Walimu wapya walioripoti makazini Halmashauri ya Mbinga wahenyeshwa

Walimu wapya walioripoti makazini Halmashauri ya Mbinga wahenyeshwa

Teleza1

Senior Member
Joined
May 16, 2020
Posts
190
Reaction score
198
Walimu walioripoti vituo vyao vipya vya kazi kuanzia tarehe 1 mpaka 14 Desemba katika Halmashauri Ya Mji wa Mbinga wameendelea kupata shida huku wakiwa hawajui hatima yao.

Mpaka sasa hawajapewa fedha yao ya kujikimu na wameendelea kusumbuliwa bila kujua hatma yao. Wenzao wa wilaya ya mbinga wameshapata pesa zao.

Tatizo kubwa la kucheleweshwa kwa pesa hizo ni kutokana Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutokuwepo ofisini mara kwa mara. Waalimu wengi wanahangaika maisha ya tabu na mashule yanafungwa hali itakuwa mbaya kwa waalimu wapya.

Labda waamuue kuwa wavuvi ziwa nyasa. Tamisemi tunaomba kwa heshima na taadhima imuangalie mkurugenzi wa halmashauri hii.
 
Pole sana, umeongea kwa hisia sana kama vile na wewe ni muhusika. kwa nini ukasomea ualimu, ualimu ni kazi ngumu sana kumbuka Yesu alikuwa mwalimu akaishia kusulubiwa. Aliyeleta uhuru nchi hii alikuwa mwalimu lakini ualimu haupewi heshima kama ubunge
 
Vp unaukumbuka huu uzi wako wakati ukitafuta ajira?

 
Walimu walioripoti vituo vyao vipya vya kazi kuanzia tarehe 1 mpaka 14 Desemba katika Halmashauri Ya Mji wa Mbinga wameendelea kupata shida huku wakiwa hawajui hatima yao..
Mbona Halmashauri/ wilaya / Manispaa nyingi tu hawajalipwa boss.
 
Walimu walioripoti vituo vyao vipya vya kazi kuanzia tarehe 1 mpaka 14 Desemba katika Halmashauri Ya Mji wa Mbinga wameendelea kupata shida huku wakiwa hawajui hatima yao...
Kizazi cha kulalamika, kizazi cha kuhisi kinaonewa.

Hivi kabla ya ajira ulikuwa unaishije?

Kazi hujaanza ushaanza kulalamika hela kuchelewa.

Ngoja nikifunze jambo, kuna kada huwa zinaajiriwa hazipewa hela ya kujikimu na salary inaweza kuchukua hata miezi mitatu haijaanza kutoka, ingekuwa ndio wewe siungeenda kwa Rais kabisa?

Kuna kada huko hawanaga hiyo hela unayolilia wewe na mshahara hauji hata miezi kadha na mtu anakomaa huoni akifungua uzi humu wala nini.

Acha kulialia, kama hela ipo utalipwa ukiona inachelewa fanya issue zingine acha kazi hiyo maana wanachelewesha hela.
 
Vumilia tu na shukuru hata umepangiwa, kuna wenzako hawajapangiwa kabisa.
 
Watanzania tunapenda sana kulalamika, wakati haujapata ajira ya ualimu ulikuwa unalalamika, umepata ajira unalalamika. Mshukuru Mungu ata umepata iyo ajira.
Hivi umerogwa ama? Hivi huyo mkurugenzi angekuwa ni yeye angeweza kuvumilia kuishi maisha ya shida? Kama serikali imetoa pesa kwanini walimu wasipewe stahiki zao?
 
Yaan hata Mwezi haujaisha tayari mshaanza kulalamika,subirini Basi mtapatiwa tu stahiki zenu ,wanawajali sana ndomaana mkapatiwa ajira
 
Back
Top Bottom