BARANGA MPINA
New Member
- Aug 28, 2022
- 3
- 1
Mwalimu John alikuwa akifundisha katika shule moja ya umma, katika kufundisha kwake Kwa miaka kadhaa, utendaji kazi wake umekuwa watofauti Sana na walimu wenzake. Ilifikia hatua walimu wenzake walishindwa kumuelewa kabisa, hali iliyopelekea utendaji wake wa kazi kuwa ni wa Maswali mengi sana.
Siku moja, siku ya Jumatatu asubuhi na mapema baada ya mwalimu John na walimu wengine kuwasili shuleni pale, mkuu wa Shule aliitisha kikao, kikao kile kilikuwa ni kujadili matokeo ya mitihani ya wanafunzi, kwani wanafunzi walikuwa wamefanya mtihani wao wa mwezi kama ilivyo ada kwenye shule Ile, hivyo baada ya majadiliano ya kina mkuu wa Shule aliwaomba walimu waeleze ni hatua gani au adhabu gani zitolewe Kwa wanafunzi walifanya vibaya katika mitihani Yao.
Katika kikao kile kila mwalimu alipendekeza adhabu ambayo yeye binafsi aliona inafaa, wapo waliopendekeza kuwa, kila mwanafunzi aliyefeli anatakiwa apewe kazi ya kulima matuta kumi ya shamba la mihogo kwenye Shamba la shule, wengine hawakuishia hapo walipendekeza kuwa wanafunzi wote waliofeli pamoja na adhabu ya kulima, pia wapatiwe majukumu ya tafuta kuni, kutafuta maji na wengine kufyatua tofali kadhaa kwaajili ya ujenzi wa uzio wa shule.
Hali ilikuwa tofauti Kwa mwalimu John, kwani, yeye alikuwa kimya muda mwingi wa kikao, hivyo, mkuu wa Shule akalazimika kumuuliza kulikoni, ndipo mwalimu John akavuta pumzi ndefu kisha akamshukuru mkuu wa Shule Kwa kumpa nafasi ya kuchangia, mwalimu John Kama ilivyo kawaida yake, aliwatazama walimu wenzake wote, kisha akasema kuwa yeye haungi mkono adhabu yoyote ile iliyopendekezwa na walimu kutolewa kwa wanafunzi waliofeli, kwani kwakweli haitawasaidia na kama itawasaidia basi haitawajenga.
Baada ya hapo Walimu wote walishangaa sana na kumtaka mwalimu John aeleze kwa kina ni kwanini anapingana nao, mwalimu JOHN alilazimika kuelezea madhara ya adhabu hizo Kwa wanafunzi, alieleza Kama ifuatavyo,
Kutolewa Kwa adhabu ambazo ni kazi zinawafanya wale wote wanaofaulu waone ya kwamba kumbe kazi ni sehemu ya adhabu na wataona kwamba kumbe kazi zinafanywa na watu waliofeli, na kwa kawaida shuleni pale mwanafunzi akifeli alitafsiriwa kuwa ni mtu asiyekuwa na akili, hivyo mwalimu John akasema adhabu hizo zitawafanya wanafunzi wadhani ya kwamba kazi za kutumia misuli ya mwili NI adhabu na hivyo zinafanywa na watu waliofeli na watu wasiokuwa na akili.
Baada ya hoja ya Kwanza mwalimu John aliendelea kusema, kazi mfano kulima, kutafuta kuni, maji kufukia visiki,n.k, zinatakiwa kutolewa Kama chachu au motisha na hasa zitolewe zaidi Kwa wanafunzi wale walifanya vizuri zaidi kwenye masomo yao, mfano, mtoto aliyefanya vizuri Sana darasani kuliko wanafunzi wenzake wote, anatakiwa apewe kazi ya kufanya, mfano kulima matuta kumi ya Mboga za majani kwenye bustani ya shule, huku Yule aliyefeli anatakiwa asipatiwe kabisa kazi yoyote ya kufanya, anatakiwa akifika darasani akae darasani na asiruhusiwe kabisa kufanya kazi Kama sehemu ya adhabu. Hili litasaidia kuwajengea fikra ya kwamba kazi ni sehemu ya mibaraka ambayo mtu hupata baada ya kufanya vizuri katika Jambo fulani.
Mwanafunzi aliyesoma kuanzia shule za awali, shule za msingi Hadi shule za upili, mpaka chuko kikuu ambaye atakuwa katika kusoma kwake amejengewa fikra ya kwamba kazi ni sehemu ya mibaraka kamwe hawezi kuogopa kufanya kazi fulani, na kamwe hawezi kuwa ni mtu wa kutumia njia za mkato kutaka kujipatia kipato, kwani akili yake itakuwa ikifahamu ya kwamba kazi ndio chanzi cha mapato na sio vinginevyo. MTU huyu anaweza kufanya kazi hata bila kutegemea ujira kwani kwake kazi ni sehemu ya furaha na kazi kwake itakuwa ni kipimo cha utu na uaminifu wake ya kwamba amepewa sio kwaajili ya kujinufaisha bali ni kwaajili ya upendeleo na kuhudumia jamii husika inayomzunguka, ujira unakuja kama matokeo ya kazi.
Baada ya maelezo mafupi ya mwalimu John, mkuu wa Shule alisimama na kusema, wakati yeye anasoma miaka ya Nyuma wanafunzi walikuwa wakipewa kazi za kufanya kila mwanafunzi alikuwa na eneo lake la kazi, ya kwamba mwanafunzi WA SHULE ya msingi alikuwa anahitimu darasa la Saba akiwa tayari anajua shughuli mbalimbali za kijamii ambazo zingeweza kumuingizia kipato, mfano, mwanafunzi huyu alikuwa anaweza kulima bustani ya Mboga na Mboga hizo zikakua kwa uzuri na akaweza kuziuza sehemu mbalimbali, hivyo hivyo kama ni sehemu au maeneo ya ufugaji, mtoto aliweza kumaliza shule alikuwa misingi yote ya kufuga mifugo au kuchunga mifugo na ikaweza kuzaliana Sana
Mwalimu Masumbuko ambaye alikuwa ni mwalimu wa taaluma katika shule ile alisimama na kusema, inawezekana kumbe tatizo la ajira kwa sasa msingi wake umeanzia kwenye Mfumo wa elimu, tena sio chuo kikuu pekee Bali ni kuanzia shule za misingi hadi shule za upili ya kwamba wanafunzi wamekuwa wakifahamu ya kwamba kazi zinazoshughukisha misuli mfano, Kilimo cha mihogo na viazi, kazi ndogo ndgo za vibarua Kama vya ufundi n.k zionekane kama ni kazi za watu wasiostaarabika, yaani kazi za watu walioshindwa maisha, ni vigumu sana kumkuta kijana aliyemaliza Shahada ya uzamivu akiwa ameshika Jembe la mkono akiwa analima kule kijijini Songambele, kwanini, ni kwasababu ya Elimu yetu ilivyo.
Kuna nchi moja jilani yetu, kuna vijana wengi Sana wenye Elimu ya Shahada za umahiri au uzamivu wanaofanya kazi Kwa kutumia nguvu zao wenyewe kulima Kilimo mbalimbali mfano, kuotesha miche ya miti, kulima matikiti n.k, huenda wao wanasaidiwa na Mfumo wao wa elimu wao ulivyo.
Mwalimu John akaomba kuongezea ya kwamba vijana tuna tatizo la kuwa na mitaji huenda ndio sababu inayofanya tukumbane na uchaguzi mkubwa wa kazi, lakini akaongezea Kwa kusema mtaji mkubwa ambao vijana tunakosa ni akili na namna tulivyo soma, wahenga wanasema mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe, ya kwamba vijana katika makundi mfano ya vijana kumi kumi wanaweza kufika katika vijiji mbalimbali mfano vijiji vya mkoa wa Njombe ambako wanaweza kupata Kazi zisizohitaji mtaji, yaani zinahitaji nguvu zao tu kuweza kujipatia pesa, Kama vile kuchukua tenda za kulima mashamba Kwa kutumia majembe ya mkono na hatimaye kupata Pesa wanazoweza kuzitumia katika uwekezaji mwingine zaidi.
Baada ya maongezi hayo, mkuu wa Shule alisimama na kufunga mjadala na walimu wote kukubaliana ya kwamba hawatotoa kazi kama adhabu na badala yake kutafuta namna nyingine ya kusaidia watoto ikiwa ni pamoja na kumshirikisha wazazi, sio kwaajili ya matokeo ya darasani tu, bali kwaajili ya taifa kwa ujumla.

Upvote
2