Walinzi wa kampuni ya SUMA JKT GUARD wana matatizo ya kisaikolojia

Walinzi wa kampuni ya SUMA JKT GUARD wana matatizo ya kisaikolojia

SITOSAHAU JKT MKATABA ULIVYOISHA NA TUKALUDISHWA NYUMBANI-- "OP MAGUFULI"

ilikuwa ni mwaka 2016 naelekea kikosi cha mafunzo ya jkt kwenye gali unapiga mwimbo wa darasa -muziki... kozi ikaanza na hatimaye ikamalizika miezi 6 baadaye nkawa service man kikosi furani nyanda za kaskazini kuishi kwa taabu na mawazo ya lini ntapata ajira nkijitazama sina kitu chochote wala home sikuacha chochote ata kuku m1 wa kienyeji....

Miaka mitatu inakata tunasikia tetesi za tarehe furani tunaludi home wenzangu wakawa wanatoloka wanaludi makwao kupambana na vitu.vingine kabla kipenga rasmi hakijaliaa mimi npo nacheki mambo mpaka tone la mwisho hatimaye tukaambiwa tukusanye kila mali ya jeshi haraka iwezekanavyo hapa ni kombati,sahani,kikombe ,kofia na mkanda kama unao

Wasichana wakaanza kulia vilio c vya nchi hiii wanaenda wapi kukaa warudi tena home kukaa wengi hawakurudi mimi nkasema narudi kupambana kitaani kwetu na ntakaa home mpaka nipate mtaji hapa ndo MOVIE inapoanzaa.
 
Habari!

Ukichukua matukio machache yaliyofanywa na hawa vijana wa SUMA JKT GUARD utagundua kuna kitu hakiko sawa. Kuna upepo umepunguza akili zao.

Majuzi jangwani walimpiga yule jamaa wa African sports na kupelekea kifo chake, tena tunapokea taarifa kuwa wamemuua mwananchi asiye na hatia aliyekuwa akilima shambani kwake karibu na msitu wanaoulinda.

Juzi jioni wakati natoka kazini narudi nyumbani njiani nikakutana na kijana wa suma kabeba Kirungu, manati, pingu na vikorokoro vingine anatembea akiekekea lindoni. Jinsi alivyojifanyia camouflage utadhani yupo vitani kumbe anakwenda kulinda kaeneo kadogo tu.

Wale vijana wa SUMA wengi wao ni vijana wa JKT waliomaliza mikataba yao na kurudi nyumbani bila mitaji.
Marafiki zao wengi ni vijana waliokuwa nao JKT ambao sasa ni watumishi wa JWTZ, TISS, ZIMAMOTO , UHAMIAJI, MAGEREZA na POLISI.

Wenzao wanakopa wanajenga, wananunua magari na kusaidia ndugu huku wao vijana wa SUMA wakilipwa kitapeli na kampuni yao ya ulinzi. Take home yao haifiki hata 250k, hawakopesheki benki, ajira yao kufukuzwa ni rahisi, hawana uhakika wa maisha ya uzeeni.
Muda wa kazi ni mwingi.

Hawa vijana wa SUMA wasaidiwe .

Ni vijana waliokosa dira , sasa wamebaki kujitutumua tu ili nao wahesabike kama wanajeshi.

Unajua JKT mtiti wake ni mzito sana, miezi 6 unakula kozi ngumu huku ukiendelea kulima kwa bidii, then umemaliza unaendelea kulimishwa zaidi kila siku. Unavumilia ukijua utafanikiwa mwisho wa siku unapewa nauli tu urudi kwenu, lazima uchanganyikiwe.

Hakuna anayekwenda JKT eti akajitolee tu kisha arudi nyumbani.
Basi serikali itoe mitaji kwa vijana wanaotoka JKT bila ajiraya uhakika ili wakaendeleze fani walizojifunza huko makambini. Wa kufuga samaki au kuku akafuge, wa kujenga akajenge n.k
huyo jamaa aliyeuliwa jangwani karibu na msitu ni jangwani ya Dar au wapi?

Hawa jamaa wamegeuka SARS ya nigeria
 
Mleta Mada uko sahihi sana,
Mwaka 2016 pale mikocheni kwa Warioba ile njia inapandisha inakuja hadi NACTE nilikuwa nashida na ofisi ya Serikali ya mtaa wa TPDC nikaenda mtaa mwingine pale mikocheni Sekondari nikaelekezwa uchochoro wa kupita kwenda TPDC nikakatisha hapo kwenye ofisi sijui za kituo cha elimu kwa watu Wazima (nyumba zao zimejengwa kwa Mbao) karibia na ofisi za Under the same Sun kwa nyuma hamna fensi mara najikuta natokea mbele kuna geti ndo nawakuta hawa Vijana wakaniuliza natokea wapi na naelekea wapi nikawajibu vizuri na kuna Document nilikuwa nazo nikawaonyesha lakini wakanishikilia niendelee kubaki hapo kuanzia saa 6 mchana hadi saa 11 jioni ikabidi nipige simu polisi makao makuu wakaja na gari Askari 5 wakawauliza nini shida wakajibu eti nimekatiza kwenye lindo lao labda nachunguza ili niibe, wakaulizwa mbona mmemshikilia masaa mengi sana bila kuripoti polisi wakakosa cha kujibu, polisi wakaniachia niende na kuwapa onyo hao jamaa
Ukweli siku hiyo nilikasirika sana kesho yake nilitaka niende makao makuu yao nikaonane na wahusika bahati nzuri Roho wa bwana alinijia na kusema samehe 7x70.
Kwahiyo mleta mada uko sahihi kabisa vijana wale wana matatizo ya kisaikolojia inabidi wahurumiwe wanafanya kazi masaa mengi sana halafu malipo kiduchu.!
Halafu nilichogundua waajiri wengi wa Makampuni ya Ulinzi wanawanyanyasa sana wafanyakazi wao kwa kigezo kuwa wao ni askari wanatakiwa kupokea amri tu hata kugoma hawaruhusiwi wanachukuwa advantages hiyo.!
 
Sasa kama una shule kidogo why usiende GardaWorld, Warrior, G4S au SGA ?

Suma JKT + Maaskari wote Polisu, JWTZ, magereza, Tanzania ni matokeo ya kushindwa kwa CCM.

Tena hao vijana wa kujitolea huko JKT wengi wamekuwa matapeli.

Wana mishahara kiduchuu sana na kwa CCM inawatumia sana miserably imeamua kuwaacha wawe juu ya sheria (Huo ndio mshahara wao).

Suma JKT wanalipwa Tsh 170,000 imagine!

Mtu anakaa JKT miaka 2 unapugwa na kulima bamia kwa ujira wa Tsh 25,000 mtaani wanajua umekuwa askari, halafu unarudi home, kimbilio Suma mshahara Tsh 170,000

Sasa si ni bora ungeenda makampuni ya ulinzi yanayolipa Tsh 250,000 ndani ya miaka 2 ungekuwa ushapiga hatua
... hivi kima cha chini nchi hii kwa ajira rasmi kama hizo za SUMA ni sh. ngapi? How comes SUMA, kampuni ya serikali, wanalipa chini ya kima cha chini? Ajabu sana hii kitu!
 
nilifikaa nyumbani nmetoka jkt mama alilia kilio sitokisahau baba alichoniambiaa pambana..
baada ya mwezi m1 kukaa home kuna jamaa alikuwa anafanya bustani ya kuotesha miche ya matunda ya maembe, parachichi(ovakado) na mapapai pembeni kidogo ya home miche mizuri c poaa hafu akawa anauza mia miaa kila mchee nlkuja kupata gepu la jamaa wa nyamongo mgodini (TEGESHA-watu wa tarime wataelewa hapa namanisha nini) anahitaji michee 2000 ya maembee tu hafu alikuwa anapesa nkamwambia mchee m1 ni sh 1000 kwa sababu ni ya kisasa hata akubishaa wala akuomba punguzo...chapu akatoaa milioni 2 mwenye miche shambani nkampa laki 2 tu tukaachanaa naye nkasepa home na 1800000 kidogo nkaanzaa kuwa na nguvu ya kukaa hata na vijana wenzangu mtaani
nkanunua pikipiki ,pikipiki ikanpa chainsaw ikanibidi niaanzishe sehemu ya kuuzaa mbao.. nkajenga kijijini kwetu nyumba ya kawaida bado napambanaa pia..FUNZO KUBWA NILILOPATA NIKIWA JKT

kujiamini---->SIMWOGOPI MTU NA SINA MCHEZO NA MAISHA YANGU
 
Kiukweli wafanyakazi wa sekta ya ulinzi hapa tz maslahi yao ni duni sana..na huku wakifanya kazi masaa mengi kwa siku.. imagine kampuni hizo za wageni mf. Sga n.k.. basic salary ni 150,000 ... Ukipambana na overtime unakutana na 250,000 mwisho wa mwezi.. kwa kampuni za wazawa huko ndio balaa....

Sijajua serikali ina mpango gani na hii sekta.. maana unakuta mlinzi analinda mali ya mamilioni ila mshahara kiduchu wakati ana familia na kuishi nyumba ya kupanga.. Mtu wa hivyo ni lazima awe na msongo wa mawazo ama ashawishike kuiba.... Mungu asaidie sana..
 
Mleta Mada uko sahihi sana,
Mwaka 2016 pale mikocheni kwa Warioba ile njia inapandisha inakuja hadi NACTE nilikuwa nashida na ofisi ya Serikali ya mtaa wa TPDC nikaenda mtaa mwingine pale mikocheni Sekondari nikaelekezwa uchochoro wa kupita kwenda TPDC nikakatisha hapo kwenye ofisi sijui za kituo cha elimu kwa watu Wazima (nyumba zao zimejengwa kwa Mbao) karibia na ofisi za Under the same Sun kwa nyuma hamna fensi mara najikuta natokea mbele kuna geti ndo nawakuta hawa Vijana wakaniuliza natokea wapi na naelekea wapi nikawajibu vizuri na kuna Document nilikuwa nazo nikawaonyesha lakini wakanishikilia niendelee kubaki hapo kuanzia saa 6 mchana hadi saa 11 jioni ikabidi nipige simu polisi makao makuu wakaja na gari Askari 5 wakawauliza nini shida wakajibu eti nimekatiza kwenye lindo lao labda nachunguza ili niibe, wakaulizwa mbona mmemshikilia masaa mengi sana bila kuripoti polisi wakakosa cha kujibu, polisi wakaniachia niende na kuwapa onyo hao jamaa
Ukweli siku hiyo nilikasirika sana kesho yake nilitaka niende makao makuu yao nikaonane na wahusika bahati nzuri Roho wa bwana alinijia na kusema samehe 7x70.
Kwahiyo mleta mada uko sahihi kabisa vijana wale wana matatizo ya kisaikolojia inabidi wahurumiwe wanafanya kazi masaa mengi sana halafu malipo kiduchu.!
Sa hiv nasikia wanasaini mkataba three years
 
Habari!

Ukichukua matukio machache yaliyofanywa na hawa vijana wa SUMA JKT GUARD utagundua kuna kitu hakiko sawa. Kuna upepo umepunguza akili zao.

Majuzi jangwani walimpiga yule jamaa wa African sports na kupelekea kifo chake, tena tunapokea taarifa kuwa wamemuua mwananchi asiye na hatia aliyekuwa akilima shambani kwake karibu na msitu wanaoulinda.

Juzi jioni wakati natoka kazini narudi nyumbani njiani nikakutana na kijana wa suma kabeba Kirungu, manati, pingu na vikorokoro vingine anatembea akiekekea lindoni. Jinsi alivyojifanyia camouflage utadhani yupo vitani kumbe anakwenda kulinda kaeneo kadogo tu.

Wale vijana wa SUMA wengi wao ni vijana wa JKT waliomaliza mikataba yao na kurudi nyumbani bila mitaji. Marafiki zao wengi ni vijana waliokuwa nao JKT ambao sasa ni watumishi wa JWTZ, TISS, ZIMAMOTO , UHAMIAJI, MAGEREZA na POLISI.

Wenzao wanakopa wanajenga, wananunua magari na kusaidia ndugu huku wao vijana wa SUMA wakilipwa kitapeli na kampuni yao ya ulinzi. Take home yao haifiki hata 250k, hawakopesheki benki, ajira yao kufukuzwa ni rahisi, hawana uhakika wa maisha ya uzeeni.
Muda wa kazi ni mwingi.

Hawa vijana wa SUMA wasaidiwe .

Ni vijana waliokosa dira , sasa wamebaki kujitutumua tu ili nao wahesabike kama wanajeshi.

Unajua JKT mtiti wake ni mzito sana, miezi 6 unakula kozi ngumu huku ukiendelea kulima kwa bidii, then umemaliza unaendelea kulimishwa zaidi kila siku. Unavumilia ukijua utafanikiwa mwisho wa siku unapewa nauli tu urudi kwenu, lazima uchanganyikiwe.

Hakuna anayekwenda JKT eti akajitolee tu kisha arudi nyumbani. Basi serikali itoe mitaji kwa vijana wanaotoka JKT bila ajiraya uhakika ili wakaendeleze fani walizojifunza huko makambini. Wa kufuga samaki au kuku akafuge, wa kujenga

Mmh..Ila mkuu kuiba ni tabia ya mtu haina mahusiano na mshahara kabsa
Sasa mtu alijiunga kwa nia ya kuajiriwa jw alafu anamaliza mkataba anarudi uraiani alafu anakuja kutana na mwenzake ameajiriwa maisha yako safi ukiangalia ni yule yule pengine alikuwa nanga au bumunda anakula mshahara. Hii naona wanaumiaga sana na sio hao tuu kina wwngi tuu hata hawapo huko suma kwa hasira wameamua kukaa tuu bila kazi ya ulinzi tena hao ni wengi kuliko walioko suma.hivi unakumbuka kipindi aliewahi kuwa mkuu wa mkoa (makonda)alipowaita afosini kwake pale ilala walivyojaa hadi yeye makonda mwenyewe alishangaa
 
... hivi kima cha chini nchi hii kwa ajira rasmi kama hizo za SUMA ni sh. ngapi? How comes SUMA, kampuni ya serikali, wanalipa chini ya kima cha chini? Ajabu sana hii kitu!
Lile ni shirika, mishahara hupangwa na bodi
 
nilifikaa nyumbani nmetoka jkt mama alilia kilio sitokisahau baba alichoniambiaa pambana..
baada ya mwezi m1 kukaa home kuna jamaa alikuwa anafanya bustani ya kuotesha miche ya matunda ya maembe, parachichi(ovakado) na mapapai pembeni kidogo ya home miche mizuri c poaa hafu akawa anauza mia miaa kila mchee nlkuja kupata gepu la jamaa wa nyamongo mgodini (TEGESHA-watu wa tarime wataelewa hapa namanisha nini) anahitaji michee 2000 ya maembee tu hafu alikuwa anapesa nkamwambia mchee m1 ni sh 1000 kwa sababu ni ya kisasa hata akubishaa wala akuomba punguzo...chapu akatoaa milioni 2 mwenye miche shambani nkampa laki 2 tu tukaachanaa naye nkasepa home na 1800000 kidogo nkaanzaa kuwa na nguvu ya kukaa hata na vijana wenzangu mtaani
nkanunua pikipiki ,pikipiki ikanpa chainsaw ikanibidi niaanzishe sehemu ya kuuzaa mbao.. nkajenga kijijini kwetu nyumba ya kawaida bado napambanaa pia..FUNZO KUBWA NILILOPATA NIKIWA JKT

kujiamini---->SIMWOGOPI MTU NA SINA MCHEZO NA MAISHA YANGU
Noma.., ila hapo bi mkubwa kulia umenikumbusha last year nilikataa kwenda jkt basi ukoo mzima ulinipigia simu kunisihi. Wazazi wetu wanakua na imani sana kwamba jkt ni pazuri kumbe jau
Ulikaa miaka mingapi mkuu?
 
huyo jamaa aliyeuliwa jangwani karibu na msitu ni jangwani ya Dar au wapi?

Hawa jamaa wamegeuka SARS ya nigeria
Ni rafiki yetu, rafiki wa wengi.
Mdau mkubwa wa soka na muziki kutoka jijini Tanga.
Wakati fulani aliwahi kuwa meneja wa swahiba wangu Mwinjuma Muumini.
Leo ametangulia mbele ya haki na kuacha simanzi kubwa Tanga na hata Dar es Salaam pia.
Abdul Ahmed "Bosnia" amezimika ghafla.
Kisa kinachosindikiza kifo chake kinaumiza na kinafikirisha sana.
Inasemekana juzi kwa kutumia usafiri wa boda boda alikuwa njiani kwenda uwanja wa Azam Complex Chamazi kuhakikisha mambo yanakaa sawa kwa timu yake ya African Sports ya Tanga dhidi ya Simba katika mchezo wao wa kirafiki.
Kwamba walipopita Jangwani bodaboda aliyembeba aliwatimulia maji watu waliokuwa wakifanya kazi ya kuondoa michanga iliyojazana Morogoro Road kufuatia athari ya mvua za hivi karibuni.
Watu wale ambao wanatajwa kama askari wa Suma JKT wakafanikiwa kuifukuza boda boda na kuikamata na kumtembezea kichapo derava wa boda boda.
Inasemekana Abdul Bosnia akaamua kumtetea bodaboda kwa maneno. Kesi ikahamia kwake akala kichapo kilichosabisha kulazwa Moi - Muhimbili kabla ya kufariki siku ya leo.
Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un.
Said Mdoe 18/11/2020
bosnia.jpg
 
Watu wa wanapenda sana kusukumizia stress zao kwa watu wengine kana kwamba wao hawana changamoto za kisaikolojia.

Inashangaza hakuna hata mmoja kama wapo basi hawafiki watano waliopost kitu positive kuwahusu hawa SUMA guards.
Nao ni bainadamu kama wengine na wanajaribu kujitoa kwenye changamoto waliyoiingia.
 
ngoja uingie kwenye 18 zao mkuu
 
Back
Top Bottom