Walimu waajiriwa wa 2011 tukutane hapa, Serikali imetusahau

Jamani tuwasililize walimu wetu mkiandamana nitawaunga mkono lianzisheni
 
Mleta Mada unatafuta sifa za Kijinga, Walimu wanachombo chao cha kudai maslahi yaan CWT sasa kesho au kesho kutwa uking'olewa meno bila ganzi au ukutwe Mabwepande kama kiongoz wa Vijana wa JKT, kama Ulimboka na wengineo wengi utamfaidisha nani? Tufuate taratibu za kudai maslahi yetu. Vingnevyo ni Umbumbu na Ulimbukeni tu, haya tumekujua wewe ni mwajiriwa sie wakulima basi.
 
Woga wako ndiyo Umaskini wako
 
walimu kweli mna matatizo makubwa ya kiakili, kwani simeahidiwa JULY, sasa mbona mshaanza kulialia na wakati julai yenyewe haijafika.
Hebu kafundishe huko acha kuwashushia hadhi walimu.

Naona unedandia treni kwa mbele. Hujui hata kinachozungumzwa hapa, ni bora ungeomba ufafanuzi kwanza.
 
Na wewe nenda kapewa salamu za Good morning teacher..........afu unaitikia goodmorning sit down,,,,,,,,,,,
 
Samahani kwa kuingiza maada tofauti,nyie waalimu ndio mpo mashuleni,tunaomba mtusaidie kitu kimoja

Ni juzi tu selection za kidato cha tano zimetoka,na ni muda mfupi hawa vijana wanatakiwa waripoti shule..Barua za maelekezo ya kujiunga huwa zinachelewa sana posta,tusaidieni kuziattach hapa itawasaidia sana

Wakuu wa shule mnaopita humu tusaidieni kwa hili
 
Naunga mkono hoja mnastahili kulipwa stahiki yenu.Wasipowawekea hayo madaraja, tafakari mwezi October 25.
 
2011 serikali ilitoa ajira kwa walimu?

Kama serikali haikuajiri walimu 2011, basi uzi huu usingefika page ya 3, wanaochangia wengi na mleta uzi ni waajiriwa wa 2011.
 
Kuna watu ufikiri wao ni mdogo sana, mfano sw...e, utafikiri anatumia ta..o kuchambua mambo, kunamahali umeelekezwa uandike utumbo wako k..nge we, back to the topic, wakuu subulini upite mwezi wa saba ndo msale, baadhi ya h/w zinaogopa kulimbikiza madeni ndo maana hazitoi barua kabla ya mishahara kupanda,
 
Kama serikali haikuajiri walimu 2011, basi uzi huu usingefika page ya 3, wanaochangia wengi na mleta uzi ni waajiriwa wa 2011.

Kufika page ya 3 haithibitishi unayoyasema,huo ni uongo,serikali haikuajiri mwaka huo taja ila toka ajira za October 2010,zikafuata za Feb 2012,halafu tambueni hata wa 2010 kuna baadhi ya halmashauri hawajapandishwa madaraja,sembuse nyie.
 
Teh teh...mkuu we muongo!! Mi nawafahamu walioajiriwa mwaka huo alafu unabisha!!....
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Katika mwaka wa masomo 2009/10 jumla ya wanafunzi 19,652 walihitimu mafunzo ya ualimu wakiwemo ngazi ya shahada 12,120 na stashahada 7,532. Kati ya wanafunzi hao jumla ya wanafunzi 17,684 walihitimu na kufaulu masomo yao, wenye shahada wakiwa 12,095 na wenye stashahada 5,589.

Uchambuzi wa sifa za wahitimu 17,684 waliohitimu na kufaulu mitihani yao umeonesha kuwa jumla ya wahitimu 8,857 wametoka kazini (in-service). Idadi hiyo inajumuisha wenye shahada 7,437 (25 kutoka Zanzibar) na wenye stashahada 1,420. Walimu hao wamerudi kwa waajiri wao ili wapangiwe kazi kulingana na elimu yao. Aidha, kuna wahitimu 328 kutoka Zanzibar (wakiwemo 303 tarajali na 25 kutoka kazini) ambao wanatarajiwa kuajiriwa katika shule na vyuo vya Zanzibar. Hivyo, wahitimu wanaobakia ambao wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu Tanzania Bara ni 8,524 wakiwemo wenye shahada 4,355 na wenye stashahada 4,169.

Kama ilivyobainishwa katika sehemu ya kwanza ya taarifa hii, jumla ya wahitimu 8,524 waliohitimu na kufaulu mitihani yao wataajiriwa na Serikali katika mwaka huu wa fedha. Vilevile Serikali imekubali kuajiri walimu 702 (wakiwemo 565 wenye shahada na 137 wenye stashahada) waliomaliza mafunzo yao miaka ya nyuma ambao wameomba kuajiriwa Serikalini.

Hivyo, jumla ya walimu wote watakaoajiriwa Serikalini kwa mwaka wa fedha 2010/2011 ni 9,226 wakiwemo wenye shahada 4,920 na wenye stashahada ni 4,306. Kati ya walimu watakaoajiriwa jumla ya walimu 9,039 wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na walimu 187 wamepangwa kufundisha katika vyuo vya ualimu.

Walimu wote wa shule za sekondari wamepangwa katika Halmashauri mbalimbali kwa kutumia kigezo cha upungufu wa walimu katika Halmashauri husika. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kuripoti katika Halmashauri aliyopangwa kwa kuwa fedha za mshahara wake zimekasimiwa kwenye Halmashauri alikopangwa na si vinginevyo. Orodha ya walimu hao na Halmashauri walikopangwa zimetumwa kwenye Mikoa na Halmashauri. Aidha, orodha hiyo inapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) na tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (www.pmoralg.go.tz).

Walimu wote wapya wanaagizwa kuhakikisha kwamba wanaripoti katika Halmashauri/ Vyuo vya Ualimu walikopangwa ifikapo tarehe 24/01/2011. Watendaji na wasimamizi wa elimu kwenye Halmashauri na Vyuo vya Ualimu watakuwepo kuwapokea.

Mwalimu yeyote atakayeshindwa kuripoti kwenye Halmashauri / Chuo alikopangwa baada ya siku saba (7) tangu tarehe anayotakiwa kuripoti atahesabika kuwa amekataa kukubali nafasi ya ajira aliyopewa na Serikali.

Baada ya kuripoti kwenye Halmashauri/Vyuo waajiri watatakiwa kuwajazia walimu hao Fomu maalum zenye Taarifa ya Kiutumishi ya Mtumishi (Personal Data Form) na kuziwasilisha Ofisi ya Rais, UTUMISHI pamoja na barua ya ajira ya mtumishi. Taarifa hizo zikiwa katika “hard” na “soft copy” ziwasilishwe UTUMISHI kabla au ifikapo tarehe 29/01/2011 ili watumishi hao waingizwe katika mfumo wa malipo (Payroll). Waajiri wanakumbushwa kwamba “Computer Data Sheet” hazitahitajika katika zoezi hili.

Waajiri (Wakurugenzi wa Halmashauri na Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi) watawalipa malipo stahili kwa mujibu wa nyaraka na miongozo ya Serikali kuhusu waajiriwa wapya.

Nawatakia utumishi mwema katika Sekta ya Elimu.

Imetolewa na:

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

MUHIDIN MICHUZI at Sunday, January 16, 2011
 
Bora umenisaidia ndugu maana wengine hatuna muda wa kubishana.
Labda nimshauri arejee mkataba wake yeye na mwajiri alisaini tarehe/mwezi/ mwaka gani anaweza jua wapi pa kuanzia.
Labda kama nimemuelewa vizuri aseme aliajiriwa october 2010. Akathibitishwa 2011. Lakini 2011 serikali haikuajiri walimu. Walimu walio hitimu 2011 waliajiriwa february 2012.
 
Bora umenisaidia ndugu maana wengine hatuna muda wa kubishana.
Labda nimshauri arejee mkataba wake yeye na mwajiri alisaini tarehe/mwezi/ mwaka gani anaweza jua wapi pa kuanzia.

Mkuu umefanya utafiti!?
 
Na usijidanganye kwakuwa uzi umefika page sijui ya ngapi ukajua kila mchangiaji hapa ni Mwalim, wengine ni wapita njia tu ndio maana ukichambua mawazo yao hayana weledi ndani yake.
 
Mkuu umesoma taarifa nilioweka hapo juu?
...huonyeshi kukubali kuwa kulikuwa na ajira za waalimu 2011... Ukweli ni kwamba kulikuwa ajira za walimu mwaka 2011...
 
Teh teh...mkuu we muongo!! Mi nawafahamu walioajiriwa mwaka huo alafu unabisha!!....
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Katika mwaka wa masomo 2009/10 jumla ya wanafunzi 19,652 walihitimu mafunzo ya ualimu wakiwemo ngazi ya shahada 12,120 na stashahada 7,532. Kati ya wanafunzi hao jumla ya wanafunzi 17,684 walihitimu na kufaulu masomo yao, wenye shahada wakiwa 12,095 na wenye stashahada 5,589.

Uchambuzi wa sifa za wahitimu 17,684 waliohitimu na kufaulu mitihani yao umeonesha kuwa jumla ya wahitimu 8,857 wametoka kazini (in-service). Idadi hiyo inajumuisha wenye shahada 7,437 (25 kutoka Zanzibar) na wenye stashahada 1,420. Walimu hao wamerudi kwa waajiri wao ili wapangiwe kazi kulingana na elimu yao. Aidha, kuna wahitimu 328 kutoka Zanzibar (wakiwemo 303 tarajali na 25 kutoka kazini) ambao wanatarajiwa kuajiriwa katika shule na vyuo vya Zanzibar. Hivyo, wahitimu wanaobakia ambao wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu Tanzania Bara ni 8,524 wakiwemo wenye shahada 4,355 na wenye stashahada 4,169.

Kama ilivyobainishwa katika sehemu ya kwanza ya taarifa hii, jumla ya wahitimu 8,524 waliohitimu na kufaulu mitihani yao wataajiriwa na Serikali katika mwaka huu wa fedha. Vilevile Serikali imekubali kuajiri walimu 702 (wakiwemo 565 wenye shahada na 137 wenye stashahada) waliomaliza mafunzo yao miaka ya nyuma ambao wameomba kuajiriwa Serikalini.

Hivyo, jumla ya walimu wote watakaoajiriwa Serikalini kwa mwaka wa fedha 2010/2011 ni 9,226 wakiwemo wenye shahada 4,920 na wenye stashahada ni 4,306. Kati ya walimu watakaoajiriwa jumla ya walimu 9,039 wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na walimu 187 wamepangwa kufundisha katika vyuo vya ualimu.

Walimu wote wa shule za sekondari wamepangwa katika Halmashauri mbalimbali kwa kutumia kigezo cha upungufu wa walimu katika Halmashauri husika. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kuripoti katika Halmashauri aliyopangwa kwa kuwa fedha za mshahara wake zimekasimiwa kwenye Halmashauri alikopangwa na si vinginevyo. Orodha ya walimu hao na Halmashauri walikopangwa zimetumwa kwenye Mikoa na Halmashauri. Aidha, orodha hiyo inapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) na tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (www.pmoralg.go.tz).

Walimu wote wapya wanaagizwa kuhakikisha kwamba wanaripoti katika Halmashauri/ Vyuo vya Ualimu walikopangwa ifikapo tarehe 24/01/2011. Watendaji na wasimamizi wa elimu kwenye Halmashauri na Vyuo vya Ualimu watakuwepo kuwapokea.

Mwalimu yeyote atakayeshindwa kuripoti kwenye Halmashauri / Chuo alikopangwa baada ya siku saba (7) tangu tarehe anayotakiwa kuripoti atahesabika kuwa amekataa kukubali nafasi ya ajira aliyopewa na Serikali.

Baada ya kuripoti kwenye Halmashauri/Vyuo waajiri watatakiwa kuwajazia walimu hao Fomu maalum zenye Taarifa ya Kiutumishi ya Mtumishi (Personal Data Form) na kuziwasilisha Ofisi ya Rais, UTUMISHI pamoja na barua ya ajira ya mtumishi. Taarifa hizo zikiwa katika “hard” na “soft copy” ziwasilishwe UTUMISHI kabla au ifikapo tarehe 29/01/2011 ili watumishi hao waingizwe katika mfumo wa malipo (Payroll). Waajiri wanakumbushwa kwamba “Computer Data Sheet” hazitahitajika katika zoezi hili.

Waajiri (Wakurugenzi wa Halmashauri na Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi) watawalipa malipo stahili kwa mujibu wa nyaraka na miongozo ya Serikali kuhusu waajiriwa wapya.

Nawatakia utumishi mwema katika Sekta ya Elimu.

Imetolewa na:

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

MUHIDIN MICHUZI at Sunday, January 16, 2011

Sasa ndugu nikwamba kusoma hujui ama?
Huo mlolongo wa maelezo ya wanasiasa wewe binafsi umeelewa hao walim tajwa hapo juu waliajiriwa mwaka gani?
 
Back
Top Bottom