KERO Walimu walioajiriwa mwaka 2026 katika Halmashauri ya Bukombe hatujalipwa fedha za kujikimu

KERO Walimu walioajiriwa mwaka 2026 katika Halmashauri ya Bukombe hatujalipwa fedha za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Walimu walioajiriwa mwaka 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe hatujalipwa fedha za kujikimu tangu tuliporipoti kazini hadi leo, huku kimya kikiwa kimetawala na bila kupewa maelezo yoyote.

Kila tunapojaribu kuhoji, tunakutana na vitisho kutoka kwa viongozi, wakati wenzetu wa kada ya afya tulioripoti pamoja tayari wamelipwa.

Tunaomba mamlaka husika zitimize wajibu wao wa kutupatia fedha hizo, kwani ni haki yetu ya msingi kama waajiriwa wapya. Ikiwa kuna maelezo au changamoto nyingine kuhusu malipo hayo, tunaomba tujulishwe ili tujue kinachoendelea.
 
Gen Z mnashida sana; hela ya kujikimu mtapewa na mwajiri kama ipo. Kama haipo mtaendelea kusubiri cha msingi mshahara wenu mpate. Mtasubiri hadi lini, haijulikani, hata miaka 6 🤷🏾
 
Walimu ajira mpya 2026 halmashauri ya wilaya ya Bukombe hatujalipwa fedha zetu za kujikimu tunaomba wahusika watekeleze wajobu wao.
Kwa taarifa zilizopo wenzetu wa kada ya afya wamelipwa tayari lakini sisi bado hatujapewa kitu bila kuelezwa chanzo tunaomba Jamii forums mtupazie sauti ili haki itendeke maana tupo kwenye hali ngumu
 
Welcome to the troubles' profession. Hapo Bado hujakunatana na mkuu mnoko, hujakaa sawa unaambiwa jaza pepmis na bando huna,mara paa umeingia benk kukopa, hujageuka meki huyu hapa kukagua wachelewaji ,unaona Bora kuhama mfumo unakwambia vacancy not budgeted. Unaamua kuwa mpooe
 
Sisi watumishi Halmashauri ya Bukombe ambao ni Walimu na Sekta ya Afya hatujapewa fedha zetu za kujikimu tangu tuanze kazi May 2025.
 
Back
Top Bottom