robbyr
Senior Member
- Apr 8, 2017
- 129
- 221
Picha: Pinterest
Upendo wa mwalimu si kumfundisha mtoto tu bali hata kulinda heshima na hisia za mtoto kwa kuweka siri au faragha za wazazi wake.
Usitumie makosa ya mtoto na kufananisha na matendo ya mzazi au wazazi wake hasa yale ambayo si chanya kwenye jamii kwani kwa picha yake na jinsi anvyojitambulisha mbele yake inaweza kuharibika kwa kushindwa kujiamini na hata kujihisi hawezi kufikia ndoto yake.
Ila unaweza kutumia mambo yale chanya wazazi wanayofanya kwenye jamii ili kumuonyesha na yeye anaweza kufikia ndoto yake na kutoa mchango bora kama wazazi katika jamii na taifa kama atazingatia nidhamu, bidii n. k
Asante.