DOKEZO Walinzi wa getini Msamvu Bus Terminal wanalazimisha kulipa Sh 300 hata kama una tiketi ya mtandaoni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ukilipitia tiketi online, automatically utabakiwa na muamala wa malipo, unapofika stendi uendako kama huna risiti utatakiwa ulipie shilingi mia tatu getini.

Kwani kulipia ticket online na kulipia ofisini kuna tofauti gani? Ukionesha SMS ya malipo hawataki, wanataka risiti ya tiketi ya EFD.

Unapolipia ticket online unakatwa na ukifika geti la stendi wanatoza tena mia tatu. Mfano, nilikata ticket online Arusha kwenda Morogoro, nimeshuka Msamvu Stendi, nataka kutoka wanadai ticket naonesha SMS ya malipo kuwa nimetoka Arusha hawataki, ilibidi nilipie mia tatu ili niweze kutoka getini.

Je, Serikali haitambui malipo ya ticket kwa njia ya Mtandao? Kwanini ukilipia ticket karatasi hawana shida? Au hawaamini mifumo yao?
 
Palikuwa pa kupata umaarufu hapo nashangaa umelipa kijinga
 
boraa huko 300, magufuli terminal hapa kutokana na uhaba wa chenji bei imekua 500 au 1000 kutokna na upatikanaji wa chenji
 
Je, Serikali haitambui malipo ya ticket kwa njia ya Mtandao? Kwanini ukilipia ticket karatasi hawana shida? Au hawaamini mifumo yao?
Wewe umewalegezea halafu hukutaka tu kuishi nao vizuri 300 kwa ina ukubwa gani mzee ndio hela yake ya chai hio malipo ya posho kwa mwezi laki 20 sasa unategemea akale wapi zaidi ya kukaba abiria wasiokua na tiketi za makaratasi?
 
boraa huko 300, magufuli terminal hapa kutokana na uhaba wa chenji bei imekua 500 au 1000 kutokna na upatikanaji wa chenji
Kutoka baada ya kufika na bus hakuna mtu ana habari na wewe hulipi hata 100
 
Wewe umewalegezea halafu hukutaka tu kuishi nao vizuri 300 kwa ina ukubwa gani mzee ndio hela yake ya chai hio malipo ya posho kwa mwezi laki 20 sasa unategemea akale wapi zaidi ya kukaba abiria wasiokua na tiketi za makaratasi?
Kwanini unampa abiria wajibu wa kulisha watu wa stendi asiowafahamu?? Hakuna kazi nyingine hao wanaokusanya hizo 300 wanaweza kufanya zaidi ya kulazimisha kupewa pesa za watu?
Halafu kwanza ishu sio 300, hata ingekuwa 100 bado watu wana wajibu wa kuhoji upuuzi.
 
magufuli tunalipa muda wa kuingia --- hapo msamvu kuna siku mtu alikuja kunipokea wakati tunatoka mimi nilioneha tiketi na yeye alionesha tiketi waliompa alivyoingia stendi. hii iliokua miaka kadhaa nyuma.

labda wenyeji watusaidie hali ipo vipi
 
Kwanini unampa abiria wajibu wa kulisha watu wa stendi asiowafahamu?? Hakuna kazi nyingine hao wanaokusanya hizo 300 wanaweza kufanya zaidi ya kulazimisha kupewa pesa za watu?
Halafu kwanza ishu sio 300, hata ingekuwa 100 bado watu wana wajibu wa kuhoji upuuzi.
Waelezee vizuri wahusika wanaowasimamia hao walinzi mimi nimeelezea uhalisia tu
 
Hakuna uhalisia kulegezea kila mtu anayetaka kuchukua pesa za watu wengine kiholela tu na kuleta usumbufu kwa kigezo cha kwamba "atakula wapi" asipochukua hizo pesa.
 
Ndio nikasema hivi kosa sio la huyo mlinzi kosa ni waliomuweka huyo mlinzi, unanielewa sijui vizuri hapo watafutwe wahusika watoe maelezo imekuaje mlinzi huyo anafanya hivyo, ushaelewa hapo Magufuli kuingia uwe na ticket au huna ticket lazima ulipie card ya kuingia sio bure unalipa una ticket huna ticket unalipa ndio unapewa card uingie, kutoka hulipi ni bure, sasa hapo watafutwe wahusika watoe maelezo, uwe unaelewa mimi sio muhusika wa hio stendi kwa hio usinibananishe as if mimi ndio muhusika mkuu wa stendi ya Msamvu Morogoro
 
Wewe umewalegezea halafu hukutaka tu kuishi nao vizuri 300 kwa ina ukubwa gani mzee ndio hela yake ya chai hio malipo ya posho kwa mwezi laki 20 sasa unategemea akale wapi zaidi ya kukaba abiria wasiokua na tiketi za makaratasi?
Tatizo sio pesa ila ni usumbufu wa kishenzi, kama ni shida ya fedha si angeomba kiungwana tu
 
Upo sahihi kabisa mkuu, ila hapo wa kuhojiwa ni Muhusika Mkuu alieweka hao Walinzi atoe maelezo yaliyoshiba kwanini hao walinzi wanafanya hivyo, nilichoeleza mimi ni assumption tu sina maana kwamba ndio ipo hivyo, unielewe hapo mkuu
 
Stendi karibia zote nahisi, hata NYEGEZI mwanza
Sasa sijui ndo utaratibu🙌
 
Back
Top Bottom