KERO Walimu wa Kibaha tulioajiriwa 2014 tupo nyuma kwa Daraja moja, Tume ya TSC inatuambia tuwe wapole

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mwalimu wa Manispaa ya Kibaha, kero yangu kubwa ni kuhusu madaraja ya ngazi ya mshahara, sisi tulioajiriwa Mwaka 2014 tupo nyuma kwa daraja moja.

Mpaka sasa kwa muda tuliokaa kazini tungetakiwa tuwe tumefikisha Mwl Daraja G lakini tupo Mwl Daraja F na hii ni kwa Walimu wote Tanzania.

Mamlaka husika wasikie kilio chetu maana maisha ni magumu sana kwani wengine wetu tuna majukumu makubwa kwenye, familia kulingana na umri wetu.

Pia, tumekuwa tukiulizia kwa viongozi wetu wa Tume ya Utumishi wa Walimu na TSC Wilaya wamekuwa wakitupa majibu ya kukatisha tamaa kwamba siyo sisi tu tulioachwa nyuma ni Tanzania nzima kwa hiyo tuwe wapole.
 
Mlikuwa mnampigia makofi magufuli huku akibinya stahiki zenu
 
nadhani wewe ni mwalimu mbinafisi,unapenda kuwasilisha hoja kwa upande wako kisa uko na degree ndo maana unasema Toka F kwenda G,kumbuka hiyo shida iliwapata walimu wote,kuanzia grade A,diploma na shahada,hivyo kama diploma yuko E alipaswa kuwa F,pia grade A ambaye yuko daraja D alipaswa kuwa E.

Kuweka kumbukumbu sawa,ninyi mlipanda daraja kwa mara ya kwanza 2021, na baadae 2024,sasa utaliliaje daraja wakati hujatimiza vigezo vya kuwa kwenye daraja eidha E ,F au G ambavyo ni miaka mitatu Toka daraja la mwisho,hivyo ninyi mnapaswa kupanda mwaka 2027.

Walimu tupunguze kulia Lia,wewee umekopa huko unakuja kulia Lia hapa upande daraja la Bure ulidhani litasaidia ugumu wa maisha.

Kaa kwa kutulia
 
Mimi ni Mwalimu wa Manispaa ya Kibaha, kero yangu kubwa ni kuhusu madaraja ya ngazi ya mshahara, sisi tulioajiriwa Mwaka 2014 tupo nyuma kwa daraja moja.

Mpaka sasa kwa muda tuliokaa kazini tungetakiwa tuwe tumefikisha Mwl Daraja G lakini tupo Mwl Daraja F na hii ni kwa Walimu wote Tanzania.

Mamlaka husika wasikie kilio chetu maana maisha ni magumu sana kwani wengine wetu tuna majukumu makubwa kwenye, familia kulingana na umri wetu.

Pia, tumekuwa tukiulizia kwa viongozi wetu wa Tume ya Utumishi wa Walimu na TSC Wilaya wamekuwa wakitupa majibu ya kukatisha tamaa kwamba siyo sisi tu tulioachwa nyuma ni Tanzania nzima kwa hiyo tuwe wapole.
Kwani pale Dodoma juzi hamkusema kwenye kikao chenu na maCCM? Someni namba hizo
 
Back
Top Bottom