Walimu wapya wamedharauliwa na kupuuzwa.

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
Wakati jana raisi akitangaza nyongeza ya mshahara kuna idadi kubwa ya walimu wapya walioajiriwa aprili ambao hawajapata mshahara mfano h/mashauri ya kilindi ni walimu wapya 15 tu walioingiziwa mshahara...halmashauri zingine ni watu 10~30 waliopata mshahara..Sasa CWT inafanya nini? na inavyoonyesha ni jambo la makusudi limefanyika maana wale wa degree wengi wamepata mshahara..jamani serikali iache utani hivi umpange mtu porini halafu usimpe mshahara unategemea aishije??
 
Wilaya ya kerwa na karagwe ndio bado ijajulikana hata hela ya kujikimu wajapewa yote hapo unategemea nn....
 
Hapa ndo huwa najiuliza kazi ya CWT ni nini
kazi yao kuchukua hela tu majukumu hawayajui
 
CWT haipo kwa maslahi ya walim. Someni katiba yake, kujiunga si lazma msiliwe pesa zenu

Kujiunga si lazima ndio, ila ujiunge usijiunge 2% yao wanachukua tu sasa huu si ni u.....!!!
 
Kujiunga si lazima ndio, ila ujiunge usijiunge 2% yao wanachukua tu sasa huu si ni u.....!!!

Tatizo la walim ndo liko hapo,yaani hatuwezi kujisimamia! Kipindi mimi nafanya kazi ya ualimu tulifanyiwa kama hivyo tukaenda Kwa mwajiri wetu mkurugenzi tukiwa na katiba ya cwt mkononi, na tukamwandikia mkurugenzi kuwa tutamshitaki kwa sababu ameidhinisha makato ya mshahara bila ridhaa yetu.katiba ya cwt inaonesha ili uwe mwanachama ni lazima ufanye application na ujaze fomu,ndani ya zile formu una sign mwenyewe kuwa ukatwe hizo asilimia.pia katiba inaeleza kuwa kama hulipi michango ya uanachama basi unakuwa umepoteza sifa.kwa hyo mkurugenzi alituelewa na akasitisha makato na akataka tumalizane na cwt kwa wale wanaotaka. Nimefanya kazi ya ualim miaka 3 na pesa yangu cwt hawakuila hata senti moja.HEBU JISIMAMIENI!watu wananenepa kwa pesa zenu
 
sasa kijana hapo kwenye kusema eti degree wamepata wote unajichanganya na hujui unachoandika, inaonekana una lako jambo,wewe sema mshahara walimu wapya hawajapata acha kuleta longolongo za wenye degree eti wamepata.nakuonaga sana mara nyingi unakashifu wenye degree NAKUAHIDI USIPOACHA HIZI BANGI ZAKO NTAKUSHUGHULIKIA.
 

Una makengeza ya macho na ubongo! kuna sehemu nimesema 'degree wote'? na ni wapi nimekashifu watu wa degree? aisee ungejua nina hasira ya kukosa mshahara usingenitibua...halafu kwa taarifa yako nina uhakika na nilichokiandika kuwa asilimia kubwa ya wenye degree wamepata mshahara...
 
hapa halmashauri ya manyoni waliopata mshahara kwa walimu wa ajira mpya ni 2 kwa idara ya msingi na 35 kwa idara ya sekondari. Degree si kgezo cha kupata mshahara, tumeenda hadi kwa mkurugenzi hakwepo tukaonana na afisa utumishi wilaya majibu aliyotupa tusubir wa mwezi huu wa tano then tuandke barua ya madai ya mshahara wa mwezi wa nne. Yan tayari tushaingizwa kwenye madeni ya walimu!!
 

Yaani kuanza kazi na madai!! Mungu anisaidie but i real hate this government
 
Mi hawajala hata mia siku wakinikata nitaandamana make mi sio mwanachama, na sitaki kusikia habari za CWT
 
Ni suala tu la kukaa chini na shemeji yao JK wakayamaliza...Na salma asisahau nduguze kwa kuwa katoka, akumbuke nyuma alaa!
 
Edited but point noted.
 

Ili upate mshahara yakupasa kuripoti kazini si zaidi ya tarehe 15 ya mwezi husika na ujaze forms mbalimbali zinazohusu mambo ya utumishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…