Walimu wapya walioripoti makazini Halmashauri ya Mbinga wahenyeshwa

Hivi umerogwa ama? Hivi huyo mkurugenzi angekuwa ni yeye angeweza kuvumilia kuishi maisha ya shida? Kama serikali imetoa pesa kwanini walimu wasipewe stahiki zao?
Yani kupata MTU unae mdai pesa ya kujikimu unataka hadi wana JF wajue kuwa unadai pesa ya kujikimu.

Kweli umasikini uliopitiliza unaondoa akili ya kufikiri. Hawa ndio walimu tunaotegemea watufundishie watoto wetu, mtu kaajiliwa juzi leo namshtaki mwajiri wake mtandaoni. Stupid
 
Pesa itolewe acha longolongo wewe
 
Watanzania tunapenda sana kulalamika, wakati haujapata ajira ya ualimu ulikuwa unalalamika, umepata ajira unalalamika. Mshukuru Mungu ata umepata iyo ajira.
Kwani watu wanatafuta ajira ili wafanye kazi bila kupokea stahiki zao?
 
Kizazi cha kulalamika, kizazi cha kuhisi kinaonewa.
Hivi kabla ya ajira ulikuwa unaishije?
Kazi hujaanza ushaanza kulalamika hela kuchelewa...
Kwahiyo kwa mtazamo wako unaona mambo ndivyo inabidi yawe? Kama wabunge hata kabla ya kuapishwa wanapeleka account zao, majina ya watoto na wenza wao halafu pesa inaingia mapema tu kwanini isiwe kwa kada nyingine?

Kuna watu uwa mnakubaliana mambo kuwa hovyo kama ndiyo utaratibu vile.
 
Walimu ingekuwa timu ya mpira wa miguu tungeiita Malalamiko fc
 

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Eti wawe wavuvi ziwa nyasaaa. Na nyavu za kuvulia watazipatia wapi ?
 
Shukuru hata ulikuwemo kati ya 8000! kama unaona tabu rudi kwenu ukaendelee na ulivyoacha,tuachie sisi tuje tuzibe nafasi hiyo
 
bado yupo bize anajibu hoja za gari, kwa kadri ya maagizo ya kiraja mkuu wa serikali!! mpeni nafasi
 
Naona mmenishambulia vibaya lakini naogopa kuweka wazi mambo mengine kwani mkurugenzi ni mlozi sana
 
Naona mmenishambulia vibaya lakini naogopa kuweka wazi mambo mengine kwani mkurugenzi ni mlozi sana
Hivi ni kweli huko wengine wameshapewa pesa ya kujikimu?.
Iringa pia mbona bado.​
 
Watanzania tunapenda sana kulalamika, wakati haujapata ajira ya ualimu ulikuwa unalalamika, umepata ajira unalalamika. Mshukuru Mungu ata umepata iyo ajira.
Kama hakuna tofauti ya kuajiriwa ualimu na kutokuwa na kazi kwa nini asilalamike. Mtu akiajiriwa ni lazima apate haki zinazokuja na ajira. Kwa nini azungushwe na haki yake. Wengine wametoka mbali, hawana ndugu huko waliko, sasa watakula nini?
 
Shukuru hata ulikuwemo kati ya 8000! kama unaona tabu rudi kwenu ukaendelee na ulivyoacha,tuachie sisi tuje tuzibe nafasi hiyo
Hata wewe itakushinda utakapoo kaa miezi bila stahiki zako. Pamoja kuwa ualimu ni kazi ya wito lakini haina maana ni kazi ya kujitolea. Kazi hii imnaitwa ya wito kwa sababu hailipi vizuri, vituo vya kazi mara nyingne vinakuwa kwenye mazingira magumu. Wakati mwingine kufikia kituo cha kazi inabidi ujitwishe sanduku na kutembea km nyingi. Kwa hiyo inahitaji moyo kuwa mwalimu. Lakini kamwe hii siyo kazi kujitolea. Kuwabeza walimu wanaodai haki ni ujinga mtupu. Kumbuka bila mwalimu usingefika hapo ulipo.
 
Unajua maana ya posho ya kujikimu na matumizi yaliyolengwa kuhusu hiyo posho?
 
Unajua maana ya posho ya kujikimu na matumizi yaliyolengwa kuhusu hiyo posho?

Wewe ndio unajua maana ya posho ya kujikimu mimi sijui ila nataka nikwambie mimi nilipata kazi kabla yako kama unaona unajua sana basi nakuhakikishia unajua utopolo tu. Kazi za Serikali ukianza kulalamika saiv ujue utalalamika mpaka unastaafu, nimekwambia kuna kada zingine hiyo posho yenyewe hakuna na salary inachukua mpaka miezi mitatu haijaanza kutoka sasa chagua kuacha kazi au kuendelea
 

Unataka kujilinganisha na mbunge? Usifananishe vitu visivyoendana. Mshahara wa mwaliku wa degree ni TGSD ambayo ni laki 7+ mshahara wa mbunge unaujua? Pensio ya mwalimu haivuki mil 100 ya mbunge mil 200+ kwa miaka mitano hilo unalijua? Maisha ni vile ulivyochagua, we ulichagua kuwa mwalimu komaa na mazingira ya ualimu wenzio walichagua kuwa wabunge hujakatazwa kuwa mbunge[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…