Makuku Rey
JF-Expert Member
- Dec 31, 2013
- 3,497
- 3,823
Sasa umelipwa siku 3 badala ya siku 7, nusu iko wapi hapo??
Nipo Tabora urambo napo hali ni tete walimu wa shahada tumepewa hela ya siku 4 huku wa primary wakipewa yote, tulipohoji tumeambiwa hela ya walimu wa shahada imekuja ya siku nne tu na nyingine watatoa.
Kiukweli walimu tunadharauliwa sana,yani hatuthaminiwi kabisa,mtu katoka IRINGA HADI TABORA URAMBO,badala ya kuwapa hela yote unampa nusu,dawa ni kusepa tu maana hawatujali.
Wakuu nimefka kwenye halmashauri niliyopangiwa kwa ajili ya kuanza kazi(njombe),lakini pesa ya kujikimu imetolewa nusu. KWA SHAHADA TSH-45000@siku, HALMASHAURI imetoa pesa ya siku 3 badala ya siku saba, wanadai eti serikali haijaleta pesa zote! WALIMU WENZANGU HUKO MLIKOLIPOTI PIA KUNA TATIZO KAMA HILI? au ndo ukiona manyoya............
Kabla ajira hazijatangazwa mlikuwa mnasumbua kweli na mlikuwa na hamu ya kwenda kuripoti. Wengine Posti zilipotoka mlitamani mkaripoti siku hiyohiyo.
Kama meenda kwa Lengo la kupiga hela jueni kuwa serikali haina Pesa. Kafanyeni kazi