Ing'ang'a
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,866
- 1,282
Huwezi kuamini. Suma jkt guard kuna vijana wasomi wazuri tu.
Suma ya miezi hii sio ile Suma ya wakati wanaanza kuchukua tenda za malindo ya kwenye taasisi. Wale wa mwanzo walikua ni wakali sana halafu uelewa wa mambo ulikua ni mdogo sana.
Vijana wenzangu wa Suma JKT guard msikate tamaa ya maisha. Wote hamuwezi kuwa polisi, magereza au JW. Tumieni kipato kidogo mnachopata kujiendeleza kwa fani mbalimbali za stadi za maisha lakini kupata mitaji.
Wengi wenu bado ni vijana wadogo. Nawasihi muache umalaya sio mzuri, kuna ukimwi na homa ya ini. Kuweni makini sana vinginevyo mtakwisha.
Umenena vyema sana Mkuu. Madogo wakipita hapa watapata kitu.