Walimu wasio na Ajira (NETO) waishauri Serikali isitishe uzalishaji wa Walimu Vyuoni

Walimu wasio na Ajira (NETO) waishauri Serikali isitishe uzalishaji wa Walimu Vyuoni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Daniel Edigar Mkinga, Katibu NETO

"Viongozi wetu wa Serikali, kutokana na uhalisia wa wahitimu na changamoto zinazoonekana katika zoezi la usaili kwa kada ya ualimu, tunapendekeza yafuatayo yafanyiwe kazi.

"Pendekezo la kwanza, kusitisha usaili mara moja kwa kada ya ualimu na kutumia utaratibu wa awali Pendekezo la pili, vyuo vimalize hatua zote za kumthibitisha mwalimu na siyo kuthibitishwa baada ya kukaa muda mrefu mtaani. Pendekezo la tatu, kusitisha uzalishaji wa walimu vyuoni hadi waliopo mtaani wapate Ajira"

Soma: Walimu Wasio na Ajira (NETO) wanaongea na waandishi wa habari kuondoa dukuduku lao
 
kusoma kozi ya kijinga kama uwalimu na kukosa ajira ni fedheha

bora mtu kama petroleum engineer, telecom na engineer zingine mtu akikaa mtaani hata miaka 10 akij kupata ajira tu tayari umaskini bye bye
.
sasa mwalimu kamshara kenyewe 600k unaajiriwa maporini huko maisha yako yote ni wewe chaki na vichaka had unazeeka
 
Hio haiwezekani. Hapo mtabanana umo umo. La msingi ni kufikiria na kushauriana kabla ya kusoma kozi. Ualimu ulikua uhakika zamani ila saizi hapana. Imekua kazi zake ni bahati
Hata kama, je kwanini serikali haikuwa na projection ya mahitaji ya walimu? Yaani kufika 2014 hakutakuwa na uhitaji wa walimu Tena na ikawekwa wazima let say from early 2000s watu wakajua kweli hakuna ajira za ualimu(mahitaji ya walimu by that time). Sasa hii ya kushtukizana mbona inadhihirisha kuwa tunaongozwa na wajingaa
 
Ni Kozi gani inayozalishwa Vyuoni ambayo inatoa ujira zenye ujira wa uhakika ?

Badala ya kuwaambia watunga Sera waje na Sera za kuchukua watu kitaa au kuhakikisha kila mtu ana ujira mnakuja na ushauri wa kuacha kuzalisha nguvu kazi ?

Kwanini tusiache kwanza hata kukusanya Kodi ukizingatia hakuna value for money kwa pesa inayokusanywa

Daniel Edigar Mkinga, Katibu NETO

"Viongozi wetu wa Serikali, kutokana na uhalisia wa wahitimu na changamoto zinazoonekana katika zoezi la usaili kwa kada ya ualimu, tunapendekeza yafuatayo yafanyiwe kazi.

"Pendekezo la kwanza, kusitisha usaili mara moja kwa kada ya ualimu na kutumia utaratibu wa awali Pendekezo la pili, vyuo vimalize hatua zote za kumthibitisha mwalimu na siyo kuthibitishwa baada ya kukaa muda mrefu mtaani. Pendekezo la tatu, kusitisha uzalishaji wa walimu vyuoni hadi waliopo mtaani wapate Ajira"

Soma: Walimu Wasio na Ajira (NETO) wanaongea na waandishi wa habari kuondoa dukuduku lao
Kama wataendelea kuzalisha walimu wawape mikopo na Ardhi ili mkikosa ajira ,muanzishe shule,vyuo,ufugaji,kilimo nk.
 
Mimi naona ni ubinafsi unawasumbua vyuo vya ualimu vifugiwe kuku au au wavifanyeje?
 
  • Thanks
Reactions: apk
Hata kama, je kwanini serikali haikuwa na projection ya mahitaji ya walimu? Yaani kufika 2014 hakutakuwa na uhitaji wa walimu Tena na ikawekwa wazima let say from early 2000s watu wakajua kweli hakuna ajira za ualimu(mahitaji ya walimu by that time). Sasa hii ya kushtukizana mbona inadhihirisha kuwa tunaongozwa na wajingaa
Unajua inashindikana kufunga kozi hio kwasababu watu wanaenda wanazeeka wanastaafu na wengine wanabadili fani. Huwezi kusema mm nafunga udahili kwasababu hawa walimu nilio nao wanatosha. Kuna kesho wakiwa ulionao hawapo au kupungua kutokana na mazingira hayo nilio sema, serikali unafikiri itakua katika mazingira gani?
 
  • Thanks
Reactions: apk
Ajira ya uhakika ni kilimo.

Lakini kwenye kilimo pia:
  • Hakuna miundombinu ya Umwagiliaji.
  • Vifaa gharama zake zipo juu,
  • Gharama za Pembejeo ndio zipo juu zaidi hasa mbegu na viua wadudu
  • Masoko hakuna, kuna masoko ya ndani yenye bei za chini
  • Wakulima wengi wanategemea Mvua tu wakati tuna Maziwa na Mito nchi nzima
Serikali itengeneze Mazingira mazuri kwenye Kilimo na Viwanda vijana tufanye kazi za uzalishaji huko. Leo kazi za Viwandani malipo ni elfu4000 kwa saa 12

😭😭😭
 
Daniel Edigar Mkinga, Katibu NETO

"Viongozi wetu wa Serikali, kutokana na uhalisia wa wahitimu na changamoto zinazoonekana katika zoezi la usaili kwa kada ya ualimu, tunapendekeza yafuatayo yafanyiwe kazi.

"Pendekezo la kwanza, kusitisha usaili mara moja kwa kada ya ualimu na kutumia utaratibu wa awali Pendekezo la pili, vyuo vimalize hatua zote za kumthibitisha mwalimu na siyo kuthibitishwa baada ya kukaa muda mrefu mtaani. Pendekezo la tatu, kusitisha uzalishaji wa walimu vyuoni hadi waliopo mtaani wapate Ajira"

Soma: Walimu Wasio na Ajira (NETO) wanaongea na waandishi wa habari kuondoa dukuduku lao
Inashangaza sana kuona walimu tena wanaojiita wasomi kukataa usaili.

Halafu nani aliwaambia wakisha graduate waajiriwe na serikali,kuna mkataba waliandikishana na serikali kuwa itawapa ajira?

Wajitafakari kwa kweli.
 
Kuna mmoja kasema chuo kiliwapa vyeti baada ya kuwatahini kwa hiyo hakuna haja ya usaili, anataka kusema kada zingine vyuo vyao hawana mitihani? Haviaminiwi mbona wanafanyishwa usaili?
 
Kuna mmoja kasema chuo kiliwapa vyeti baada ya kuwatahini kwa hiyo hakuna haja ya usaili, anataka kusema kada zingine vyuo vyao hawana mitihani? Haviaminiwi mbona wanafanyishwa usaili?
Usaili sio njia sahihi ya kupata wataalamu .

Huwa naangalia maswali yanayoulizwa katika interview za written ni maswali ya kijinga Sana ambayo hayapimi weledi au utaalamu na ufanisi alionao MTU .

Ningepata nafasi ya kuishauri hii Serikali, nigeweka utaratibu wa internship na wakawa wanalipwa at least 300K Kwa kila Mwalimu ndani ya mwaka mmoja.
 
Pale kulikua na aina tatu za usaili written, practical na mahojiano zote hizi hazifai mbona mnakomaa na written kwani ndio kilichofanyika pekee
 
Mhh kwani kada ya ualimu ndiyo ina uhaba wa ajira sana. Kiufupi walimu mnaogopa usaili. Hakuna kozi yenye ukiisoma unakuwa na uhakika 100% kwamba punde ukimaliza utaaajiriwa. Haipo kabisa. Zote tunasoma n probability.....usilalamike. sana.
 
Wengi wao wana ufaulu wa chini mno, huku wengine wakiwa wamefeli kabisaa kufikia viwango vinavyoendana na mahitaji ya ufaulu katika kada ya ualimu.

Hawana sifa, vigezo wala viwango vya kuidhinishwa kua walimu. NETO ikiwa intertained ni hatari kwa ustawi na ubora wa elimu na taaluma kwa Taifa letu.

Wenye kukidhi vigezo na viwango tajika waendelee kupewa fursa na nafasi ya kufundisha ili hatimae viwango vya elimu katika taifa letu viendelee kuimarika.

Kwa ambao hawana sifa na viwango vya ufundishaji, ni muhimu wakasaidiwa ili kusudi wakajikite kwenye kilimo, ufugaji au biashara na maeneo mengine ya kisekta yenye ajira za uhakika na za kutosha kama kama sekta hizo.

Kujihusisha kwao na magenge ya khalifu au kushiriki kuanzisha vitendo vya uvunjifu wa amani na uchochezi kutawafanya kuishia pabaya tu.🐒

Mungu Ibariki Tanzania

Pia soma
- Umoja wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) wakubali wito wa Simbachawene lakini wataka kuwepo na Ulinzi kwenye kikao
 
Back
Top Bottom