Walimu wanataka Katiba mpya kama sheria mama ili iisimamie maslahi yao na sio blah blah za Waziri wa TAMISEMI

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Posts
9,863
Reaction score
20,806
Waziri wa TAMISEMI ndugu Inocent Bashungwa, tumezisikia blah blah zako kuhusu walimu na matatizo yao ambayo ni sugu tangu Uhuru.

Walimu ndio waasisi wa Taifa hili lakini serikali ya CCM ndio imewanyonga sana na kuifanya jamii iwatukane na kuwaaibisha hadi imefikia hatua hakuna mtoto anaetamani kuja kuwa mwalimu!

Serikali imeifanya kazi ya ualimu kuwa ni kazi ya kijinga, duni, isiyofaa na aibu kwa Taifa. Blah blah za matamko ya wanasiasa na wenyeviti wa vyama vya wafanyakazi hazina tija tena kwa wafanyakazi hisusan walimu hapa nchini.

Tunataka sheria mama ya kikatiba na yenye meno dhidi ya serikali maslahi yao yanapo puuzwa kama Sasa!msifanye siasa siasa kwenye matatizo ya walimu! Mmewfanya walimu kama toilet paper wakati wa chaguzi za kula kwenu na kupiga dana dana kutatua matatizo yao.

Sasa wanataka katiba mpya kama msingi wa utatuzi wa Matatizo yao na sio utashi wa wanasiasa walioshika hatamu. Muda wa Rasimu ya Warioba kufanywa katiba mpya itatue changamoto zao umefika!

Nashauri Mzee Warioba ajumuishwe kwenye kikosi kazi cha Mukandala, mchakato wa katiba mpya ukamilike mapema kabla ya uchaguzi mkuu 2025!

Blah blah na maneno na kutaka kuwalambisha asali hazitowasaidia! Nawahakikishia hakutakuwa na uchaguzi mkuu bila ya katiba mpya kupatikana!!

Endeleeni kucheza vigodoro na kukata mauno sisi kama wananchi wenye nchi na dola hatukubali uchaguzi bila katiba mpya. Hata mkiwalambisha asali wataitema wanataka katiba mpya sio maneno!

Mwambie Mama Samiah amjumuishe Warioba aanze kazi sarakasi zinaharakisha zaidi ya muda aliopewa na wenye nchi!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"

"Ukishupaza shingo, shingo itavunjika"

"Wananchi ndio wenye dola na sio wanasiasa"
 
Wakati walimu wengine wanateseka na tozo, na huo ubabaishaji wa Tamisemi; Mwalimu mwenzao mpwayungu village anazurura tu angani na mwewe ✈️! Mara yuko Uganda, mara yuko Burundi, mara yuko Rwanda, juzijuzi tu hapa alikuwa Juba Sudan!!

Yaani anafaidi tu mema ya dunia!
 
Kwani hiyo katiba mpya ilikuwa inasema nini kuhusu waalimu hebu tuwekee hapa tutathimini kama hayahitajiki marekebisho
 
Haiwezi kujadiliwa kama hatujakubaliana Mahali pa kuanzia.

RASIMU alosimamia Judge WARIOBA tukubaliane ndo iwe starting point.

Baada ya hapo ndo tujadiliane na kufanya Maboresho panapotakiwa.

Mukandala na Timu yake wanafanya hadaa kupoteza muda.

Hapatakuwa na uchaguzi wowote bila KATIBA mpya na TUME huru ya Uchaguzi.
 
Amelambishwa asali akashindwa kutema huyo!

Amesahau kuwa yeye ni mwanamabadiliko mkuu KWENYE Taifa hili!!

Namshauri awashe Moto wa katiba!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"
 
Kwani hiyo katiba mpya ilikuwa inasema nini kuhusu waalimu hebu tuwekee hapa tutathimini kama hayahitajiki marekebisho
Katiba mpya itajumuisha maslahi ya wafanyakazi na haki zao!

Jukwaa la katiba litakuwa na wajumbe wasomi watakaosimamia hoja za wafanyakazi kuhusu maslahi yao!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"
 
Haiwezi kujadiliwa kama hatujakubaliana Mahali pa kuanzia.

RASIMU alosimamia Judge WARIOBA tukubaliane ndo iwe starting point.

Baada ya hapo ndo tujadiliane na kufanya Maboresho panapotakiwa.

Mukandala na Timu yake wanafanya hadaa kupoteza muda.

Hapatakuwa na uchaguzi wowote bila KATIBA mpya na TUME huru ya Uchaguzi.
Nchi ina upuuzi Sana, Mukandala wa nini wakati anayofanya Warioba alishafanya?
 
Katiba mpya itajumuisha maslahi ya wafanyakazi na haki zao!

Jukwaa la katiba litakuwa na wajumbe wasomi watakaosimamia hoja za wafanyakazi kuhusu maslahi yao!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"
Kivipi mkuu hebu tuwekee uhalisia unaotarajiwa maana wengi wanaopigania katiba mpya ukiwauliza wanachotaka katiba mpya ifanye unagundua hawajui hata kazi na maana ya katiba
 
Wapo viongozi wa CCM waliokariri wanadhani wananchi na CDM wataendelea KUSUSIA uchaguzi muda wote na kuwaachia kuchezea SANDUKU la KURA.

Kwa changamoto tunazopitia kama Nchi, ni Hatari kudharau sauti ya HAKI.

Ameeeen.
 
Kivipi mkuu hebu tuwekee uhalisia unaotarajiwa maana wengi wanaopigania katiba mpya ukiwauliza wanachotaka katiba mpya ifanye unagundua hawajui hata kazi na maana ya katiba
Nataka Sanduku la kura liheshimiwe.

Ofisi ya waziri mkuu isihusike moja Kwa moja na uchaguzi.

Tuwe na Tume huru ya Uchaguzi ambayo ni huru, Ofisi ya Rais isiingilie Wala kuteua wajumbe wa Tume. Kenya ni mfano mzuri.

Madaraka ya Rais yapunguzwe, Asiteue majudge na mahakimu Wala kuwalipa mshahara, Ili wawe huru.

Matokeo ya Urais yahojiwe Mahakamani.

Usidhani hatujui tunataka nn!!!!;
 
Waziri wa TAMISEMI ndugu Inocent Bashungwa, tumezisikia blah blah zako kuhusu walimu na matatizo yao ambayo ni sugu tangu Uhuru.

Walimu ndio waasisi wa Taifa hili lakini serikali ya CCM ndio imewanyonga sana na kuifanya jamii iwatukane na kuwaaibisha hadi imefikia hatua hakuna mtoto anaetamani kuja kuwa mwalimu!

Serikali imeifanya kazi ya ualimu kuwa ni kazi ya kijinga, duni, isiyofaa na aibu kwa Taifa. Blah blah za matamko ya wanasiasa na wenyeviti wa vyama vya wafanyakazi hazina tija tena kwa wafanyakazi hisusan walimu hapa nchini.

Tunataka sheria mama ya kikatiba na yenye meno dhidi ya serikali maslahi yao yanapo puuzwa kama Sasa!msifanye siasa siasa kwenye matatizo ya walimu! Mmewfanya walimu kama toilet paper wakati wa chaguzi za kula kwenu na kupiga dana dana kutatua matatizo yao.

Sasa wanataka katiba mpya kama msingi wa utatuzi wa Matatizo yao na sio utashi wa wanasiasa walioshika hatamu. Muda wa Rasimu ya Warioba kufanywa katiba mpya itatue changamoto zao umefika!

Nashauri Mzee Warioba ajumuishwe kwenye kikosi kazi cha Mukandala, mchakato wa katiba mpya ukamilike mapema kabla ya uchaguzi mkuu 2025!

Blah blah na maneno na kutaka kuwalambisha asali hazitowasaidia! Nawahakikishia hakutakuwa na uchaguzi mkuu bila ya katiba mpya kupatikana!!

Endeleeni kucheza vigodoro na kukata mauno sisi kama wananchi wenye nchi na dola hatukubali uchaguzi bila katiba mpya. Hata mkiwalambisha asali wataitema wanataka katiba mpya sio maneno!

Mwambie Mama Samiah amjumuishe Warioba aanze kazi sarakasi zinaharakisha zaidi ya muda aliopewa na wenye nchi!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"

"Ukishupaza shingo, shingo itavunjika"

"Wananchi ndio wenye dola na sio wanasiasa"
Kama ni walimu wa kenta ni sawa,siyo wa hapa kwetu.
 
Kivipi mkuu hebu tuwekee uhalisia unaotarajiwa maana wengi wanaopigania katiba mpya ukiwauliza wanachotaka katiba mpya ifanye unagundua hawajui hata kazi na maana ya katiba
Wewe ndiye hujui!. Kuna mtanzania anaetumia common sense asiyefahamu kuwa hatuna tume huru ya uchaguzi, madaraka makubwa ya Rais ya kufanya anachojisikia hata Kama kinaumiza wananchi mfano tozo inayoendelea kwa kila muamala katika utawala huu wa Samia SULUHU ?. Kuna mtanzania mwenye akili timamu asiyefahamu namna akina Nape Nnauye, Januari Makamba na Mwigulu Nchemba wanavyotukejeli watanzania kuwa Kama vipi tuhamie Burundi Kama hatutaki kulipa tozo? na maneno mengine ya shombo ya aina ya Mwigulu na Nnaupe na January Makamba?. Wewe ndiye haujui kuwa watanzania wanataka katiba mpya itakayoanisha utaratibu mzuri wa namna ya kudhibiti rushwa, kudhibiti madaraka makubwa ya Rais, taasisi kupata nguvu za mamlaka za kufanya maamuzi pasipokusubiri kibali kutoka kwa watawala waliohodhi kila kitu!.
 
Back
Top Bottom