Utakapoliona jina lako na sehemu ulipangiwa, hakikisha kwamba:
1) Ndani ya siku 3 tayari umeshafungasha virago vyako kuelekea ulipopangiwa- hii itakusaidia kwenda kuyajua mazingira yako ya kituo cha kazi na jinsi utakavyopambana na changamoto za chaka.
2) Hakikisha umebeba vyeti halisi na wala sio photocopy- hii itakusaidia kuondoa usumbufu wa kukuingiza kwenye system ya mshahara maana nilishawaonaga walimu wengi pale baraza la mitihani (NECTA), wakiwa wanahangaika wakati wenzao wapo vituo vya kazi.
3) Hakikisha angalau una kianzio(pesa) ya kujikimu angalau ya siku 2 kuepuka usumbufu unaoweza kutokea halmashauri zenu- kuna walimu nilishawaonaga walienda kuomba kulala kwa mwenyekiti wa kijiji... Nasisitiza hasa kwa wadada mana hii huwaga ni advantage ya watu wengine kutaka kuwarubuni wadada walimu ili watoe papch.
4) Kwa wale wajasiriamali (entrepreneur) hakikisha unayasoma mazingira vizuri ili usije ukategemea mshahara pekee- nimewahi kuwaona walimu wakilalamika tarehe za mwanzo kuwa mshahara umekata.
5) Fanya kazi kwa bidii kuleta tija katika hili taifa kwa kuwa ualimu ni sawa na mapigo ya moyo ya taifa.
6) Achaneni na mambo ya mikopo wakati ndio kwanza hata mwaka hujamaliza sjui sacos, vicoba au hata mabenk makubwa. Nimewahi kuona walimu wakilia sana jamaa walikuja kusafisha chumba.
7) Chagueni mifuko ya kibima yenye makato nafuu, hapa unatakiwa uwe makini sana bila kukurupuka.
8) Changamoto ni nyingi sana ila naimani mlifundishwa vyuoni jinsi ya kukabiliana nazo, hii sio kwenye ualimu pekee bali kwenye kada zote.
9) Kujifunza kusave mshahara ni kitu muhimu sana ili kufikia malengo uliyojiwekea itashangaza kuona mwalimu umefanya kazi mwaka mzima bila kuwa na mradi wa nyongeza.
10) MWISHO NAWATAKIA WALIMU WOTE TARAJALI HERI NA MAFANIKIO MEMA KUELEKEA AJIRA MPYA.