ministrant
JF-Expert Member
- Jan 17, 2014
- 754
- 1,478
Ashakum si matusi, ila nachelea kusema hao walimu wa lugha ni vilaza kupitiliza. Maana kuna jamaa kadhaa ni walimu wa lugha na nipo nao kwenye kundi sogozi lakini wao wenyewe wana changamoto kubwa katika uandishi wa Kiswahili, hawaelewi matumizi sahihi ya "Z" na "Dh", yaani pakuweka "dhana"anaweka "Zana" na kinyume chake, hawana weledi wa matumizi ya "h", sehemu ya kusema "habari" inawekwa "abali", "asubuhi" itaandikwa "hasubui".Hivi mtoto wa fomfour miaka 17 hadi 20 inakuwaje hawezi kutofautisha Kati ya "r" na "l"
"Karibu" mtoto anaandika " kalibu"
👉Kwenye matamshi ya lugha binafsi siwezi tupa lawama hii ni kutokana na athari za kimakabila/kilugha
Lakini swala zima la maandishi imekuwa ni changamoto sana
👉Matumizi ya 'x" badala ya s
Matumizi ya vifupisho kwa Kila neno
👉Matumizi ya neno "h" hayazingatiwi kabisa kwa baadhi ya maneno
Mfano "haraka" mtu anaandika "araka"
Nitoe Rai kwa walimu wa kiswahili
👉Naomba muwe wakali sana kwa wanafunzi wenu. Msiweke vema tu bali mzingatie sarufi.
👉Kama hamuwezi kuwa wakali ebu kagueni sana miandiko ya wanafunzi wenu ni aibu mtoto anakaa shule zaidi ya miaka 11 hajui maandishi ya kiswahili vizuri na ni lugha mama?
👉Mbinu ya mwisho, andaeni midahalo ya kiswahili, lakini pia mwalimu tumia njia ya uhamasishaji "hali" kwa kutumia zawadi kwa mwanafunzi mzuri zaidi.
Ona tu huu uandishi huu👇
Binafsi naona miaka kadhaa ijayo kiswahili sanifu kitapotea kwa kasi kama hizi lugha za asili