Uchaguzi 2020 Walinzi wa karibu wa Mbowe wajiunga CCM, mmoja awa mgombea Udiwani

Uchaguzi 2020 Walinzi wa karibu wa Mbowe wajiunga CCM, mmoja awa mgombea Udiwani

Ulinzi ni ajira yenye kikomo cha mkataba...na siku hizi unaingia mkataba na kampuni sio na mtu
Utakuwa mjinga au mpumbavu kuingia mkataba na kampuni ya ulinzi bila kufanya uhakiki (vetting) achilia mbali kwa mwanasiasa tena Mwenyekiti wa chama ''kikuu'' cha upinzani nchini!
 
Nimetazama video na picha ila sijaweza kujiridhisha kwa 100% kama muhusika ndiye.

By the way, unawezaje kuthibitisha kuwa ni ccm 'wamemchomeka' huyo jamaa Chadema na si kwamba Chadema ndiyo 'imemchomeka' jamaa ccm?
 
Kitu ambacho hujakielewa ni kuwa tofauti na miaka yote, mwaka huu majimboni kuna wagombea wa CCM ambao ni Chadema B yani mwaka huu kuna mgombea wa Chadema na Chadema B. Sasa Jiulize kwanini waliitangulia wote hawakufanya hivi ila Magufuli amefanya. Ni kuwa hana tena uongozi wa kimfumo. Ni dilema.

Sasa unashangaa mlinzi wa Mbowe kuingia kugombea? Tuna mpaka wanausalama wa ndani kabisa huko na wanatupatia mipango yote ovu. Yapo majimbo mawili Dar ambayo msimamizi wa uchaguzi ni mtumishi tukuka ndani ya Chadema. Mbona safari hii mnalo. Nyie wanaccm mumeachwa huku mitandanoni pigeni makelele wee ila mpo mfukoni kama simu zetu. Tunawatoa huko tunawaperuzi then tunawarusisheni humo. Keshokutwa Lissu pia hamtamuona Kisutu na mtatulia tuliiiii!
Duh.. Kujifariji kwingine jamani!
 
Hahah hali ni tete aiseee from kumchukua Dr. Slaa mpk kumkimbilia Mlinzi wa Mbowe?hahahah daah
 
Kamati Kuu ya Chadema ilijifungia Wiki nzima kumtafuta Mrithi wa John Heche kwny Uenyekiti wa Bavicha Taifa wakaishia kumchagua Patrobas Katambi ( Afisa Kipenyo) hahaha na wakawafyeka wale Chadema Itikadi wafia Chama kwa maneno ya kejeli eti Mamluki kumbe wamechagua Membe jr!

Kidumu Chama cha Mapinduzi
 
Msemajiukweli unawaita watu "wajinga" kwa maoni yao, wakati na mimi nakuona wewe mjinga vilevile kwa kuamini mtu akiwa mlinzi wa Mbowe hawezi kujiunga na chama kingine cha siasa, na kama unajidanganya hao walinzi kugombea kupitia CCM ndio watashinda huo udiwani nakupa pole sana kwa ujinga wako.

Washamba kweli, mmechukua baunsa ili akapore ushindi kwa nguvu, kazi mnayo.
 
Mchukueni na msafisha vyoo wake. Maana inaonekana kila aliyewahi kuwa karibu na mbowe ni dili huko magambani
 
Kamati Kuu ya Chadema ilijifungia Wiki nzima kumtafuta Mrithi wa John Heche kwny Uenyekiti wa Bavicha Taifa wakaishia kumchagua Patrobas Katambi ( Afisa Kipenyo) hahaha na wakawafyeka wale Chadema Itikadi wafia Chama kwa maneno ya kejeli eti Mamluki kumbe wamechagua Membe jr!

Kidumu Chama cha Mapinduzi
Huku Ccm na ulinzi wao wote mara paap Mangula kapigwa sumu.

Sijui hata iliwezekana vipi aisee.
 
Kwa hiyo siku jirani yake Mh. Mbowe nayeye akijiunga na CCM pia itakuwa habari siyo!!
 
Ishu si kuhamia CCM ishu ni kwamba wana impact gani katika Chama? Je wana shawishi kiasi kwamba CHADEMA kiteteke?
 
Utaratibu ni uleule hata Chadema wakipata wabunge ama madiwani.kuunga mkono juhudi ni zoezi endelevu.
 
Mimi nilidhani malengo makuu ya CHADEMA ni kushika dola, sikujua kama malengo yao makuu ni ''moto uleule''!
Kwani mlinzi wa Mbowe ndiyo angefanikisha lengo la CHADEMA la kuchukua dola ?

Sikutegemea kama thread ya namna hii inaweza kuletwa na wewe.
 
Utakuwa mjinga au mpumbavu kuingia mkataba na kampuni ya ulinzi bila kufanya uhakiki (vetting) achilia mbali kwa mwanasiasa tena Mwenyekiti wa chama ''kikuu'' cha upinzani nchini!
Usiweke mada mezani ukiwa na majibu yako tayari kichwani

Jr[emoji769]
 
..tutumie MBINU ktk siasa.

..tusitumie HILA ktk siasa.

..sasa ikibaki CCM peke yake hali itakuwaje?
 
Back
Top Bottom