Walimu waijia juu Serikali, wasema Kikokotoo bado kipo kinasubiri kuwaliza watumishi

Walimu waijia juu Serikali, wasema Kikokotoo bado kipo kinasubiri kuwaliza watumishi

Yani magufuli akishinda awamu iyayo. Ni kuwa tutajutaaa. Awamu ya kwanza tutaiona kama trailer.
 
Alitumbuliwa Mama Kikokotoo Akaachwa Jenister
Uonevu Upo Mkubwa
 
Unaposema lazima kikokotoo kijali uhai wa mifuko unamaanisha nini?

Ni pesa yangu, inawekwa kwa miaka isiyopungua 30 ya utumishi wangu uliotukuka. Kwa ujinga wa wanaoweka, wananiambia kuna kikokotoo cha jinsi ya kupata savings zangu? Na pia niache na nyingine kwaajili ya mfuko, miaka 30 walikuwa wanazichimbia chini pesa? Hakuna hata faida iliyotokana na uwekezaji wangu wa miaka 30?

Mnapeana nyumba, mnalipana kufuru, mnajilimbikizia ardhi, hamkati kodi, kwa umri nilioishi, sijaona jema lolote lililofanywa na bunge(pensheni ya 282m kwa miaka 5) au serikali ukilinganisha na jasho walilovuja wananchi.
Tatizo kubwa tulilonalo Watanzania hasa sisi Wafanyakazi ni kuchukulia hifadhi ya Jamii kama uwekezaji wa fedha za akiba benki! Hifadhi ya Jamii ni tofauti kabisa na uwekaji wa akiba benki!

Hifadhi ya jamii ni utaratibu wa kumlinda Mfanyakazi ili asiathiriwe na majanga ya kukosa kipato kutokana na sababu zozote zile ikiwemo Kupoteza uwezo wa kufanya kazi, kuugua, kupoteza ajira, kustaafu na kwa jamii ya wale wanaomtegemea endapo Mfanyakazi atakufa.

Suala hili linahitaji elimu kubwa sana kwa jamii ya Wafanyakazi ili tuelewe maana ya Hifadhi ya Jamii vs Uwekaji wa akiba. Zamani huduma ya provident fund ilikuwepo ambapo Wafanyakazi waliweka akiba katika mifuko na walipostaafu walipewa hela zao lakini hazikuwasaidia na pia zilikiuka ILO Conventions zinazosimamia masuala ya hifadhi ya Jamii Duniani.

Huwezi kusema Sheria ya Kikokotoo alichokipiga stop Mhe. Rais bado ipo!!! Kanuni hazipo katika Sheria, bali zilitungwa na Waziri mwenye dhamana. Mhe Rais anapozuia Kanuni husika zisitumike na kwamba wadau warejee kwenye meza ya duara na kuhakikisha wanakuja na Kanuni bora kwa pande zote (mifuko na Wanufaika), hiyo maana yake ni kwamba Kanuni mpya za Waziri zimefutwa kupitia agizo la Mhe. Rais na kwamba Kanuni zitakazoletwa baada ya 2023 ndizo sasa zitakuwa Kanuni mpya zitakazotumika.

Sheria inayotajwa, Sheria Na. 2 ya 2018 ya PSSSF ni Sheria iliyounganisha Mifuko ya PSPF (iliyohudumika Watumishi wa Umma katika Serikali Kuu), LAPF ( Iliyohudumia Watumishi wa Serikali za Mitaa), GEPF (Iliyohudumia Watumishi wa Majeshi yetu) na PPF (Iliyohudumia Watumishi wa Mashirika ya Umma). Pia sheria hii imerekebisha baadhi ya vifungu vya Sheria ya NSSF ili iendane na mfumo huu mpya wa kuwa na mifuko miwili nchini ikihudumia Sekta ya Umma (PSSSF) na Sekta Binafsi (NSSF). Kwa hiyo ni kweli Sheria bado haijafutwa lakini haizuii Kanuni za Vikokotoo kufanyiwa marekebisho kama Mhe. Rais alivyoelekeza.

Nimalizie kwa kusema kuwa, Wafanyakazi hatuna budi kutafuta ukweli wa masuala haya ya Hifadhi ya Jamii. Tukiendelea kushabikia suala la mivhango yetu katika mifuko kuwa ni akiba, tutakuwa hatutendi haki kwetu sisi wenyewe na kwa Serikali yetu. Hifadhi na Akiba ni vitu viwili vyenye maana tofauti kabisa.
 
Kwel mkuu mkoan iringa kuna walim wanajiita wazalendo huwaa nawaonea huruma sana wote n ccm zen wakitoka kubwabwaja kwa media wanaaza kunywa bingwa na eagle za buku buku pamoja na vitoko vya jelo jelo
Hili kundi linawatu wapumbavu wengi sn
 
Wabunge wa CCM vilaza kabisa, Kuondoa FAO la kujitoa Ni kunyanyasa wanyonge.

Sasa hivi wamerudi Tena kutudanganya.

FAO la kujitoa...Pesa za akiba Ni Haki ya wafanyakazi.
Hizo Pesa sio hisani ya Serikali au mkopo
 
Tatizo kubwa tulilonalo Watanzania hasa sisi Wafanyakazi ni kuchukulia hifadhi ya Jamii kama uwekezaji wa fedha za akiba benki! Hifadhi ya Jamii ni tofauti kabisa na uwekaji wa akiba benki!

Hifadhi ya jamii ni utaratibu wa kumlinda Mfanyakazi ili asiathiriwe na majanga ya kukosa kipato kutokana na sababu zozote zile ikiwemo Kupoteza uwezo wa kufanya kazi, kuugua, kupoteza ajira, kustaafu na kwa jamii ya wale wanaomtegemea endapo Mfanyakazi atakufa.

Suala hili linahitaji elimu kubwa sana kwa jamii ya Wafanyakazi ili tuelewe maana ya Hifadhi ya Jamii vs Uwekaji wa akiba. Zamani huduma ya provident fund ilikuwepo ambapo Wafanyakazi waliweka akiba katika mifuko na walipostaafu walipewa hela zao lakini hazikuwasaidia na pia zilikiuka ILO Conventions zinazosimamia masuala ya hifadhi ya Jamii Duniani.

Huwezi kusema Sheria ya Kikokotoo alichokipiga stop Mhe. Rais bado ipo!!! Kanuni hazipo katika Sheria, bali zilitungwa na Waziri mwenye dhamana. Mhe Rais anapozuia Kanuni husika zisitumike na kwamba wadau warejee kwenye meza ya duara na kuhakikisha wanakuja na Kanuni bora kwa pande zote (mifuko na Wanufaika), hiyo maana yake ni kwamba Kanuni mpya za Waziri zimefutwa kupitia agizo la Mhe. Rais na kwamba Kanuni zitakazoletwa baada ya 2023 ndizo sasa zitakuwa Kanuni mpya zitakazotumika.

Sheria inayotajwa, Sheria Na. 2 ya 2018 ya PSSSF ni Sheria iliyounganisha Mifuko ya PSPF (iliyohudumika Watumishi wa Umma katika Serikali Kuu), LAPF ( Iliyohudumia Watumishi wa Serikali za Mitaa), GEPF (Iliyohudumia Watumishi wa Majeshi yetu) na PPF (Iliyohudumia Watumishi wa Mashirika ya Umma). Pia sheria hii imerekebisha baadhi ya vifungu vya Sheria ya NSSF ili iendane na mfumo huu mpya wa kuwa na mifuko miwili nchini ikihudumia Sekta ya Umma (PSSSF) na Sekta Binafsi (NSSF). Kwa hiyo ni kweli Sheria bado haijafutwa lakini haizuii Kanuni za Vikokotoo kufanyiwa marekebisho kama Mhe. Rais alivyoelekeza.

Nimalizie kwa kusema kuwa, Wafanyakazi hatuna budi kutafuta ukweli wa masuala haya ya Hifadhi ya Jamii. Tukiendelea kushabikia suala la mivhango yetu katika mifuko kuwa ni akiba, tutakuwa hatutendi haki kwetu sisi wenyewe na kwa Serikali yetu. Hifadhi na Akiba ni vitu viwili vyenye maana tofauti kabisa.
Kama Serikali inawajali Watanzania, je Wakulima wanatunza uzeeni?

Hiyo Pesa ya mifuko Ni pesa ya Serikali?

Kwa hiyo mtu amesoma mpaka amepata kazi, Ni Mjinga..hajui maisha yake ya mbele?

Akina Lusinde Kibakaji na Deo Jah wa Njombe Ni wasomi, mbona wabunge wanapewa pension fully?

Watanzania Ni wajinga Sana, hawajui Kupanga maisha yao? Mbona hakuwapangii mishahara yao namna ya kutumia!

Wafanyabiashara wengi hawapo NSSF...je Serikali inawajali uzeeni?

Mwaka 2018 Serikali iliondoa FAO la kujitoa kwa Kura nyingi za CCM

Rais akasikia nchi Nzima ikilalakika, Waziri Jenister Mhagama, haikupata maoni ya wafanyakazi. Kwa Nini hawakupeleka marekebisho?

Wafanyakazi Ni wasomi na watu wenye akili, Acha upotoshaji.

Jf Ni jukwaa la watu wenye akili...

Rudi Tena kwa majibu Mkuu hapa.
 
Hifadhi ya jamii ni utaratibu wa kumlinda Mfanyakazi ili asiathiriwe na majanga ya kukosa kipato kutokana na sababu zozote zile ikiwemo Kupoteza uwezo wa kufanya kazi, kuugua, kupoteza ajira, kustaafu na kwa jamii ya wale wanaomtegemea endapo Mfanyakazi atakufa.
Maelezo mengi ni porojo za kisiasa, uko upande gani labda kati ya wanufaika na wanufaishishaji? Maana hii aya inakinzana na kila kitu kingine ulichoeleza.

Mfanyakazi anayelindwa hapa ni nani? Ni wale wazee wa EAC waliokuwa wanasoteshwa miaka 20? Ni hawa ambao vibarua vikiota nyasi inakuchukua miaka 2 kumpa 33% ya akiba yake? Na kwa muda upi?

Ni hawa ambao wanasubiri mafao yao kwa miaka 3 sasa huku mtaani?

Ni hawa ambao umekuwa ukikata pesa zao bila kujua kama alithibitishwa kazini au la, ila anapoanza kudai, unamwambia leta barua ya kuthibitishwa kazini kama kigezo kikuu cha kumpa au kutompa?

Ni hawa ambao itawabidi wasubiri mpaka 55 kupata akiba yao kama lolote limetokea kabla ya hiyo 55?

Mathalani, NHIF imechangiwa na watumishi kwa kwa muda gani kabla yakuanza kutoa huduma? Huduma zipi wanazotoa za maana?

Unapopinga kuwa sio uwekezaji, mnawatozea nini watumiaji wa daraja la Kigamboni?

Miradi kama Machinga complex ilijengwa kwaajili ya wasiojiweza? Kwamba sio uwekezaji

Nilisikia kuwa mtafuta pesa ni mmoja tu kati ya ile mihimili, ni vipi wengine kiinua mgongo chao kiwe 282m kwa 5yrs na wengine 52m kwa 36yrs? Usiniambie habari za basic na gross hapa, na hio sio kesi, wanalipwa hata kabla ya wakati, kikubwa kipi walichoifanyia nchi au jamii?

SISI, sio neno linalokufaa wewe. Mke wa rizimoko ni muajiriwa wa NHC, unadhani naye anaweza kuwa na malalamiko kama hayo? Wale waliojazana pale BOT, unadhani wanashida hiyo? Kamuulize mwalimu wa Kantalamba kule ili ujue tofauti.

NINYI SIO SISI.
 
Tuwe tunatenda haki kwa Mhe. Rais Dr. JPJM kwa namna alivyolishughulikia suala la kikokotoo. Unaposema Kikokotoo bado kipo unamaanisha nini wakati Walimu (Waliokuwa PSPF) wanaendelea kulipwa kwa Kikokotoo cha 1/540 Accrued Factor, 15.5 Reducing Factor na Mkupuo wa 50% kama ilivyokuwa hapo awali. Kikokotoo cha 1/580, 12.5 & 25% kilipigwa stop hadi 2023 na Wafanyakazi tunafahamu Serikali imeshaanza mazungumzo na Wadau ili kupata kikokotoo kitakachokidhi haja za pande zote (Mifuko na Wanachama).

Ni vyema mabaya tuyaseme lakini yanapofanyika mazuri pia tuyaseme. Lazima Kikokotoo kipya kitengenezwe kitakachojali Uhai wa Mifuko na wakati huo huo kiwapatie wastaafu mafao yatakayowapatia maisha yenye staha wakiwa nje ya ajira. Walimu waendelee kuwasiliana na CWT ambayo ipo ndani ya TUCTA waweze kujua ukweli wa jambo hili na kuepuka uchichezi usio wa lazima baina ya Walimu na Mhe. Rais.
Tusiwe na tabia ya kubeza msoni ya watu na kujikita kwenye kusifu mambo ambayo kwa akili ya kawaida yako wazi.

Mswaada wa sheria ya kikokotoo uliandaliwa na upande wa serikali ya JPM, haukuwa mswaada binafsi kutoka kwa mbunge yeyote bungeni. KWA HIYO KILICHOKUWA KINALETWA KILIKUWA NA BARAKA ZOTE ZA SERIKALI YA JPM. Alichokifanya ni kiini macho ili tuone kwamba Rais kasema kitu.

Licha ya kwamba Rais alisema tuendelee na utaratibu wa siku zote hadi 2023 NSSF walibaki kwenye sheria mpya. Kwa hiyo professionals wote kule NSSF ni mwendo wa 33% tu.

Halafu unapodiriki kusema
Serikali imeshaanza mazungumzo na Wadau ili kupata kikokotoo kitakachokidhi haja za pande zote (Mifuko na Wanachama), UKUMBUKE MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII HAIKUANZISHWA ILI IKIDHI HAJA YA MIFUKO HIYO. Yaani fedha za watumishi zitumike hovyo halafu baadaye mchangie hasara.(mlaji Na mtumiaji Mbaya wa fedha za mifuko ni serikali, uhai hafifu mifuko ya HIFADHI Ya JAMII umesababishwa na serikali)

TUACHE UNAFIKI NA KUJIPENDEKEZA. HUSUSANI WATU WANAPOONGELEA MASLAHI YAO MUHIMU.
 
Chama cha kutetea haki na maslahi ya walimu Tanzania CHAKAMWATA kimelia kilio cha uchungu mkubwa sana kwamba kuna uonevu mkubwa sana unaofanywa na serikali ya awamu ya 5.

Kimedai kwamba serikali iliwadanganya kusitishwa KIKOKOTOO na FAO LA KUJITOA. Kwamba hivi vitu bado vipo na vinasubiri muda kuanza kutumika. Haya ni majibu waliyopewa na Waziri Jenister Muhagama na katibu mkuu wake wa wizara.

Walimu mliopigiwa simu kupitia kwa Waziri Jenister mkaambiwa kua mnapendwa mkafurahi jipimeni na fikirieni maisha na familia zenu.
"Takwimu zao zinaonyesha hakuna dalili yoyote kwa Mgombea wa Chama cha Meko full kupata hata asilimia 40 ya kura. Chama cha Meko full wameshakata tamaa na ushindi. Kwa msingi huo wamepangwa kumtangaza Mgombea wa Chama Cha Meko full usiku wa manane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom