Walimu wa vyuo vikuu ambao hawajawahi kufanya kazi katika field wanazofundisha, wanaweza kuwa walimu wazuri?

Walimu wa vyuo vikuu ambao hawajawahi kufanya kazi katika field wanazofundisha, wanaweza kuwa walimu wazuri?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Habari wakuu,

Kuna jambo moja huwa najiuliza kuhusu walimu (wahadhiri) wa vyuo vikuu ambao tangu wamalize shahada zao za kwanza na kufanya vizuri, hawajawahi kufanya kazi katika taaluma walizosomea lakini wanaendelezwa/wanajiendeleza mpaka kufikia kupata Doctorate au Uprofesa na kurudi vyuoni kuendelea kurudisha kama wanaweza kuwa walimu wazuri wa kuwapa wanafunzi wao maarifa.

Hawa ni wale ambao hubakizwa vyuoni baada ya kupata ufaulu wa juu na kuanza kusimamia seminars kisha wakipata masters wanakuwa Assistant Lecturers then Lecturers baada ya kupata PhD na hata kuwa professor baadae ila hawajawahi kufanya kazi zaidi tu ya kuwa academicians.

Je, walimu hawa wanafaa kutoa maarifa yanayotakiwa ili wanafunzi wao waweze kuwa competent katika nadharia na zaidi katika vitendo?

Binafsi naamini kuwa through practice, kuna mambo mengi mtu unajifunza, mambo ambayo hata wanafunzi wako wanapaswa kufundishwa na hasa kama utakuwa ume-practise muda mrefu.

Ni imani yangu pia, mtu alie-practise anaweza kuandaa notes nzuri zaidi na hata kutoa assignment/test zitazomsaidia mwanafunzi kwenye field husika na pia kutunga maswali/ mitihani yenye uhalisia zaidi na kile ambacho mwanafunzi wake atakutananacho field.
 
Wapo wengine wazuri sana hata kama hakupitia field ya ufundishaji. Chukua hata f6 leavers wanaofundisha kwa kujitolea au tuition wengine wako vizuri sana kwenye ufundishaji na wakaeleweka kuliko hata walimu wenyewe.

Pia wapo walimu kwa weledi katika ufundishaji na bado deliverance ni hafifu hata kutoeleweka kwa wanafunzi. But all in all, uweledi na uzoefu una umuhimu na nafasi yake ktk ufundishaji.
 
Nadhani unaongelea UDSM hasa, kufundisha kwa vitendo nadhani ni kwa vyuo vya ufundi na udaktari, nadharia inapanua uwezo wa mtu kufikiri sio kuweza tu kupanga ma file ofisini.
 
Nimefanya kazi mara nyingi na engineers waalim UDSM, aisee ni weupe sana field. Nimeona hilo gap mwakani nitajaribu kuomba kazi ya kufundisha Mzumbe au UDOM niweze kuwasaidia vijana
 
Ma lecturer wazuri huwa ni wale wenye background za education walioanza kufundisha shuleni kwanza. Hawa wanaobakishwa chuoni kwa GPA kubwa huwa hawawezi ku deliver Mambo na wakaeleweka wao huwa ni mwendo wa kusoma madesa na hawataki kuulizwa maswali. KWA uzoefu wangu chuoni nili waelewa wahadhiri waliopitia education kiurahisi zaidi.
 
Nadhani unaongelea UDSM hasa, kufundisha kwa vitendo nadhani ni kwa vyuo vya ufundi na udaktari, nadharia inapanua uwezo wa mtu kufikiri sio kuweza tu kupanga ma file ofisini.
Hata hyo nadharia inabidi mtu awe ame ki practice akielezea Ina sound good, kuliko kusoma hizo nadharia kitu ambacho hata mwanafunzi anaweza kusoma. Ni sawa na kuwa na prof wa ujasiriamali huku hajawahi kuwa na genge la vitu.
 
Hivi ni vipawa vya watu, mtu anaweza bakizwa na akawa mwalimu Bora kabisa bila hata background ya education.
 
Hata hyo nadharia inabidi mtu awe ame ki practice akielezea Ina sound good, kuliko kusoma hizo nadharia kitu ambacho hata mwanafunzi anaweza kusoma. Ni sawa na kuwa na prof wa ujasiriamali huku hajawahi kuwa na genge la vtu
Hapa ndo changamoto walimu wengi wako theoretically zaidi, practical hamna kitu.
 
Kwa Mkufunzi kua na field experience ni bora mara elfu moja hata kama una kipawa cha kufundisha. Unakua huna vivid examples zaidi ya zile ulizoona kwenye madesa.
 
Most of my teachers in college didn't have industrial experience and when I look back I think it wasn't necessary for a couple of reasons. First, my teachers didn't prepare me to be a worker, but rather a thinker. By thinker, I mean a person who can take a new issues on his own and try to find solutions from multiple sources.

They understood that the world is changing very fast and whatever they teach me will be history the time I finish my studies. Second, teachers in my school were required to engage in current research works which keep them abreast with current development in the areas of their disciplines. Third, fundamentals in many disciplines have already been discovered or worked out. The only thing you miss from field experience is the application of those fundamentals in real life. For a very smart teacher that isn't a big deal.
 
Wanakuwa walimu waziri tu,wanakufundisha nadharia vzr kabisa,mfano kwenye uhandisi, uwezi ku design kitu Kama huna nadharia ya kutosha kwenye taaruma yako

Kwahiyo lazima upikwe vzr ki nadharia, kwenye vitendo hapo,wapo walimu wanaoajiriwa kwa ajri ya kazi hiyo, wao watakupa shule ya vitendo

Walimu wazuri wa nadharia ndio roho ya vyuo vikuu.
 
mleta mada ume pose swali zuri sana litakalohitaji kutafakariwa na mamlaka zetu za elimu. Mfano nilifanya utafiti kidogo kwenye sekta ya elimu niliona walimu waliotoka f6 na kwenda diploma ya education walikuwa competent mno kudeliver kuliko walioenda kuchukua degree ya education.

Sababu kubwa niliona kuwa ni aina ya walimu waliowaandaa, mode ya kuandaliwa kwao na pia practical aspect.

Kama kuna kitu Taifa hili na watawala wetu wanatakiwa kulaumiwa kwacho ni kuucheza na mfumo wetu wa elimu,
 
Back
Top Bottom