Nchi kama Rwanda au Cameroon ukaona ubaguzi ulipowafikisha.

Caspian ina uhusiano gani na asili ya Mtu? Vipi TAIFA GAS? Vipi IPP?

Watanzania >98% ni Wabantu, hivyo ubaguzi kwangu mimi ni upendeleo wa Makusudi kwa majority, kwa maana nyingine Uchumi na fursa hapa Tanzania ni lazima ziende kwa Watanzania wenye asili ya hapa ambao ndio wengi, sisi weusi ndio tumiliki njia kuu za Kiuchumi na minority kama Waarabu, Wahindi, Wazungu, Wachina na wengineo wasio asili ya Afrika wawe chini yetu na hilo linawezekana tu kama kukiwa na hatua za makusudi kabisa kutoa upendeleo kwa watu wetu kwenye kila kitu kuanzia mikopo benki, ajira, uongozi mpaka kwenye Sanaa na Michezo timu zetu zimilikiwe na sisi na siyo Waasia au Waarabu kama ilivyo leo hii, huo ndio ubaguzi ninaouongelea.

Na Nchi zote zilizoendelea Dunia zimefanya hivyo, unafikiri kwa nini AK kuna Black empowerment Programm iliyoanzishwa na Serikali ya Thabo Mbeki ?
 
Waafrika ni watu pekee ambao wanalia kubaguliwa na kila mtu hata kwenye nchi yao, once again takwimu zinasema Wahindi Tanzania ni 85% ya Uchumi wa Tanzania.
Kuna kitu hakipo sawa hapo, kwa hali ya kawaida Muhindi ndiye aliyepaswa kulalamika kubaguliwa Tanzania na siyo kinyume chake.

Kuna watu wanamtetea Rostam wanasema ni mwenzao lkn yeye Rostamu hawaoni hivyo!
Hili ni jambazi kuu tz ..mpaka tembo wetu wanamjua ccm kimechukuliwa na kuwa mali na kampuni ya wahindi na waarabu sasa hivi pesa za serikali uetu ni mali zao wanachota tu ...hakina singasinga , gsm ,ristam ,zungu , samia nk haya yote kayaleta mzee wa msoga
 
Daah, nimesoma hapo 2003 - 2006. Ila Sikuwahi kukutana na ubaguzi wa rangi kiukweli, labda kama ndio wameanza sasa.

Ila nilichogundua kwa wanafunzi wa kihindi ni wivu kwa wenzao waKiafrika pale wanapofanya vizuri zaidi yao kwenye mitihani. Yaani ukishika namba moja darasani basi utaona wanavyokuangalia kwa jicho la husda, yaani ni kama hawategemei Muafrika awe bright kuliko wao
Ulisoma wakati wa Mr thind au

Ova
 
Misingi ya kikoloni ilishaweka hiyo mizizi, jitihada za ziada zinahitaji kupindua meza kwa kweli
Slave mentality
Maujinga haya did amin
Ndy alikataaga akawatimua
Na yote kwa sababu wao wanajiona
Kiuchumi wako vzr
Ndomana inabadi wabongo asilia wapambane wawe na uchumi mkubwa,hebu angalia top 10 ya matajiri bongo,tuangalie wabongo wanao miliki viwanda vikubwa ni wangapi

Ova
 
Na Nchi zote zilizoendelea Dunia zimefanya hivyo, unafikiri kwa nini AK kuna Black empowerment Programm iliyoanzishwa na Serikali ya Thabo Mbeki ?
Jaribu kufikiri tena.

Hicho unachosema ni BLACK EMPOWERMENT kwa AK hakijasaidia kivyovyote kuwezesha wazawa ambao ndio wengi.

Uchumi wa AK bado uko mikononi mwa Wazungu
 
Sina hakika kama Serikali yetu italishughulikia!
Wahindi wasikie tu ni Wabaguzi wa kutupwa.Kule kwao tu nasikia wanaishi kwa matabaka.
The late Mtikila ndiye alikuwa anawaita Magabacholi miaka ile ya 85's
 
Hili suala sio la kuvumilia kabisa..yani ndani ya nchi yako bado unanyanyasika utoke uende kwenye nchi zao nako unyanyasike...hii si sawa.

Kama serikali imeshindwa kusimama na kukemea wazi wqzi vitendo hivyi vya ubaguzi ifike hatua wananchi tuanze kuwanyoosha hawa ma gabachori.


#MaendeleoHayanaChama
Sio Serikali tu wakulaumu, hata vibaka wezi na majambazi, wamewafumbia mno macho hawa ushindi.. Na hatusikii panyaroad wakifanya yao kwa hawa watu..
 
Jaribu kufikiri tena.

Hicho unachosema ni BLACK EMPOWERMENT kwa AK hakijasaidia kivyovyote kuwezesha wazawa ambao ndio wengi.

Uchumi wa AK bado uko mikononi mwa Wazungu

Lakini angalau wamejaribu, huwezi kumaliza na kuondoa hali iliyodumu kwa miaka zaidi ya 100 ndani ya muda mchache, angalau AK wao walikaliwa kwa mabavu sisi kila kitu ni chetu lkn bado tunashindwa kujipendelea na kujiwezesha kumiliki njia zote za Kiuchumi kwenye Nchi yetu!
 
Jaribu kufikiri tena.

Hicho unachosema ni BLACK EMPOWERMENT kwa AK hakijasaidia kivyovyote kuwezesha wazawa ambao ndio wengi.

Uchumi wa AK bado uko mikononi mwa Wazungu
Tena hiyo black empowerment ndiyo balaa zaidi. Watatajirika 'weusi' wenzetu wachache na dinner wanakutana na hao weupe kupiga stori (kwa sababu ndiyo level yao).

Hapa Tanzania alikuwepo mmoja mpigania uzawa na Mzee wetu marehemu. Kuna wakati alipigapiga sana kelele, Rais Mwinyi kipindi hicho akampa kiwanja hapo ilipo Serena Hotel, baada ya muda akawauzia haohao aliokuwa akiwalaumu!
 
Back
Top Bottom