Walinzi wa kampuni ya SUMA JKT GUARD wana matatizo ya kisaikolojia


Umenena vyema sana Mkuu. Madogo wakipita hapa watapata kitu.
 
Noma.., ila hapo bi mkubwa kulia umenikumbusha last year nilikataa kwenda jkt basi ukoo mzima ulinipigia simu kunisihi. Wazazi wetu wanakua na imani sana kwamba jkt ni pazuri kumbe jau
Ulikaa miaka mingapi mkuu?
miaka mitatu mkuu kwa mateso makali mno
 
180000/= take home!!! yani nkiishika machine huku nikawa ninamsaidizi nkaingia pori nkadondoshaa mbao wiki 2 nachana mbao c chini ya 600 za nchi 2/6 hapa kuna sehem naziuza directly UBAO 6500 kwa mbao 600=3,900,000tsh toa 900000 kama pesa ya mtaji na usafiri 3000000 kwa 2wiki....hafu uje uniajiri unipe 180000 kwa mwezi kwa akili zipi hizo wakuuu.
 
Umenikumbusha juzi kati kuna mmoja wao alitumia faru john ikamzid akaanza kutamba kwamba wao wanafundishwa kumaliza mchez sio kupiga kuna binti mmoja akamfanyia fujo kumbe huyo binti bwana wake mgambo nilishudia akichwapwa makofi kama mtoto mpaka Leo kupita kijiwen anaona aibu nilijarb kumuuliza kwann mjeda kabisa anapigwa na mgambo akadai askar kwa askar hawapigan
 
Wanafikia htua mpaka wanaua raia halaf unataka tuwasifie mkuu??
 

Kweli kabisa, nina jamaa zangu degree-holder wapo huko huwa najiuliza ni wamezichanga vibaya karata zao au ndio life halina formula???
 
Ni kweli kabisa usemayo,nakumbuka kuna pale Jkt mgulani nilikuwa nasomea udereva,kipindi nasoma nikakuta baadhi ya vijana muda wao wa kuondoka unakaribia ili waje wengine sasa kukawa na sintofahamu wengine baadhi watachukuliwa baadhi wataachwa,siku mbili mbele nikaona wanaambiwa wakachukue vyeti vyao vya service man ili kurudi zao nyumbani,wengi wao walikuwa wanalia wenye roho nyepesi wanaondoka muda huohuo ila wengineo ndio ivyo wanalia na kusikitika,utakuta mtu wakati anatoka kwao aliwaaga wenzake wakijua anaenda kuajiriwa kumbe ajira hakuna na akija kukumbuka wale aliowaacha kitaa maujuzi yao yeye anarudi tu home hana kitu....ila inasikitisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…