EricMan
JF-Expert Member
- Oct 5, 2017
- 3,050
- 5,420
"Umoja wa Waalimu Wasio na Ajira (NETO) ulianza na Wanachama (wajumbe) 15 kupitia makundi ya WhatsApp. Tulianzisha NETO kwasababu ya sintofahamu ya ajira iliyopo kwa wahitimu kuanzia mwaka 2015 mpaka 2023."
"Masuala ya usaili kumekuwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikituumiza wasailiwa, changamoto hizi ni kubwa zimefika hatua zina athiri mpaka uchumi wetu moja kwa moja wasailiwa ambao ndio tuna maisha magumu mtaani, hawana ajira wanajitafuta kwa kiwango kidogo sana na kupata lakini wameathiriwa na huu usaili, wametumia gharama kubwa sana kiasi hatua ambayo wengine wameingia madeni."
"Utafutaji wetu wa sisi ambao tumekosa ajira mtaani kwa kweli ni mgumu mno kiasi ambacho kupata 2,000/- kwa siku ya kula imekuwa ngumu. Baadhi ya watu wameenda kwenye usaili wakiwa wamechukua pesa kwa watu, mtu anaendesha pikipiki anaamua kukopa pesa ya kipande kwa bosi wake ili aweze kwenda kufanya usaijili Bahati mbaya hachaguliwi, hicho kitendo kina waumiza wengi. Lakini bado si hivyo tu kuna watu wanabiashara zao ndogo ndogo zimekufa kwasababu changamoto hii wanapoenda kufanya usaili ni mbali inatumika gharama kubwa kwahiyo imeathiri kwa kiwangu kikubwa hasa walala hoi ambao kwa asilimia kubwa hatuna biashara za msingi."
Katibu wa Umoja wa Waalimu Wasio na Ajira (NETO), Daniel Edgar, ameiomba Serikali kutoa ajira kwa wahitimu wa ualimu waliomaliza masomo yao kati ya mwaka 2015 na 2024.
Ameeleza kuwa kundi hilo lina kila sababu ya kuomba ajira, kwani wengi wao bado hawajapata nafasi ya kufanya kazi rasmi.
Aidha, Edgar ameitaka serikali kusimamia upangaji wa mishahara katika taasisi za elimu binafsi. Ameeleza kuwa kwa sasa, kuna tofauti kubwa katika malipo ya waalimu wa taaluma moja kulingana na ngazi tofauti za elimu, jambo ambalo linahitaji uangalizi wa serikali.
Amependekeza kuwa waalimu walipwe mishahara kulingana na kiwango chao cha elimu ili kuhakikisha haki inatendeka.
"Viongozi wetu wa Serikali, kutokana na uhalisia wa wahitimu na changamoto zinazoonekana katika zoezi la usaili kwa kada ya ualimu, tunapendekeza yafuatayo yafanyiwe kazi.
"Pendekezo la kwanza, kusitisha usaili mara moja kwa kada ya ualimu na kutumia utaratibu wa awali Pendekezo la pili, vyuo vimalize hatua zote za kumthibitisha mwalimu na siyo kuthibitishwa baada ya kukaa muda mrefu mtaani. Pendekezo la tatu, kusitisha uzalishaji wa walimu vyuoni hadi waliopo mtaani wapate Ajira"
Walimu wasio na ajira tangu 2015 mpaka sasa wameanzisha umoja wao wakiilalamikia Serikali kwa nini wanakosa ajira ilihali mapato ya Serikali yameongezeka.
Wameenda mbali na kufanya ulinganisho wa ukasanyaji wa mapato wakati wa Kikwete ambapo makusanyo yalikuwa madogo lakini karibu walimu wote waliajiriwa. Lakini kwa Awamu ya Dkt. Samia mapato ni makubwa sana lakini walimu bado ajira yao ni kidogo sana na wengi wao bado wako mitaani. Wanauliza kulikoni?.
Mimi nadhani ni vema Serikali ikawapa jibu la kuwaridhisha na ione namna ya kuongeza ajira kwa sababu shule nyingi zina upungufu wa walimu. Nashauri pia kama itapendeza walimu wote wasio na ajira wachukuliwe wote na kusimamia uchaguzi ujao wa Oktoba, 2025.
Ujumbe wao siyo mzuri kwa Serikali inabidi Serikali ijitafakari.