A
Anonymous
Guest
MHESHIMIWA WAZIRI.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mji wa Serikali Mtumba Mtaa wa Utumishi.
S.L.P 670.
DODOMA, TANZANIA.
Yah: MAPUNJO YA DARAJA KWA WALIMU WALIOAJIRIWA MWAKA 2014.
Husika na somo tajwa hapo juu.
2. Kwa heshima kubwa, nakuandikia barua hii kwa niaba ya Walimu tuliyoajiriwa katika Utumishi wa Umma ( ngazi ya Shahada) mwaka 2014, tunawasilisha ombi hili mbele yako tukiiomba Serikali itazame kwa karibu changamoto ya kiutumishi iliyotokana na kuchelewa kwetu kupandishwa madaraja kwa wakati uliostahili.
3. kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 [Public Service Act, Cap. 298], Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003,kanuni na. 8 ya Teachers Service Commission Regulations, 2016 pamoja na Local Government (Teachers’ Service) Scheme, 2016, maendeleo ya mwalimu katika kada hutegemea uzoefu, muda wa utumishi, sifa pamoja na utendaji kazi. Aidha, kwa mujibu wa Mwongozo wa Miundo ya Utumishi wa Kada za Walimu (Teachers Service Scheme), mtumishi aliyethibitishwa kazini hustahili kupandishwa daraja baada ya kipindi maalum kwa kuzingatia masharti ya kada na utendaji wa kazi ulioridhisha. Kwa msingi huo, sisi walimu tulioajiriwa mwaka 2014 tulitarajia kupandishwa madaraja kama ifuatavyo:-
5. Tunatambua na kuthamini juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali katika kipindi cha uhakiki wa watumishi wa umma. Hata hivyo, baada ya uhakiki huo kukamilika, athari zilizotokana na kusimamishwa kwa upandishaji madaraja zimeendelea kubaki upande wetu bila kufanyika marekebisho ya kurejesha progression ya kawaida ya kada.
Kutokana na hali hiyo, sisi walimu walioajiriwa mwaka 2014 tunaomba Serikali yako itafakari kwa huruma na haki ya kiutumishi kufanya marekebisho yafuatayo:

- Kupanda daraja kwa mara ya kwanza mwaka 2018 -kutoka daraja D kwenda E
- Kupanda daraja kwa mara ya pili mwaka 2021- kutoka daraja E kwenda F
- Kupanda daraja kwa mara ya tatu mwaka 2024 - kutoka daraja F kwenda G
5. Tunatambua na kuthamini juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali katika kipindi cha uhakiki wa watumishi wa umma. Hata hivyo, baada ya uhakiki huo kukamilika, athari zilizotokana na kusimamishwa kwa upandishaji madaraja zimeendelea kubaki upande wetu bila kufanyika marekebisho ya kurejesha progression ya kawaida ya kada.
Kutokana na hali hiyo, sisi walimu walioajiriwa mwaka 2014 tunaomba Serikali yako itafakari kwa huruma na haki ya kiutumishi kufanya marekebisho yafuatayo:
- Kufanya mapitio ya maendeleo yetu ya kada kwa kuzingatia muda halisi wa utumishi tulionao;
- Kutupandisha madaraja kwa mserereko au kufanya marekebisho yatakayorejesha seniority yetu ya kiutumishi;
- Kurekebisha tofauti iliyojitokeza ya kufanana madaraja kati yetu na baadhi ya watumishi walioajiriwa baada yetu;