Walimu wawakomba walimu wenzao mishahara yao.

Walimu wawakomba walimu wenzao mishahara yao.

Hebu waeleze walimu kazi mbili tu...! zinazofanywa na cwt kwa faida yao. Maana unaweza kuwa unaongea tu ki-mbumbumbu huna chochote unachokijua kuhusu cwt. Waeleze walimu sasa manufaa wanayopata kutokana na cwt...!
Au una chuki binafsi na CCM maana nimeshindwa kuelewa CCM imeingiaje kwenye hii thread.

Mkuu tatizo la wengi ni kuchukia kitu wasichokifahamu. hii inatokana na uvivu wa kufikiri na kusubiri mwingine afikirie ndio wao wafuate. chuki zake na ccm anahusisha na mambo yasiyoingiliana, yaani kila hoja hawezi kuijadili bila kutaja vyama tena ccm ktk mtizamo hasi.
 
Mimi hao viongozi hawanijui vizuri ckuzaliwa kumuogopa mtu bali aliyenipa hii pumzi sasa wajichanganye waingie kumi na nane zangu watajua nidhamu ya uoga nilishaacha tumboni mwa mama yangu,huu co muda wa kuogopana hao wezi akilini mwangu hawaingii sasa subirini.
 
Nadhani upole na kukosa utayari wa kufuatilia haki zetu ndo unatuponza Tanzania. Wakati walimu wapya wanaenda vituoni, niliona watu wa mifuko ya pensheni tu ndo walituna wawakilishi wao ili kuja kuwaelimisha walimu wapya namna watakavyo nufaika na mfuko husika. Ni lazima kujiunga na mfuko mmojawapo ila ni ihali ya mtu kwenda mfuko fulani. Hawa watu walitoa semina kwa kina. Namna makato yalivyo, wanavyochangia kusomesha mtumishi na mafao mengi mengi. Cha ajabu hao CWT hata monitor hakuwapo kutoa maelezo kwa wageni jinsi chama kinavyoendeshwa, manufaa yake kwa mwanachama na hata changamoto. Ila wako makini kukata ada ambayo hata mkataba wake wala katiba walimu wapya hawaijui na haijulikani ni mikakati ipo ipo ili kuwajuza. Wenzao hao walifafanua hadi changamoto zao. Kimsingi CWT hawafai na ni kirusi cha secta ya ualimu.
 
Hivi wana uhalali gani wa kukata pesa ya mtu bila kuingia nae mkataba nakumbuka kipindi cha mgomo serikali ilisema c walimu wote ni wanachama wa cwt sasa wanakataje pesa toka kwa walimu wote je, pesa hiyo yote wanafanyia nini?
 
Back
Top Bottom