Nadhani upole na kukosa utayari wa kufuatilia haki zetu ndo unatuponza Tanzania. Wakati walimu wapya wanaenda vituoni, niliona watu wa mifuko ya pensheni tu ndo walituna wawakilishi wao ili kuja kuwaelimisha walimu wapya namna watakavyo nufaika na mfuko husika. Ni lazima kujiunga na mfuko mmojawapo ila ni ihali ya mtu kwenda mfuko fulani. Hawa watu walitoa semina kwa kina. Namna makato yalivyo, wanavyochangia kusomesha mtumishi na mafao mengi mengi. Cha ajabu hao CWT hata monitor hakuwapo kutoa maelezo kwa wageni jinsi chama kinavyoendeshwa, manufaa yake kwa mwanachama na hata changamoto. Ila wako makini kukata ada ambayo hata mkataba wake wala katiba walimu wapya hawaijui na haijulikani ni mikakati ipo ipo ili kuwajuza. Wenzao hao walifafanua hadi changamoto zao. Kimsingi CWT hawafai na ni kirusi cha secta ya ualimu.