Walimu wapya mmejiandaaje kuripoti vituo mtakavyopangiwa?

Walimu wapya mmejiandaaje kuripoti vituo mtakavyopangiwa?

Mimi naomba kujua mwalimu wa degree anaanzia na mshahara kiasi gani basic na kiasi gani kinabaki ( take home) baada ya makato yote kukatwa
 
nasikia watakao ripoti cheti cha kuzaluwa ni muhimu(original) sasa rafiki yangu(wa kike) katika harakati za hapa na pale alikipotrza ilanalibaki na nakala zake hii inaweza kuwa kikwazo kwake ktk kupokelewa.huko atakako kuwa kapangiwa?

vyeti lazima kwani lazima wakague na kutuma hazina.
kama hana maybe police report inaweza ikasaidia
 
Nacomba kuuliza kuwa mnaporipoti mnatakiwa Kwanzaa kufika kwa mkurugenzi au kwa mkuu wa Shule,na Je pesa ya kujikimuv. Kwa shahada ni shl ngapi??
 
Makaura;

usikubali kufungua a/c NMB,utajuta! Benki hii ina urasimu wa ajabu ajabu„folen zisizo na kichwa wala miguu ;ATM zao zipo slow sana na muda mwingi hukata network hivyo huleta usumbufu kwa wateja!
NAKUSHAURI NENDA CRDB wapo vizuri sana hutajutia

ndg yangu nakushaur ufungue nmb sababu ukiwa mwl halaf ukifungua benk nyngne salar yko itachelewa halaf kuna wlaya nying hakuna hakuna benk nyngne zaid ya mmb
 
Last edited by a moderator:
kwel ila hao wenyew wamezungumza kwamba safar hii itakuwa n tofauti yaan huo mwez unaoenda kuripoti basi mwisho wa mwez wake unaanza kuchukua mshahara

Unachokisema kinaweza kuwa kweli, maana hata ajira za mwaka jana ilikuwa hivyo karibia nchi nzima, wengi walipata mshahara mwezi huo huo, bila shaka mpaka sasa kwa watu walioajiliwa mwaka jana hakuna mtu mwenye malimbikizo ya fedha serikalini!
 
1. Usisahau kununua Tochi kutokana na Giza la vijijini ni kubwa sana hivyo unaweza kuumwa na nyoka najua kuna watu wamezaliwa Dar-es- salaam wasitegemee kuishi maisha ya Dar-es-salaam taa nyingi.

2. Mwalimu mpya kumbuka Kuchukua mafuta ya taa ya kutosha kwani Hivyo vijiji mnavyopangiwa havina hata umeme wa REA hivyo mafuta ya taa yatawasaidia kuangazia ndani kwako.

3: Baiskeli Kumbuka mwalimu unaenda porini hivyo baiskeli itakusaidi kufata mshahara wako huko halimashauri Unaweza kuendesha baiskeli kwa siku tatu hivyo kukurahisishia Safari hivyo baiskeli ni muhimu Kwani unaweza hata kuchotea maji pia kwani vijiji vingi havina huduma ya maji iliyokaribu sana ukiweza hata piki piki itakusaidia Pia.

4. Dagaa wa kutosha ifahamike kuwa vijijini hakuna Bucha na mara nyingi wanapenda kula vibudu (wanyama waliojifia) huwa hawachinji kwani kumchinja ng'ombe hupunguza utajiri hivyo Huwezi kula majani ya maboga mwaka mzima kama binadamu dagaa zitakusaidia sana.

5.Redio kuajili ya Kupata taarifa mbalimbali hasa mpira na taarifa ya habari kwani vijiji vingi havina mitandao ya simu hivyo hutaweza ku access mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook na WhatsApp hivyo redio ina umuhimu ikizingatiwa kuwa magazeti hufikaga huko baada ya miezi miwili nayo utayakuta kwenye duka yakifungiwa bidhaa.

6. Panga au shoka ikumbukwe kuwa vijijini watu wengi hutumia Kuni hivyo mkaa haupo hivyo panga litakusaidia wakati wa kutafuta kuni.

Nilikua kwa Bibi Huko SHULE YA MSINGI IYOMBAKUSOVYA Huku wilayani SIKONGE hakuna waalimu kabisa pia Katika Shule ya msingi CHINYANG'UKU hakuna kabisa waalimu hivyo naomba mfike huko!

Mwisho ewe Mwalimu Ukipangiwa kituo kumbuka Kulipoti mapema!
 
hahaha bora umewakumbusha, na mwaka huu hakuna uhamisho
 
Ndugu Walimu kijijini ndo safari yetu saivi ko 2jadili zana muhimu zakukabili mazingira hayo.
 
SERIKALI imesema ajira za walimu wapya
zitaanza rasmi Mei Mosi, mwaka huu huku
ikiweka wazi kuwa walimu hao wasitegemee
kupangiwa katika maeneo ya majiji,
manispaa na miji.
Walimu hao wametakiwa kutotegemea
kupangiwa katika maeneo hayo kutokana na
idadi ya walimu waliopo ni kubwa na inakidhi
mahitaji, huku maeneo yaliyopewa
kipaumbele ni vijijini na halmashauri ambazo
zina mahitaji na upungufu mkubwa wa
walimu.
Idadi ya walimu wapya watakaoanza ajira
zao mwezi ujao ni 31,056 ambapo kwa
walimu wa ngazi ya Cheti ni 11,795,
Stashahada (Diploma) 6,596 na wenye
Shahada (Degree) 12,665.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
ajira mpya za walimu kwa mwaka
2014/2015.
Alisema kwa mwaka huu ajira hizo
zimechelewa kutokana na TAMISEMI pamoja
na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
kufanya ufuatiliaji wa kina hadi katika ngazi
ya shule ili kubaini kwa uhakika mahitaji
halisi ya walimu kwa kila halmahauri na
shule.
“Ufuatiliaji huo umebaini kuwepo kwa
halmashauri na shule hasa za mjini zenye
walimu wa ziada na zingine hasa za vijijini
zina upungufu mkubwa wa walimu,” alisema
Sagini.
Alisema taarifa hizo zimesaidia kuwapanga
walimu wapya kwa usawa ili kuondoa
uwiano usioridhisha kwenye maeneo mengi
ya vijijini. Alisema kwa sasa wanakamilisha
taratibu za kupata kibali kwa ajili ya ajira za
walimu na fedha za kuwalipa stahili zao ili
waanze ajira zao rasmi mwezi ujao.
Aidha, alisema orodha ya walimu na vituo
watakavyopangiwa vitawekwa katika tovuti
ya Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ambayo
ni www.pmoralg.com na ya Wizara ya Elimu
www.moe. go.tz ifikapo Aprili 24, mwaka
huu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa
TAMISEMI, Zuberi Samataba alisema, pia
ufuatiliaji huo ulikuwa ni kuhakikisha
wanakuwa na taarifa sahihi za walimu
wanaoajiri wote ni wapya ambao
hawajawahi kuajiriwa ili kuepuka usumbufu
kwa walimu ambao hawatoi taarifa.
Alisema baadhi ya walimu ambao
wameshaajiriwa wanapoenda kusoma,
hupangiwa upya vituo na hawatoi taarifa
hivyo kuleta usumbufu wa kuchelewa
kutopata mishahara yao.
“Kuna baadhi ya walimu wameshaajiriwa
kwa hiyo jina linapoingizwa katika taratibu
za malipo, linagoma kuingia ndipo ukifuatilia
unajua alikuwa ameajiriwa, inabidi
umwambie arudi kwa mwajiri wake.
Kwa hiyo kwa hawa walimu wapya
nawashauri waende kuripoti katika vituo
walivyopangiwa na wakubali kufanya kazi
katika maeneo hayo, sio waripoti halafu
waondoke,” alisema.
 
Umefanikiwa kusomea ualimu na kuhitimu
mafunzo yako ya ualimu 2014/2015 na
kusubiri wapi utapangiwa kituo cha kazi . Wapo
wanaosubiri kuangalia wamepangiwa wapi na
wakiona wamepangia kijijini eti wanawaza
kutoripoti kituoni , ndugu kama haya ndiyo
mawazo yako basi badili leo hii .
Wote tukikataa kufanya kazi vijijini nani
ataenda kuwakomboa hawa wanakijiji walio
wengi Tanzania ?
Maisha mazuri yanapatikana popote pale
kulingana na akili yako ya kutumia fulsa
zilizopo hapo ulipo na kujituma kwa kazi
yoyote ile ulibahatika kuipata . Mshukuru
Mungu kwa wewe kupata kazi hiyo ya ualimu .
Wapo waliokataa kazi ya ualimu miaka kumi
iliyopita lakini mpaka leo hii wapo mtaani
wanazunguka na bahasha kutafuta kazi na
hawapati . karipoti kituoni kwako ulikopangia
mapema ipasavyo na fanya kazi hiyo kwa
moyo wote .
Kwa wale wenye mtazamo wa kuwa
watafanya kazi miaka miwili tu ili wabadili fani
hiyo ya ualimu na kusomea vitu vingine pia
wamepotea . Kasomee kitu kingine kama una
uhakika wa kupewa kazi na mtu
unayemfahamu la sivyo utajuta kama utaende
kusomea fanihiyo nyingine na kuacha kabisa
kazi ya ualimu uliyokwisha ipata .
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa-( TAMISEMI ) itatangaza ajira
za Walimu kwa mwaka 2014 /2015 ngazi ya
Cheti , Stashahada na Shahada wakati wowote
kuanzia sasa . Endelea kufuatilia hapa upate
kujua umepangwa wapi !
Unaweza kutumiwa taarifa kwenye email yako
kwa kujiunga hapa dakika 2 tu
Kwa mtazamo rahisi kabisa kati ya mwalimu
anayefanya kazi kijijini na mwalimu
anayefanya kazi mjini unadhani nani atakuwa
anakaa na pesa muda mrefu kabla ya
mshahara mwingine ? Mjini matumizi ni mengi
kuliko kijijini hili huwezi kupinga ukipinga
wewe asili yako ni ubishi tu . Kwahiyo
usichague sehemu ya kufanya kazi enzi hizi
za kikwete . Kipindi cha hayati J . K . nyerere
ungeweza kuchagua sehemu ya kufanya kazi
kwakua wataalamu walikuwa wachache leo
hiii wasomi ni wengi ajira hazitoshi .
Nende kijiji kijana ukalete maendeleo.
Ukiwafundisha watoto hawa waliosahaulika
kwa baadhi ya huduma utabarikiwa zaidi na
Mungu wako . Isitoshe tuliowengi tumekulia
vijijini au tumezaliwa vijijini sasa jiulize kama
walimu waliokufundisha wewe ulipokuwa
kujijini nao wasingekuja kuripoti wewe muda
huu ungekuwa wapi kama sio kuchunga mbuzi
za babu au za baba yako ailizorithishwa na
baba yake .
Kuwa mzalendo kwa hili ewe uliyesomea fani
ya ualimu . Kuanzia leo kama ulikuwa unasema
nimesomea ualimu basi tu nilitaka kuwa
mwanasheria badili mtazamo wako na furahia
kazi hiyo ya ualimu utaona manufaaa yake
baada ya muda mfupi tu .
Unaweza kuwa umeharibiwa saikolojia yako na
jamii kwa kusikia kuwa eti walimu wanalipwa
mishahara midogo . Si kweli ukilinganisha na
maisha halisi ya kazi ya ualimu . Mbona
walimu wanajenga nyumba nzuri wananunua
magari mazuri hata kuliko afika yoyote
mwingine wa serikalini unakotamani wewe
ungekuwepo . Hata ukipata mshahara wa
mabilioni kwa mwezi hautakutosha
mwanadamu. Kadili unavyopata mshahara
mkubwa ndivyo matumizi yako yanavyokuwa
makubwa zaidi
Kama umenielewa bonyeza alama ya f t g
hapo chini kisha share makala hii kwa rafiki
waliopo huko facebook, twitter na google plus
nao waungane nasi kuleta mabadiliko chanya
kwenye jamii yetu .
Basi napenda niishie hapa kwa walionielewa
nawashukuru na kwa wasionielewa
nawashukuru pia maana yake hata
nisipowashukuru hawawezi kunielewa .
Kama bado hujajiunga na mtandao huu wa
chatguest ili tukutumie taarifa siku majina ya
walimu wapya 2015 yatakapotangazwa basi
jiunge kwa kubonyeza hapa Utatumiwa taarifa
kwenye email yako kukujuza kuwa idara
husika imeshatangaza majina ya walimu
wapya waliopangiwa vituo vya kazi 2015
 

Attachments

  • 1429503275533.jpg
    1429503275533.jpg
    66.8 KB · Views: 378
mkuu ualimu ndio una furahi hivi kweli tanzania kuna umaskini wa hali ya juu sana.

Daaaah yani wejamaaa laiti ungekuaa unawajuaa wanafunzi niliosoma nao advanced level mh wangekupa tarifa zangu kuwa since form 5 lengo langu nikuwa mwalimu na sasa my dream inatimia so niachenijipe raha kwa kutimiza malengo yangu.

Istoshe its non of ua bsnc
 
Vile vile kama mimi ni maskini sawa je wewe tajiri mbona baba yako hakufungulii kampuni ili akuhurumiee unavyozurura na bahasha za kaki mji mzima?

mimi maskini bt hakika mwisho wa mwezi may ntatiaa 518000 takoni wakati wewe bado unang'aaa sharubu tu kitaaaa,,,, vile vile kusimamia uchaguzi October inanihusu zote hizo pesa bado kuandikisha daftari la kudumu bado inanihusu.

SHALET hujielewi kabisa yani au wewe wazani mtu huzaliwa na utajiri??????
 
Vile vile kama mimi ni maskini sawa je wewe tajiri mbona baba yako hakufungulii kampuni ili akuhurumiee unavyozurura na bahasha za kaki mji mzima?

mimi maskini bt hakika mwisho wa mwezi may ntatiaa 518000 takoni wakati wewe bado unang'aaa sharubu tu kitaaaa,,,, vile vile kusimamia uchaguzi October inanihusu zote hizo pesa bado kuandikisha daftari la kudumu bado inanihusu.

SHALET hujielewi kabisa yani au wewe wazani mtu huzaliwa na utajiri??????

😕 Ahahah shida ya kaz ya ualimu haina posho yan mwendo wa.salary tu
 
Swala la posho tuachiee sisi tunajuaa tuapata vipi.

Ualimu ni miongoni mwa kada ambayo serikali haikubanii muda wa kufanya mambo yako kitaani sasa sisi huo muda ndo posho yetu.
Hakili kumkichwa kuutumiaa huo muda ktk kuingiza kipato
 
Back
Top Bottom