A
Anonymous
Guest
Nimekuwa mmoja wa Walimu wa mkataba (part-timers) katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo kazi yetu kuu ni kusaidia kufundisha wanafunzi wa kozi za Diploma ya Famasia (Pharmacy) na Diploma ya Maabara ya Tiba (Medical Laboratory Sciences) chini ya Shule Kuu ya Tiba (School of Medicine).
Wengi wetu tunatoka kwenye taasisi mbalimbali za afya mkoani Dodoma kama Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa na Chuo Kikuu cha St. John’s.
Tulipokea ombi la usaidizi kutoka kwa Wakuu wa Idara wa UDOM kwa sababu chuo kilikuwa na uhaba mkubwa wa walimu kwenye kozi hizi za diploma. Kwa moyo wa kujitolea na taaluma yetu, tukakubali.
Tulianza ufundishaji huu tangu mwezi Novemba 2025, na tukahitimisha mwezi Machi 2026, katika kipindi chote hicho cha miezi minne, nilikuwa najipanga vizuri:
Niliandaa kozi (course outline), nilishaingia madarasani na kufundisha kwa uaminifu, nilisahihisha mitihani ya mwisho ya chuo (University Examinations - UE), nilipandisha na kuwasilisha matokeo yote ya wanafunzi kama makubaliano ya kimkataba yanavyotaka.
Kulingana na mkataba wetu, mara tu unapokamilisha kufundisha na kuwasilisha matokeo, unapaswa kulipwa stahiki zako zote bila kuchelewa lakini kinachotutokea sasa hivi ni tofauti kabisa na makubaliano yetu!
Hakuna Hela: Kuta za Usimamizi na Majibu ya Ukimya
Tangu tumalize mwezi wa Tatu, sasa hivi ni mwezi wa nane, zaidi ya miezi minne imepita na hatujapewa hata sarafu moja!
Kila tukijaribu kufuatilia malipo yetu kupitia Idara ya Famasia na Microbiology, majibu tunayopewa ni yale yale: "Chuo bado hakijapata hela." Tukijaribu kumtafuta Mkuu wa Kitengo cha Tiba (Dean, School of Medicine), mara nyingi simu zetu hazipokelewi kabisa.
Ukiuliza kama kuna shida kwenye matokeo ya wanafunzi, unaambiwa hakuna shida yoyote. Tatizo ni moja tu hawana fedha za kutulipa sisi walimu zaidi ya 10 tuliowasaidia!
Gharama Zetu za Mfukoni na Athari za Kiuchumi
Watu wengi hawajui maumivu tunayopitia ili kufika darasani. Kampasi ya UDOM haipo karibu; kutoka mjini hadi kule ni zaidi ya kilomita 30.
Tulikuwa tunaendesha magari na kutumia vyombo vyetu vya usafiri, tulikuwa tukanunua mafuta kwa fedha zetu wenyewe za mifukoni tukiamini tutarudishiwa kwenye malipo yetu, leo hii nauli na gharama za mafuta tulizotumia zinatutesa, huku chuo kikiwa kimya!
Kitu kinachoumiza zaidi ni kwamba hii si mara ya kwanza. Mwaka 2025 pia ilitokea hali hii hii tulimaliza kufundisha mwezi wa Nane, tukaja kulipwa mwezi wa Kwanza mwaka uliofuata (baada ya miezi 5).
Inavyoonekana, uongozi unataka kujirudia tena kwenye mtindo huo huo wa kutuweka njaa kwa miezi nenda rudi.
Hivi kweli ni haki mwalimu utumie mafuta yako, usafiri kilomita 30, ufundishe, usahihishe mitihani, utoe matokeo, alafu ukae miezi minne au mitano bila kulipwa stahiki zako?
Tunaomba sana uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na mamlaka zinazohusika zitutazame kwa jicho la huruma na kutulipa jasho letu. Tunafanya kazi hii kwa mapenzi na taaluma yetu, lakini mazingira haya yanavunja sana morali yetu ya kufundisha!