Wildchild
JF-Expert Member
- Aug 29, 2018
- 19,411
- 21,938
Unaendelea kuleta siasa kwenye mambo ya msingi.Wengi wao wana ufaulu wa chini mno, huku wengine wakiwa wamefeli kabisaa kufikia viwango vinavyoendana na mahitaji ya ufaulu katika kada ya ualimu.
Hawana sifa, vigezo wala viwango vya kuidhinishwa kua walimu. NETO ikiwa intertained ni hatari kwa ustawi na ubora wa elimu na taaluma kwa Taifa letu.
Wenye kukidhi vigezo na viwango tajika waendelee kupewa fursa na nafasi ya kufundisha ili hatimae viwango vya elimu katika taifa letu viendelee kuimarika.
Kwa ambao hawana sifa na viwango vya ufundishaji, ni muhimu wakasaidiwa ili kusudi wakajikite kwenye kilimo, ufugaji au biashara na maeneo mengine ya kisekta yenye ajira za uhakika na za kutosha kama kama sekta hizo.
Kujihusisha kwao na magenge ya khalifu au kushiriki kuanzisha vitendo vya uvunjifu wa amani na uchochezi kutawafanya kuishia pabaya tu.🐒
Mungu Ibariki Tanzania