Magema Jr
JF-Expert Member
- Apr 22, 2020
- 1,299
- 1,197
😢😢Kwa Tanzania ualimu ni laana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😢😢Kwa Tanzania ualimu ni laana
Yani kupata MTU unae mdai pesa ya kujikimu unataka hadi wana JF wajue kuwa unadai pesa ya kujikimu.Hivi umerogwa ama? Hivi huyo mkurugenzi angekuwa ni yeye angeweza kuvumilia kuishi maisha ya shida? Kama serikali imetoa pesa kwanini walimu wasipewe stahiki zao?
Pesa itolewe acha longolongo weweYani kupata MTU unae mdai pesa ya kujikimu unataka hadi wana JF wajue kuwa unadai pesa ya kujikimu. Kweli umasikini uliopitiliza unaondoa akili ya kufikiri. Hawa ndio walimu tunaotegemea watufundishie watoto wetu, mtu kaajiliwa juzi leo namshtaki mwajiri wake mtandaoni. Stupid
Kwani watu wanatafuta ajira ili wafanye kazi bila kupokea stahiki zao?Watanzania tunapenda sana kulalamika, wakati haujapata ajira ya ualimu ulikuwa unalalamika, umepata ajira unalalamika. Mshukuru Mungu ata umepata iyo ajira.
Kwahiyo kwa mtazamo wako unaona mambo ndivyo inabidi yawe? Kama wabunge hata kabla ya kuapishwa wanapeleka account zao, majina ya watoto na wenza wao halafu pesa inaingia mapema tu kwanini isiwe kwa kada nyingine?Kizazi cha kulalamika, kizazi cha kuhisi kinaonewa.
Hivi kabla ya ajira ulikuwa unaishije?
Kazi hujaanza ushaanza kulalamika hela kuchelewa...
Walimu walioripoti vituo vyao vipya vya kazi kuanzia tarehe 1 mpaka 14 Desemba katika Halmashauri Ya Mji wa Mbinga wameendelea kupata shida huku wakiwa hawajui hatima yao.
Mpaka sasa hawajapewa fedha yao ya kujikimu na wameendelea kusumbuliwa bila kujua hatma yao. Wenzao wa wilaya ya mbinga wameshapata pesa zao.
Tatizo kubwa la kucheleweshwa kwa pesa hizo ni kutokana Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutokuwepo ofisini mara kwa mara. Waalimu wengi wanahangaika maisha ya tabu na mashule yanafungwa hali itakuwa mbaya kwa waalimu wapya.
Labda waamuue kuwa wavuvi ziwa nyasa. Tamisemi tunaomba kwa heshima na taadhima imuangalie mkurugenzi wa halmashauri hii.
bado yupo bize anajibu hoja za gari, kwa kadri ya maagizo ya kiraja mkuu wa serikali!! mpeni nafasiWalimu walioripoti vituo vyao vipya vya kazi kuanzia tarehe 1 mpaka 14 Desemba katika Halmashauri Ya Mji wa Mbinga wameendelea kupata shida huku wakiwa hawajui hatima yao.
Mpaka sasa hawajapewa fedha yao ya kujikimu na wameendelea kusumbuliwa bila kujua hatma yao. Wenzao wa wilaya ya mbinga wameshapata pesa zao.
Tatizo kubwa la kucheleweshwa kwa pesa hizo ni kutokana Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutokuwepo ofisini mara kwa mara. Waalimu wengi wanahangaika maisha ya tabu na mashule yanafungwa hali itakuwa mbaya kwa waalimu wapya.
Labda waamuue kuwa wavuvi ziwa nyasa. Tamisemi tunaomba kwa heshima na taadhima imuangalie mkurugenzi wa halmashauri hii.
Naona mmenishambulia vibaya lakini naogopa kuweka wazi mambo mengine kwani mkurugenzi ni mlozi sana
Kweli tupu!Kwa Tanzania ualimu ni laana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaah wee mchokozi.Jiandaeni kisaikolojia pesa mtapewa pasaka huko mwezi april.
Kama hakuna tofauti ya kuajiriwa ualimu na kutokuwa na kazi kwa nini asilalamike. Mtu akiajiriwa ni lazima apate haki zinazokuja na ajira. Kwa nini azungushwe na haki yake. Wengine wametoka mbali, hawana ndugu huko waliko, sasa watakula nini?Watanzania tunapenda sana kulalamika, wakati haujapata ajira ya ualimu ulikuwa unalalamika, umepata ajira unalalamika. Mshukuru Mungu ata umepata iyo ajira.
Hata wewe itakushinda utakapoo kaa miezi bila stahiki zako. Pamoja kuwa ualimu ni kazi ya wito lakini haina maana ni kazi ya kujitolea. Kazi hii imnaitwa ya wito kwa sababu hailipi vizuri, vituo vya kazi mara nyingne vinakuwa kwenye mazingira magumu. Wakati mwingine kufikia kituo cha kazi inabidi ujitwishe sanduku na kutembea km nyingi. Kwa hiyo inahitaji moyo kuwa mwalimu. Lakini kamwe hii siyo kazi kujitolea. Kuwabeza walimu wanaodai haki ni ujinga mtupu. Kumbuka bila mwalimu usingefika hapo ulipo.Shukuru hata ulikuwemo kati ya 8000! kama unaona tabu rudi kwenu ukaendelee na ulivyoacha,tuachie sisi tuje tuzibe nafasi hiyo
Unajua maana ya posho ya kujikimu na matumizi yaliyolengwa kuhusu hiyo posho?Kizazi cha kulalamika, kizazi cha kuhisi kinaonewa.
Hivi kabla ya ajira ulikuwa unaishije?
Kazi hujaanza ushaanza kulalamika hela kuchelewa.
Ngoja nikifunze jambo, kuna kada huwa zinaajiriwa hazipewa hela ya kujikimu na salary inaweza kuchukua hata miezi mitatu haijaanza kutoka, ingekuwa ndio wewe siungeenda kwa Rais kabisa?
Kuna kada huko hawanaga hiyo hela unayolilia wewe na mshahara hauji hata miezi kadha na mtu anakomaa huoni akifungua uzi humu wala nini.
Acha kulialia, kama hela ipo utalipwa ukiona inachelewa fanya issue zingine acha kazi hiyo maana wanachelewesha hela.
Unajua maana ya posho ya kujikimu na matumizi yaliyolengwa kuhusu hiyo posho?
Kwahiyo kwa mtazamo wako unaona mambo ndivyo inabidi yawe? Kama wabunge hata kabla ya kuapishwa wanapeleka account zao, majina ya watoto na wenza wao halafu pesa inaingia mapema tu kwanini isiwe kwa kada nyingine?
Kuna watu uwa mnakubaliana mambo kuwa hovyo kama ndiyo utaratibu vile.