Walimu wacharazwa bakora tena, mbele ya wanafunzi wao!!

Walimu wacharazwa bakora tena, mbele ya wanafunzi wao!!

Aisee, hii ni aibu kwa nchi inayojigamba kuwa ina utawala bora na unaofuata sheria. JK upo wapi?
JK afanye nini? hao waalim si ni wasomi, nikiwa na maana wanajua haki zao! labda uniambia ni UPE kama mkuu wa mkoa fulani. walikubali vipi kulala chini na kucharazwa na sungu sungu ambao hata shule hawakwenda. JK atafanya mangapi? makosa ni yao wenyewe kukubali kulazwa chini mbele ya kadamnasi na machokoraa.
 
Sio waalimu tu, things are now going out of proportions, jumamosi mkuu wa mkoa
( RC) katuma mapolisi na maafisa usalama kumtoa ndani ya ofisi mwenyekiti wa baraza la Ardhi na nyumba Kigoma eti kwa sababu hafuati maelekezo yake.

Inaelekea rule of law inaanza kupuuzwa, ukifanya kosa naamua adhabu ya kukupa papo hapo ndio maana yake.

Tunakwenda wapi????

tunakwenda kuzimu
 
JK afanye nini? hao waalim si ni wasomi, nikiwa na maana wanajua haki zao! labda uniambia ni UPE kama mkuu wa mkoa fulani. walikubali vipi kulala chini na kucharazwa na sungu sungu ambao hata shule hawakwenda. JK atafanya mangapi? makosa ni yao wenyewe kukubali kulazwa chini mbele ya kadamnasi na machokoraa.

Mkuu hebu tema mate chini...!

Unawajuwa watawala wa nchi hii? Amini usiamni hata wewe siku moja unaweza kucharazwa bakora na Makamba au hata Mbunge wa viti maalumu. Huko vijijini hali ni mbaya sana na hawa walimu wanahitaji msaada ambao utawasaidia wao na pia sisi wenyewe ambao zamu yetu walau bado haijafika!
 
mmmh I'm shocked... watu bado wanaishi kwenye stone age? why would they force them to attend the meeting? even if it was compulsory for them to attend this kind of meetings there should be another discipline action against them instead of humiliating them....

Halafu kwanini wakampiga mke wa mwalim mkuu? halafu hawa sungusungu are they trained to hit ppl only? aint they supposed to have basic knowledge on human rights ?
 
Mkuu hebu tema mate chini...!

Unawajuwa watawala wa nchi hii? Amini usiamni hata wewe siku moja unaweza kucharazwa bakora na Makamba au hata Mbunge wa viti maalumu. Huko vijijini hali ni mbaya sana na hawa walimu wanahitaji msaada ambao utawasaidia wao na pia sisi wenyewe ambao zamu yetu walau bado haijafika!

DC sio vijijini tu mambo haya hutokea hata mijini, ona wamachinga wanavyopigwa na askari wa jiji kunyang'anywa bidhaa zao na hata kuvuliwa nguo wakati mwingine je kuna yoyote kati yetu aliyethubutu angalau kukemea vitu hivyo? Wanajeshi wanapiga trafiki, wanapiga watu wa Dawasco eti hawataki kukatiwa maji na Dawasco hawasemi kitu na waliopigwa hawasemi kitu rule of law Tanzania ipo theoretically everyone has his own laws to suit his desire basi
 
Nakubaliana na Dark City huko vijijini hakuna sheria wala mahakama. Ni uchifu tuu ndio unaendelea.

LAKINI WAZIRI WA ELIMU ANASEMA NINI KUHUSU MATOKEO YA AINA HII MBONA AMENYAMAZA KIMYA?

Angejaribu kwenda kuwapa pole na kuonyesha support kwa walimu basi ingekuwa ni funzo kubwa. Na hao ni lazima washitakiwe.

Tunacharaza viboko walimu halafu tunalalamika elimu duni na kadhalika. Yatakwendaje haya?
 
Mkuu hii hali inasikitisha. Kwa kweli kitendo cha watu kufumbia macho huu utaratibu wa kishenzi wa wenye mamlaka kuwachapa bakora wanyonge ni kibaya na inabidi kilaaniwe. Inatakiwa kila mtu asimame imara kulaani matumizi ya nguvu za dola au nyingine kuwanyanyasa watu wasio na hatia.

Nakubaliana na Dark City huko vijijini hakuna sheria wala mahakama. Ni uchifu tuu ndio unaendelea.

LAKINI WAZIRI WA ELIMU ANASEMA NINI KUHUSU MATOKEO YA AINA HII MBONA AMENYAMAZA KIMYA?

Angejaribu kwenda kuwapa pole na kuonyesha support kwa walimu basi ingekuwa ni funzo kubwa. Na hao ni lazima washitakiwe.

Tunacharaza viboko walimu halafu tunalalamika elimu duni na kadhalika. Yatakwendaje haya?

Katika nchi hii hakuna mtu anajali maslahi ya wanyonge. Labda tu kama anaomba kura. Subirini kuanzia August utaona jinsi ambavyo kila mtu atajitutumua. Ni unafiki tu.
 
Leo meya amempa mwandishi wa mtanzania hukohuko Bukoba! Kaaz kwel kwel!
 
nasema hivi pamoja na umasikini wangu nilionao na hali ngumu ya maisha MTU YOYOTE HANICHARAZI VIBOKO.
 
Hii ni njia moja mbaya sana ya udhalilishaji hasa kwa mwl ambaye ni mtu muhimu ktk jamii. Je hakuna njia nyingine mbadala wa kutoa adhabu badala ya viboko tena mbele ya wtt?km kweli taarifa hii ni ya ukweli basi walimu wanapaswa kufika mbali zaidi. Ni uonevu wa aina yake. Mimi km m2 mzima bora risasi kuliko nichapwe viboko tena mbele ya wnfnz. Duuuuh!sisi watz wapole kupita kiasi.
 
Back
Top Bottom