Walimu wa arts jiandaeni kisaikolojia

Walimu wa arts jiandaeni kisaikolojia

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,917
Reaction score
11,801
Nipo field huku nimejaribu kuzungukia shule nyingi za kata zimepata mgao wa walimu mpaka 7 wa masomo ya art ukijumlisha na wale zamani unakuta shule ina walimu 15 wa arts hasa masomo ya History,kiswahili,geography wakati huo huo shule ina wanafunzi 200 kila darasa mkondo 1 ni dhahiri walimu wa masomo ya art wametosha mliopo vyuoni jiandaeni kisaikolojia.
 
Research yako ya kata moja usifanye conclusion ya nchi nzima na kuvunja wenzako moyo.

Walimu mliopo vyuoni msivunjike moyo hata mwaka jana yalisemwa hivi hivi lakini sasa hivi watu wapo kwenye ajira!
 
Walimu Wa Sanaa wamejaa Sana mpaka baadhi ya halmashauri zinataka wapunguzwe.....

Huu ni mwaka Wa mwisho kwa ajira za arts subjects.....
 
Ya Meru ndo inatisha sanaa walipangwa na TAmisemi walimu780 ambao wamepangiwa vituo ni 709 tu wengine watapelekwa kungine kama Longido nk.. kuna baadhi ya Shule huku Meru wamepata walimu wapya mpka47,41,42 37 nk
 
Hao 47 unakuta 30 ni wa kiswahili.... Hahaaaaa walimu mkale bata tu...
 
mfano mara sec kuna walimu kama 65 kwaiyo nikugawana topics tu
 
Mimi nimepangiwa shule fulani hapa Geita nimepewa form two geog. Vpnd 3 kwa wiki yaani dk 120 tgts in
 
Tureshapoteza mwelekeo wizara ya elimu,mamboya ndani,next afya
 
Naona wazushi washaanza prediction kama kawaida yao hivi nyie watu hamchoki kujadili ajira za ualimu mtafikiri nyie ndo serikali nataka niwaambie waalimu walioko vyuoni msiwe na wasiwasi sababu serikali ndio inaajiri na haijasema ajira za walimu wa masomo ya sanaa zimekwisha hivyo kama ajira hazitakuwepo mtaarifiwa na mamlaka husika na sio hawa wazushi wa hapa jf.
 
Ajira za ualimu kwa masomo ya Sanaa mwisho!!! Walimu wamejaa huko halmashauri mpaka wanakosa pa kwenda!!!
 
Ajira za ualimu kwa masomo ya Sanaa mwisho!!! Walimu wamejaa huko halmashauri mpaka wanakosa pa kwenda!!!

Huo ndio ukwelii ila nimefurahi kuona wameajiri graduate wengi kwaiyo najua walimu kudai haki sasa wawe sawa na wafanyakazi wa kada nyingine inawezekana maana jana tu nimeona Arumeru wameriot safi sanaaa yanii.Zaman walimu wengi walikua wale wazee hata kudai haki hawajui.
 
Meru wameshindwa kuwaajili walimu.Halafu kuna taarifa kuwa pana afisa utumishi mnyanyasaji sana.Hebu mliopo Meru tujulisheni kuhusu mtu huyo.
 
Meru wameshindwa kuwaajili walimu.Halafu kuna taarifa kuwa pana afisa utumishi mnyanyasaji sana.Hebu mliopo Meru tujulisheni kuhusu mtu huyo.

Ni mtu wa ajabu sanaa huyo jamaa dharau kwa sanaa
 
walimu wa arts walishatosha nadhani kwa sababu ni mwaka wa uchaguiz wameonewa huruma mwakani itakuwa kasheshe kidogo
 
Back
Top Bottom