Walimu wapya mmejiandaaje kuripoti vituo mtakavyopangiwa?

Walimu wapya mmejiandaaje kuripoti vituo mtakavyopangiwa?

Watu watayakumbuka hayo uliyosema wakiwa eneo la tukio ila wengine hawana jinsi wanataka kujiandaa ila mambo hayaendi bas balaa tu kweli maisha ni magumu jaman daah
 
(certificate) 296,000/= (diploma),432,000/= serikali iangalie mishahara jamani maana hii mishahara IDARA nyingine ni POSHO
 
Nawasalimu
Kwa Wale Wenzangu Na Mimi Mlopangwa Ajira Mpya Za Ualimu Tusijisahau Kuwa Na Transcript Ya Semister Zote. Jambo Hli Nimekumbushwa Mara Nyingi Sana Na Walionitangulia Na Nimetoa Tahadhari Kwakua Huwa Linawarudisha Wengi Chuoni.
Mbarikiwe SANA.
 
Pia wawe na cheti cha kuzaliwa. Na pass ports kama nne za rangi. Wawe na akaunti kuepuka kero.
 
Yap ndugu kachukueni mie nimeingia Dom leo kesho naanza mchakato wa kuchukua Transcript.
 
Kachukueni transcripts jamani msije mkapishana na gari la mshahara la mwezi wa nne. Linarudi ndio unakwenda.
 
Kachukueni transcripts jamani msije mkapishana na gari la mshahara la mwezi wa nne. Linarudi ndio unakwenda.

Mkurugenzi anataarifa zote zituhusuzo, suala la vyeti ni mpaka vitakapo toka.

Nadhani unaukumbuka uzi huu.

Ni vitu gani muhimu Mwalimu unavyotakiwa kuwa navyo wakati wa kuripoti kazini?

na mwalimu huyu akatoa maelezo haya.

  • Academic Certificates - Form 4, Form 6 kwanza - Vitahitajika ,
  • Vyeti vya vyuo vitafuata baada ya kuwa vimetoka vitatumika kama viambatanisho ujazapo fomu za TSD ili kupata TSD Number.
  • Passport size, andaa za kutosha maana maeneo mengine huduma za picha huwa ni shida.
  • Kimsingi huwa hakuna usumbufu wowote sababu taarifa zako huwa tayari Mkurugenzi anazo.

binafsi nilimuelewa, zaidi ya hapo mwenye uwezekano wa kufanya hivyo afanye, maana tunatofautiana.
 
Back
Top Bottom