Walinzi wa kampuni ya SUMA JKT GUARD wana matatizo ya kisaikolojia

Walinzi wa kampuni ya SUMA JKT GUARD wana matatizo ya kisaikolojia

Wapo pale stendi kuu ya Dom, wamekaa kishari Shari tu, ile sehemu inatakiwa watu wanaojua customer care, sio hawa wadogo zetu wenye stress,
Wengine wanaolinda Azania benk Dar, Masdo house, karibu na sanamu ya askari, usiku wanavuta bangi tupu.
 
Habari!

Ukichukua matukio machache yaliyofanywa na hawa vijana wa SUMA JKT GUARD utagundua kuna kitu hakiko sawa. Kuna upepo umepunguza akili zao.

Majuzi jangwani walimpiga yule jamaa wa African sports na kupelekea kifo chake, tena tunapokea taarifa kuwa wamemuua mwananchi asiye na hatia aliyekuwa akilima shambani kwake karibu na msitu wanaoulinda.

Juzi jioni wakati natoka kazini narudi nyumbani njiani nikakutana na kijana wa suma kabeba Kirungu, manati, pingu na vikorokoro vingine anatembea akiekekea lindoni. Jinsi alivyojifanyia camouflage utadhani yupo vitani kumbe anakwenda kulinda kaeneo kadogo tu.

Wale vijana wa SUMA wengi wao ni vijana wa JKT waliomaliza mikataba yao na kurudi nyumbani bila mitaji.
Marafiki zao wengi ni vijana waliokuwa nao JKT ambao sasa ni watumishi wa JWTZ, TISS, ZIMAMOTO , UHAMIAJI, MAGEREZA na POLISI.

Wenzao wanakopa wanajenga, wananunua magari na kusaidia ndugu huku wao vijana wa SUMA wakilipwa kitapeli na kampuni yao ya ulinzi. Take home yao haifiki hata 250k, hawakopesheki benki, ajira yao kufukuzwa ni rahisi, hawana uhakika wa maisha ya uzeeni.
Muda wa kazi ni mwingi.

Hawa vijana wa SUMA wasaidiwe .

Ni vijana waliokosa dira , sasa wamebaki kujitutumua tu ili nao wahesabike kama wanajeshi.

Unajua JKT mtiti wake ni mzito sana, miezi 6 unakula kozi ngumu huku ukiendelea kulima kwa bidii, then umemaliza unaendelea kulimishwa zaidi kila siku. Unavumilia ukijua utafanikiwa mwisho wa siku unapewa nauli tu urudi kwenu, lazima uchanganyikiwe.

Hakuna anayekwenda JKT eti akajitolee tu kisha arudi nyumbani.
Basi serikali itoe mitaji kwa vijana wanaotoka JKT bila ajiraya uhakika ili wakaendeleze fani walizojifunza huko makambini. Wa kufuga samaki au kuku akafuge, wa kujenga akajenge n.k
Mtu amemaliza Kozi, kakaa Kambini miaka (7), Ajira hapati ila Wenzake wanapata na akipata Yeye ni ya Kulinda tu Vyooo unadhani atakuwa sawa?
 
Wapo pale stendi kuu ya Dom,wamekaa kishari Shari tu,ile sehemu inatakiwa watu wanaojua customer care,sio Hawa wadogo zetu wenye stress,
Wengine wanaolinda Azania benk Dar,Masdo house,karibu na sanamu ya askari,usiku wanavuta bangi tupu,
... wanashindwa kutofautisha miamri amri yao ya kijeshi makambini huko na namna ya ku-deal na raia wasiohitaji kujua taratibu zao za kijeshi. Jeshi lilitakiwa kujua hawa wanaenda kutumikia umma na mafunzo yao yawe ya mlengo huo.
 
Huwezi kuamini. Suma jkt guard kuna vijana wasomi wazuri tu.
Suma ya miezi hii sio ile Suma ya wakati wanaanza kuchukua tenda za malindo ya kwenye taasisi. Wale wa mwanzo walikua ni wakali sana harafu uelewa wa mambo ulikua ni mdogo sana.

Vijana wenzangu wa Suma jkt guard msikate tamaa ya maisha. Wote hamuwezi kua polisi, magereza au jw. Tumieni kipato kidogo munachopata kujiendeleza kwa fani mbalimbali za stadi za maisha lakini kupata mitaji.

Wengi wenu bado ni vijana wadogo. Nawasihi muache umalaya sio mzuri, kuna ukimwi na homa ya ini. Kuweni makini sana vinginevyo mutakwisha.
Sasa kama una shule kidogo why usiende GardaWorld, Warrior, G4S au SGA ?

Suma JKT + Maaskari wote Polisu, JWTZ, magereza, Tanzania ni matokeo ya kushindwa kwa CCM.

Tena hao vijana wa kujitolea huko JKT wengi wamekuwa matapeli.

Wana mishahara kiduchuu sana na kwa CCM inawatumia sana miserably imeamua kuwaacha wawe juu ya sheria (Huo ndio mshahara wao).

Suma JKT wanalipwa Tsh 170,000 imagine!

Mtu anakaa JKT miaka 2 unapugwa na kulima bamia kwa ujira wa Tsh 25,000 mtaani wanajua umekuwa askari, halafu unarudi home, kimbilio Suma mshahara Tsh 170,000

Sasa si ni bora ungeenda makampuni ya ulinzi yanayolipa Tsh 250,000 ndani ya miaka 2 ungekuwa ushapiga hatua
 
Wengine wapo bandarini pale wanapigishwa vibarua halafu wanalipwa buku sita tu kwa shift.......wakati vibarua wenzao ambao si watu wa suma wanalipwa zaidi ya iyo yani full unyonyaji kutoka kwa mabosi zao....wenyewe wanadai wao hulipwa 50 elfu tu kwa mwezi walitarajia pale bandari wangepata posho sawa na wenzao ili hata wajiendeleze kumbe wakubwa zao wamewageuza kitega uchumi cha kupiga ela za bandari.....
 
Huwezi kuamini. Suma jkt guard kuna vijana wasomi wazuri tu.
Suma ya miezi hii sio ile Suma ya wakati wanaanza kuchukua tenda za malindo ya kwenye taasisi. Wale wa mwanzo walikua ni wakali sana harafu uelewa wa mambo ulikua ni mdogo sana.

Vijana wenzangu wa Suma jkt guard msikate tamaa ya maisha. Wote hamuwezi kua polisi, magereza au jw. Tumieni kipato kidogo munachopata kujiendeleza kwa fani mbalimbali za stadi za maisha lakini kupata mitaji.

Wengi wenu bado ni vijana wadogo. Nawasihi muache umalaya sio mzuri, kuna ukimwi na homa ya ini. Kuweni makini sana vinginevyo mutakwisha.
Sasa kama una shule kidogo why usiende GardaWorld, Warrior, G4S au SGA ?

Suma JKT + Maaskari wote Polisu, JWTZ, magereza, Tanzania ni matokeo ya kushindwa kwa CCM.

Tena hao vijana wa kujitolea huko JKT wengi wamekuwa matapeli.

Wana mishahara kiduchuu sana na kwa CCM inawatumia sana miserably imeamua kuwaacha wawe juu ya sheria (Huo ndio mshahara wao).

Suma JKT wanalipwa Tsh 170,000 imagine!

Mtu anakaa JKT miaka 2 unapugwa na kulima bamia kwa ujira wa Tsh 25,000 mtaani wanajua umekuwa askari, halafu unarudi home, kimbilio Suma mshahara Tsh 170,000

Sasa si ni bora ungeenda makampuni ya ulinzi yanayolipa Tsh 250,000 ndani ya miaka 2 ungekuwa ushapiga hatua
Wametuibia sana laptop Udom enzi hizo. Tz ni nchi masikini sana sijui kwanini tunajimwambafy, mtu umempa dhamana ya kulinda mali halafu unamlipa 250k!
Suma JKT wanalipwa Tsh 170,000.

Makampuni makubwa kama SGA, Warrior ,G4S au GardaWorld ndio wanalipa Tsh 250,000.

Sometimes, huwezi hata kulaumu maana kima cha chini cha mshahara wa serikali ni Tsh 150,000.

Serikali yenyewe inawaoipa walimu wa shule za msingi Tsh 344,000 kwa mwezi!!!!!!!
 
Back
Top Bottom