Walimu wanaogoma kwenda vituo vya kazi walivyopangiwa,Serikali ifanye nini?

Walimu wanaogoma kwenda vituo vya kazi walivyopangiwa,Serikali ifanye nini?

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
3,395
Reaction score
1,112
Wakuu! Leo katika magazeti mbalimbali na taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari kuna walimu wanagoma kwenda vituo vyao vya kazi haswa mikoa ya pembezoni ukiwamo mkoa wa Kigoma. Nimejaribu kufanya brainstorming nikakumbuka ni dhahiri kuna sababu zinazotajwa ni za msingi. Ukosefu wa miundombinu bora ya usafiri, mikoa ya Tabora,Kigoma,Mtwara,Lindi na Manyara inatajwa kuwa na miundombinu duni hivyo kuwapunguzia mvuto walimu. Hali ya hewa,hapa kuna watu wanazungumzia joto na mvua kwamba kuna maeneo ni kame hivyo yatampa wakati mgumu walimu kwani wengi wanategemea kujishughulisha na shughuli za kiuchumi vile mshahara ni mdogo. Suala lingine ni mazingira ya kazi, kuanzia kukosekana kwa nyumba za walimu na makazi bora. Lakini,nje ya hayo yote bado tunahitaji usawa wa idadi ya walimu wilaya.Je, serikali ifanye nini?
 
Cjajua kama hii kitu ipo au la....ila mimi Nashauri ianzishe hardship allowance kwa walimu walio meneo ya vijijini ili angalau nao wapate moyo wa kukaa sehem hizo hata kama ni kwa miaka miwili mitatu.
 
Ndugu zanguni aacheni tu tupo huku vijijini ni hatari umeme hakuna, maji hakuna.
 
Mbali na hardship allowance, napendekeza walimu wa vijijini pamoja na wafanyakazi wengine ndio wapewe kipaumbele katika kwenda kusoma. Aksante
 
Hivi inawezekanaje unampangia mwalimu kwenda kufundisha kigoma ilihali hata mazingira yenyewe hayajaandiliwa?? Anafikaje huko kigoma?? tena unakuta tangu amemaliza shule hajapata hata katemporary kwa kuingizia kipato??
 
Ndugu zanguni aacheni tu tupo huku vijijini ni hatari umeme hakuna, maji hakuna.
nakubali umeme hakuna and you can survive,hata walio mijini wakati mwingine wanapiga deshi ya umeme!!ila hapo kwenye maji sijui una maanisha nini kusema maji hakuna!!!!
 
Ndugu zanguni aacheni tu tupo huku vijijini ni hatari umeme hakuna, maji hakuna.

Kifupi serikali inapaswa kuzijibu hoja za walimu kutokwenda vijijini ila kwa vitendo..kuangalia maslahi yao na kuyaboresha mazingira..
 
Aende nani sasa?
Na je, huko wasikotaka kwenda hakuna wanaoishi? Kama wapo wanaishije? Utajibu wamezoea, sawa.
Kwani wao wakienda hawatazoea?

Kama hawataki wapangiwe wengine wenye nia na njaa, hao wagomao waweza kuwa hawana nia wala njaa.

QUOTE]Ualimu ni wito[QUOTE
 
Hizo sababu na kwa mikoa uliyohitaja ni kweli dhairi shairi ..mie nadhani hii marginalised regions watu wawe motivated.
 
Wakuu! Leo katika magazeti mbalimbali na taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari kuna walimu wanagoma kwenda vituo vyao vya kazi haswa mikoa ya pembezoni ukiwamo mkoa wa Kigoma. Nimejaribu kufanya brainstorming nikakumbuka ni dhahiri kuna sababu zinazotajwa ni za msingi. Ukosefu wa miundombinu bora ya usafiri, mikoa ya Tabora,Kigoma,Mtwara,Lindi na Manyara inatajwa kuwa na miundombinu duni hivyo kuwapunguzia mvuto walimu. Hali ya hewa,hapa kuna watu wanazungumzia joto na mvua kwamba kuna maeneo ni kame hivyo yatampa wakati mgumu walimu kwani wengi wanategemea kujishughulisha na shughuli za kiuchumi vile mshahara ni mdogo. Suala lingine ni mazingira ya kazi, kuanzia kukosekana kwa nyumba za walimu na makazi bora. Lakini,nje ya hayo yote bado tunahitaji usawa wa idadi ya walimu wilaya.Je, serikali ifanye nini?

Jana niliona watu kibao wa Kigoma wanamsifia Kikwete kuwa kawaletea maendeleo na sasa wana ''lami hadi sebuleni''. Sasa inakuwaje tena walimu wakatae Kigoma. Nashauri TBCCM ianzishe vipindi vya kutangaza vivutio vya mikoa mbalimbali ili kiwavutia walimu kwenda kufanya kazi mikoa mbalimbali, kama tunavyovutia wawekezaji au watalii.
 
lami itoke wapi kigoma,walimu wakipewa extra money kama wanavyodai wengi wanaweza kubaki kwenda ktk vituo walivyopangiwa. Lakini serikali wakiendelea na mtazamo hasi juu ya walimu watakuwa wanacheza mchezo wa pata potea. Wawape kipau mbele walimu wataona hakuna usumbufu utakaojitokeza ktk sekta ya elimu TZ.
 
Sasa nani aende?
Na je, huko wasikotaka kwenda hakuna wanaoishi? Kama wapo wanaishije? Utajibu wamezoea, sawa.
Kwani wao wakienda hawatazoea?

Kama hawataki wapangiwe wengine wenye nia na njaa, hao wagomao waweza kuwa hawana nia wala njaa.

QUOTE]Ualimu ni wito[QUOTE

Usifikiri kila anayekaa kijiji fulan karidhika nacho, wengine wamekosa altenative ndo maana wamejikatia tamaa. Ingekuwa watu wanazoea kusingekuwa na na wimbi kubwa la watu kukimbilia mjini. Jus imagine mtu kakulia mjini harafu anafika miaaka 20 unampereka kijijini eti kisa ukamlipe mshahara mbuzi! No way out hapa serikari lazima iwaangalie upya watu wanaofanya kazi vijijini. Naamin serikari inaweza kuwapa cchote kama itajibana kwnye mashangingi na mambo mengine.
 
Tatizo serikali inafanya haya as if ni adhabu,nchi yetu sote iweje usioneshe kuwajali watu wako? ajira si adhabu jamani.
 
Sasa nani aende?
Na je, huko wasikotaka kwenda hakuna wanaoishi? Kama wapo wanaishije? Utajibu wamezoea, sawa.
Kwani wao wakienda hawatazoea?

Kama hawataki wapangiwe wengine wenye nia na njaa, hao wagomao waweza kuwa hawana nia wala njaa.

QUOTE]Ualimu ni wito[QUOTE

Hahahahahahahahahahahaha na kwa kua ni wito na hamuwezi kuuthamini endeleeni kusubiri majanga ktk mitihani ya watoto na wadogo zenu.
 
Sasa nani aende?
Na je, huko wasikotaka kwenda hakuna wanaoishi? Kama wapo wanaishije? Utajibu wamezoea, sawa.
Kwani wao wakienda hawatazoea?

Kama hawataki wapangiwe wengine wenye nia na njaa, hao wagomao waweza kuwa hawana nia wala njaa.

QUOTE]Ualimu ni wito[QUOTE

futa kauli yako ualimu ni kazi kama zingine ualimu n wito n sera ya serikali ilikuwapa moyo walimu wazidi kuwakandamiza kwa maslahi madogo mazingira duni uhabawa vitendea kazi na mengine mengi kama hayo mpaka sasa Tz ualimu ndo kazi iliyoonekana ni ya watu wasio na elimu maskini na wanaodharaulika zaidi miaka ya zaman mwalimu alione kidogo ni mtu mwenye hadhi katika jamii lakini kwa sasa hata mwalimu anashidwa kujitambulisha kwa cheo chake kutokana na manyanyaso wanayo patiwa na serikali ifike kipindi mwalimu awe na hadhi kama enzi za mwalimu
 
Mkuu mimi siamini kama bado ualimu ni wito labda nipewe maana halisi ya neno wito katika ulimwengu wa kibepari maana vitu hubadilika kulingana na wakati, nadhani kuna pahala tunakosea kwenye hii dhana ya elimu ni wito kitu ambacho kinawavunja moyo walimu......ualimu wito,vipi uhasibu na udaktari....:nono:
 
Tatizo linapokuja ni pale panapokosekana jitihada za kuwafanya wale wanaofanya kazi vijijini mijini na vijijini wajione wapo nchi moja.Najiuliza nyumba za kupanga huko vijijini zikoje huwa sipati picha :-*
 
Lakini mkuu watu ni rasilimali ya taifa na kama wanatakiwa kulitumikia bila shaka watatakiwa kuwa allocated anywhere hivyo tatizo ni miundombinu juu ya kuwavuta watu wetu kwani haiwezekani kuwa na sera ya waliozaliwa mjini wafanye kazi mjini na wale wa vijijini wafanye kazi mjini.
 
Sasa nani aende?
Na je, huko wasikotaka kwenda hakuna wanaoishi? Kama wapo wanaishije? Utajibu wamezoea, sawa.
Kwani wao wakienda hawatazoea?

Kama hawataki wapangiwe wengine wenye nia na njaa, hao wagomao waweza kuwa hawana nia wala njaa.

QUOTE]Ualimu ni wito[QUOTE

ualimu siyo wito nikazi kama zilivyo kazinyingine ,mwalimu nae athaminiwe.
 
Back
Top Bottom