Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,112
Wakuu! Leo katika magazeti mbalimbali na taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari kuna walimu wanagoma kwenda vituo vyao vya kazi haswa mikoa ya pembezoni ukiwamo mkoa wa Kigoma. Nimejaribu kufanya brainstorming nikakumbuka ni dhahiri kuna sababu zinazotajwa ni za msingi. Ukosefu wa miundombinu bora ya usafiri, mikoa ya Tabora,Kigoma,Mtwara,Lindi na Manyara inatajwa kuwa na miundombinu duni hivyo kuwapunguzia mvuto walimu. Hali ya hewa,hapa kuna watu wanazungumzia joto na mvua kwamba kuna maeneo ni kame hivyo yatampa wakati mgumu walimu kwani wengi wanategemea kujishughulisha na shughuli za kiuchumi vile mshahara ni mdogo. Suala lingine ni mazingira ya kazi, kuanzia kukosekana kwa nyumba za walimu na makazi bora. Lakini,nje ya hayo yote bado tunahitaji usawa wa idadi ya walimu wilaya.Je, serikali ifanye nini?