JK afanye nini? hao waalim si ni wasomi, nikiwa na maana wanajua haki zao! labda uniambia ni UPE kama mkuu wa mkoa fulani. walikubali vipi kulala chini na kucharazwa na sungu sungu ambao hata shule hawakwenda. JK atafanya mangapi? makosa ni yao wenyewe kukubali kulazwa chini mbele ya kadamnasi na machokoraa.Aisee, hii ni aibu kwa nchi inayojigamba kuwa ina utawala bora na unaofuata sheria. JK upo wapi?
Sio waalimu tu, things are now going out of proportions, jumamosi mkuu wa mkoa
( RC) katuma mapolisi na maafisa usalama kumtoa ndani ya ofisi mwenyekiti wa baraza la Ardhi na nyumba Kigoma eti kwa sababu hafuati maelekezo yake.
Inaelekea rule of law inaanza kupuuzwa, ukifanya kosa naamua adhabu ya kukupa papo hapo ndio maana yake.
Tunakwenda wapi????
JK afanye nini? hao waalim si ni wasomi, nikiwa na maana wanajua haki zao! labda uniambia ni UPE kama mkuu wa mkoa fulani. walikubali vipi kulala chini na kucharazwa na sungu sungu ambao hata shule hawakwenda. JK atafanya mangapi? makosa ni yao wenyewe kukubali kulazwa chini mbele ya kadamnasi na machokoraa.
Nyerere alipewa na nani mamlaka ya kuwachapa wanachuo cha udsm?
nyerere alipewa na nani mamlaka ya kuwachapa wanachuo cha udsm?
Mkuu hebu tema mate chini...!
Unawajuwa watawala wa nchi hii? Amini usiamni hata wewe siku moja unaweza kucharazwa bakora na Makamba au hata Mbunge wa viti maalumu. Huko vijijini hali ni mbaya sana na hawa walimu wanahitaji msaada ambao utawasaidia wao na pia sisi wenyewe ambao zamu yetu walau bado haijafika!
DC sio vijijini tu mambo haya hutokea hata mijini, ona wamachinga wanavyopigwa na askari wa jiji kunyang'anywa bidhaa zao na hata kuvuliwa nguo wakati mwingine je kuna yoyote kati yetu aliyethubutu angalau kukemea vitu hivyo? Wanajeshi wanapiga trafiki, wanapiga watu wa Dawasco eti hawataki kukatiwa maji na Dawasco hawasemi kitu na waliopigwa hawasemi kitu rule of law Tanzania ipo theoretically everyone has his own laws to suit his desire basi
Nakubaliana na Dark City huko vijijini hakuna sheria wala mahakama. Ni uchifu tuu ndio unaendelea.
LAKINI WAZIRI WA ELIMU ANASEMA NINI KUHUSU MATOKEO YA AINA HII MBONA AMENYAMAZA KIMYA?
Angejaribu kwenda kuwapa pole na kuonyesha support kwa walimu basi ingekuwa ni funzo kubwa. Na hao ni lazima washitakiwe.
Tunacharaza viboko walimu halafu tunalalamika elimu duni na kadhalika. Yatakwendaje haya?