Walinzi wa kampuni ya SUMA JKT GUARD wana matatizo ya kisaikolojia

Walinzi wa kampuni ya SUMA JKT GUARD wana matatizo ya kisaikolojia

Mleta Mada uko sahihi sana,
Mwaka 2016 pale mikocheni kwa Warioba ile njia inapandisha inakuja hadi NACTE nilikuwa nashida na ofisi ya Serikali ya mtaa wa TPDC nikaenda mtaa mwingine pale mikocheni Sekondari nikaelekezwa uchochoro wa kupita kwenda TPDC nikakatisha hapo kwenye ofisi sijui za kituo cha elimu kwa watu Wazima (nyumba zao zimejengwa kwa Mbao) karibia na ofisi za Under the same Sun kwa nyuma hamna fensi mara najikuta natokea mbele kuna geti ndo nawakuta hawa Vijana wakaniuliza natokea wapi na naelekea wapi nikawajibu vizuri na kuna Document nilikuwa nazo nikawaonyesha lakini wakanishikilia niendelee kubaki hapo kuanzia saa 6 mchana hadi saa 11 jioni ikabidi nipige simu polisi makao makuu wakaja na gari Askari 5 wakawauliza nini shida wakajibu eti nimekatiza kwenye lindo lao labda nachunguza ili niibe, wakaulizwa mbona mmemshikilia masaa mengi sana bila kuripoti polisi wakakosa cha kujibu, polisi wakaniachia niende na kuwapa onyo hao jamaa
Ukweli siku hiyo nilikasirika sana kesho yake nilitaka niende makao makuu yao nikaonane na wahusika bahati nzuri Roho wa bwana alinijia na kusema samehe 7x70.
Kwahiyo mleta mada uko sahihi kabisa vijana wale wana matatizo ya kisaikolojia inabidi wahurumiwe wanafanya kazi masaa mengi sana halafu malipo kiduchu.!
Dunia ya sasa si ya kusema usamehe.
 
Hakika wewe utakuwa ni mzazi. Umeandika maneno yenye hekima sana mkuu.

Watu wanawacheka vijana wa SUMA badala ya kuwatia moyo.

Kwani kuna vijana wangapi tumemaliza nao form four na wameshindwa kwenda five na six?

Suala la kuwa na madaraja katika jamii ni kawaida sana mbona hata Ulaya ipo?

Komaeni vijana wenzangu wote muwe SUMA JKT, MGAMBO au hata raia wa kawaida unayepambana kujikomboa kiuchumi, Mungu atawafungulia milango ya baraka.
Hakika mkuu.
 
Hakika wewe utakuwa ni mzazi. Umeandika maneno yenye hekima sana mkuu.

Watu wanawacheka vijana wa SUMA badala ya kuwatia moyo.

Kwani kuna vijana wangapi tumemaliza nao form four na wameshindwa kwenda five na six?

Suala la kuwa na madaraja katika jamii ni kawaida sana mbona hata Ulaya ipo?

Komaeni vijana wenzangu wote muwe SUMA JKT, MGAMBO au hata raia wa kawaida unayepambana kujikomboa kiuchumi, Mungu atawafungulia milango ya baraka.
Kwani wao ndio wenye stress tu peke Yao ?

Wajinga tu hao
 
Ila kusema kweli hawa jamaa hawako vizuri kisaikolojia kabisa, Nikiwa TIBA_UDOM ndio wanaletwa kwa mara ya kwanza et ikifika sa5 wanakuja Kwwnye madarasa wansema muda umeisha turudi Hostel, aseeh Mbaya zaidi et Mwanafunzi katoka usiku huko alipokuwa anazuiliwa asiingie hostel!!!
 
Habari!

Ukichukua matukio machache yaliyofanywa na hawa vijana wa SUMA JKT GUARD utagundua kuna kitu hakiko sawa. Kuna upepo umepunguza akili zao.

Majuzi jangwani walimpiga yule jamaa wa African sports na kupelekea kifo chake, tena tunapokea taarifa kuwa wamemuua mwananchi asiye na hatia aliyekuwa akilima shambani kwake karibu na msitu wanaoulinda.

Juzi jioni wakati natoka kazini narudi nyumbani njiani nikakutana na kijana wa suma kabeba Kirungu, manati, pingu na vikorokoro vingine anatembea akiekekea lindoni. Jinsi alivyojifanyia camouflage utadhani yupo vitani kumbe anakwenda kulinda kaeneo kadogo tu.

Wale vijana wa SUMA wengi wao ni vijana wa JKT waliomaliza mikataba yao na kurudi nyumbani bila mitaji. Marafiki zao wengi ni vijana waliokuwa nao JKT ambao sasa ni watumishi wa JWTZ, TISS, ZIMAMOTO , UHAMIAJI, MAGEREZA na POLISI.

Wenzao wanakopa wanajenga, wananunua magari na kusaidia ndugu huku wao vijana wa SUMA wakilipwa kitapeli na kampuni yao ya ulinzi. Take home yao haifiki hata 250k, hawakopesheki benki, ajira yao kufukuzwa ni rahisi, hawana uhakika wa maisha ya uzeeni.
Muda wa kazi ni mwingi.

Hawa vijana wa SUMA wasaidiwe .

Ni vijana waliokosa dira , sasa wamebaki kujitutumua tu ili nao wahesabike kama wanajeshi.

Unajua JKT mtiti wake ni mzito sana, miezi 6 unakula kozi ngumu huku ukiendelea kulima kwa bidii, then umemaliza unaendelea kulimishwa zaidi kila siku. Unavumilia ukijua utafanikiwa mwisho wa siku unapewa nauli tu urudi kwenu, lazima uchanganyikiwe.

Hakuna anayekwenda JKT eti akajitolee tu kisha arudi nyumbani. Basi serikali itoe mitaji kwa vijana wanaotoka JKT bila ajiraya uhakika ili wakaendeleze fani walizojifunza huko makambini. Wa kufuga samaki au kuku akafuge, wa kujenga akajenge n.k
Usiombe uwakute wale wanaopangwa kulinda ATMs, wanapiga mizinga hatari
 
... kuna kamoja wiki iliyopita nilikashuhudia mahali kanataka kuingia kwenye public transport bila kulipa nauli kama kaka zao JW na Polisi kisa kamevaa magwanda ya SUMA! Kalisukumizwa kakadondoka kuleee! Huhitaji kumtamzama mara mbili kujua ni victim wa psychological problems.

mkuu nadhani hii ilitokea kituo cha shekilango cha UDART mana pale walikuwa wawili sasa walitaka kupita kibabe bila kulipa nauli kumbe nao wale walinzi wa mwendokasi wamevaa kiraia lakina nadhani nao ni wanajeshi wale mana walianza kuwapiga mitama mpaka raia wakaja kuingilia kati ili waachiwe huru

sas ndio mmoja wa wale walinzi wakawa wanawapa habari raia kuwa hawa wanataka kupita bure tena kwa mabavu kama hawana hela wangeniomba kiustaarabu ili niwaruhusu wapite ila hawakufanikiwa kupita wakaenda zao

naunga mkono hoja kuwa hawa watu hawapo sawa kiakili mana pia wanapenda kutumi nguvu sana hata kwa wanafunzi wa vyuoni
 
Hawa hawa ndio watakuja kuleta mpasuko tu katka taifa, ni suala la muda.....


Yaani kuna uhuni hicho kikampuni cha ulinzi n kivuli cha watu fulani...

Kila kichwa kinaandikiwa kinalipwa kilo 5 halafu kinakuja kupewa kilo unusu.....

Wafikirieni kuwa nao n watu
 
... ni kakitengo fulani ka uzalishaji mmiliki akiwa JKT; mishahara yao inatokana na wanachozalisha - ulinzi, matofali, kokoto, maji ya Uhuru, n.k.
Duuu unaongea ukweli mtupu pia mtoa mada amesahau kuwa wengine wapewa ajira na taasisi nzuri km Tanapa,Tawa na Ncaa halafu wao wapo kiKK guard lazima stress

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Hahahaaa ngoja nikubali tu mkuu. Kwa vyovyote itakuwa umeshakutana nao kwenye kona ngumu.
Waliwahi niweka mtu kati kuanzia sa8 usiku Hadi sa3 asubuhi!! Utawala wa College of Education kisa chenyewe hakina kichwa Wala miguu, Mbaya zaidi mmoja wao akanipa namba yake aseeeh, Nilimtukana sijawahi tukana Wala kudharau kazi ya mtu Kama nilivyofanya kwa huyo, SUMAJKT
 
realy wana shida af na ao wanajiona ni wanajeshi kam wa jkt ilingalii ni coz ya miezi sita ndo inawafanya wanasumbua ila watawasumbua wasio wajua kwetu wata ungua na jua
 
Inawezekana ni kweli hawako sawa nakumbuka tukio moja

Kuna mmoja alipanda daladala kadaiwa nauli akavimba anataka kupigana na konda kwakua nilikua seat ya karibu na mlango nikashuka fasta kuachanisha, ikabd nimlipie nauli kwakua ni bei che tu nkashangaa ananibadilikia na mm ananiambia braza sijakuomba unilipie nauli na usiingilie ugomvi usio kuhusu..

ilibid nimpige biti ya hatar maana alikua hana ubavu wa kusukuma ngumi hata 3 mbele yangu
 
Back
Top Bottom