Walimu zaidi ya 10000 kukosa ajira

Mimi niliajiriwa 2008 na 2011 nikaacha kazi. Mshahara ukafutwa na pia nikaomba kituo kipya. Itakuaje wadau
 
Hits: 497
SERIKALI imesema ajira za walimu wapya
zitaanza rasmi Mei Mosi, mwaka huu huku
ikiweka wazi kuwa walimu hao wasitegemee
kupangiwa katika maeneo ya majiji,
manispaa na miji.
Walimu hao wametakiwa kutotegemea
kupangiwa katika maeneo hayo kutokana na
idadi ya walimu waliopo ni kubwa na inakidhi
mahitaji, huku maeneo yaliyopewa
kipaumbele ni vijijini na halmashauri ambazo
zina mahitaji na upungufu mkubwa wa
walimu.
Idadi ya walimu wapya watakaoanza ajira
zao mwezi ujao ni 31,056 ambapo kwa
walimu wa ngazi ya Cheti ni 11,795,
Stashahada (Diploma) 6,596 na wenye
Shahada (Degree) 12,665.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
ajira mpya za walimu kwa mwaka
2014/2015.
Alisema kwa mwaka huu ajira hizo
zimechelewa kutokana na TAMISEMI pamoja
na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
kufanya ufuatiliaji wa kina hadi katika ngazi
ya shule ili kubaini kwa uhakika mahitaji
halisi ya walimu kwa kila halmahauri na
shule.
“Ufuatiliaji huo umebaini kuwepo kwa
halmashauri na shule hasa za mjini zenye
walimu wa ziada na zingine hasa za vijijini
zina upungufu mkubwa wa walimu,” alisema
Sagini.
Alisema taarifa hizo zimesaidia kuwapanga
walimu wapya kwa usawa ili kuondoa
uwiano usioridhisha kwenye maeneo mengi
ya vijijini. Alisema kwa sasa wanakamilisha
taratibu za kupata kibali kwa ajili ya ajira za
walimu na fedha za kuwalipa stahili zao ili
waanze ajira zao rasmi mwezi ujao.
Aidha, alisema orodha ya walimu na vituo
watakavyopangiwa vitawekwa katika tovuti
ya Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ambayo
ni www.pmoralg.com na ya Wizara ya Elimu
www.moe. go.tz ifikapo Aprili 24, mwaka
huu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa
TAMISEMI, Zuberi Samataba alisema, pia
ufuatiliaji huo ulikuwa ni kuhakikisha
wanakuwa na taarifa sahihi za walimu
wanaoajiri wote ni wapya ambao hawajawahi
kuajiriwa ili kuepuka usumbufu kwa walimu
ambao hawatoi taarifa.
Alisema baadhi ya w
 
Mimi naona wengi au wote watapata. Kwa sababu mwakajana wale wa cheti walikuwa elfu 17 lakini mwaka huu wapo 11 (yawezekana ndiyo idadi ya waliohotimu)
Kwa wale wa diploma mwaka jana walikuwa elfu 5 ila mwaka huu ni elfu 6
Na wa degree mwakajana walikuwa elfu 12 na mwaka huu ni elfu 12 as well. Hapa ukitoa na wale waliokuwa wanajiendeleza ambao wanaweza kuwa elfu moja na zaidi wanaobaki wote ni ajira mpya nadhani wengi watapata kama sio wote
 

bora nizibe pua maana naweza kuangamia na hii hewa chafu kulikoni
 

Mawazo mazuri sana unafikiri kwa busara hongera keep it up.
 
Mawazo mazuri sana unafikiri kwa busara hongera keep it up.

Kwa kuongezea wale wa cheti wamepungua kutokana na kigezo cha kuondoa dv IV.28 pts na kuchukua 27+pts, so hao watu 6000+ wamepungua hivyo kufidiwa ktk ngaz zngne (dipo & b.i.e)
 
Mimi niliajiriwa 2008 na 2011 nikaacha kazi. Mshahara ukafutwa na pia nikaomba kituo kipya. Itakuaje wadau

Ulkua na malengo gani kuacha kazi ile hali hujaandaa kikamilifu kazi ambayo ultqka kuifanya baada ya kuacha ualimu??

''Acha kazi uone jinsi ilivo kazi kupata kazi''

Mungu akusaidie upate tena!!
 
Ulkua na malengo gani kuacha kazi ile hali hujaandaa kikamilifu kazi ambayo ultqka kuifanya baada ya kuacha ualimu??

''Acha kazi uone jinsi ilivo kazi kupata kazi''

Mungu akusaidie upate tena!!

Private unapaweza? njoo private me nawakimbia trh 1 May
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…