RSM Dominik
JF-Expert Member
- Apr 3, 2026
- 207
- 561
Wakuu habari za mihangaiko ya hapa na pale.
Kuna jambo linasikitisha kidogo, na kama ungekuwa ni wewe sidhani kama ungefurahia, mwaka jana 2025 serikali ilianzisha mradi wa kusapoti elimu yetu kutokana na upungufu wa walimu mashuleni na katika mradi huo viliainishwa vitu vingi ikiwemo sifa za walimu wa kwenda kujitolea, malipo yao nk. Na mradi ulilenga kutatua shida za upungufu mashuleni hasa shule za vijijini. Mdogo wangu ni miongoni mwa waliochaguliwa na TAMISEMI kwenda kufundisha.
Vijana waliochaguliwa ni mia sita na points na walipangiwa vijijini ambako mazingira ni magumu mno, hakuna nyumba za walimu za kuishi, huduma hakuna maji hakuna, miundombinu migumu, mawasiliano ya shida cha ajabu halmashauri haziwapi ushirikiano wowote.
Halmashauri zinasema huo ni mzigo wa TAMISEMI makao makuu. Cha ajabu malipo walimu hawa yanaingia kupitia akaunti za shule husika.
Hii ni torture, imagine mwalimu inambidi amuombe mkuu wa shule akamtolee hiyo pesa na pesa ikiingia akaunti ya shule ina milolongo inayohusisha kuandika barua na kuipeleka kwa afisa elimu na DED Ambapo walimu wakuu huomba pesa ya mafuta kwa walimu wa kujitolea kutokana na umbali wa halmashauri zilipo nahiyo huleta migogoro kwani walimu wa kujitolea wanakuwa hawana kitu.
Ajabu hata ajira zinazotangazwa walimu hao licha ya majina yao kuwepo TAMISEMI hawaajiriwi wanaajiriwa watoto wa 2000. Na malipo yao ni laki tatu kwa mwezi bila NSSF wala bima.
Wakuu kama kuna wawakilishi wa Tamisemi makao makuu, waliangalie hili, kama hawawaajiri basi wawaboreshee namna ya kuwalipa yaani pesa iingie direct kwenye akaunti zao binafsi na sio za shule, waongeze posho walau laki nne au tano, sababu ile pesa ni ndogo ilipaswa yale mazingira akae mtu mwenye ajira ambaye atleast ana kipato cha kusurvive.
Ahsante.
Pia soma
- KERO - Walimu tulioajiriwa chini ya Mradi wa GPE-TSP unaosimamiwa na TAMISEMI tuna hali mbaya kimaslahi, hatujalipwa