Uchaguzi 2020 Walinzi wa karibu wa Mbowe wajiunga CCM, mmoja awa mgombea Udiwani

Uchaguzi 2020 Walinzi wa karibu wa Mbowe wajiunga CCM, mmoja awa mgombea Udiwani

Jopo la ulinzi wa Freeman Mbowe limejiunga CCM huku mmojawapo akiwa mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM. Tukisema CCM ni mfumo wa kisiasa nchini kuna baadhi ya watu hawaelewi!

Kuna ''wajinga'' fulani wanadhani Siasa za uanaharakati Tanzania zinaweza kuwawezesha kuchukua dola. Upinzani nchini bado sana na kwa siasa hizi za uanaharakati utasubiri sana kupata dola

Maneno ya Mwl. Nyerere yasemayo, ''Mpinzani wa kweli atatoka CCM'' bado mpaka sasa yanasimama

PICHA NA VIDEO:

2485778_FB_IMG_1595009729173.jpg

Waliokuwa walinzi wa Mbowe wakiwa kazini kabla ya kujiunga CCM!

VIDEO ikimuonyesha Mlinzi wa karibu wa Mbowe na jopo lake wakienda kuchukua fomu za Udiwani.

MLINZZI%20WA%20MBOWE%20WEB.jpg

Mmoja wa walinzi wa karibu wa Mbowe akichukua fomu za Udiwani

Mlinzi ni mtumishi si mwanachama, analipwa mshahara, mlinzi si ajira ya kudumu. Mleta mada tueleze nini unataka kutuambia, kuwa wamekimbia chama? Hapana labda tu kama hujui ajira ni nini.
 
Mkuu tatizo sio kwamba mambo yanaendelea, tatizo ni kwann wanaondoka tena wengine hata bila kufukuzwa uanachama, hauoni hiyo Kama ni kasoro kubwa sana?
Mlinzi si mwanachama ni mwajiriwa hana kadi ya uanachama vinginevyo asingekuwa analipwa mshahara. Mchezaji mpira wa klabu si mwanachama ni mwajiriwa.
Uwezo wetu wa kifikiri ni mdogo kwa sababu tunajikita kwenye ushabiki wa kijimga.
 
Kitu ambacho hujakielewa ni kuwa tofauti na miaka yote, mwaka huu majimboni kuna wagombea wa CCM ambao ni Chadema B yani mwaka huu kuna mgombea wa Chadema na Chadema B. Sasa Jiulize kwanini waliitangulia wote hawakufanya hivi ila Magufuli amefanya. Ni kuwa hana tena uongozi wa kimfumo. Ni dilema.

Sasa unashangaa mlinzi wa Mbowe kuingia kugombea? Tuna mpaka wanausalama wa ndani kabisa huko na wanatupatia mipango yote ovu. Yapo majimbo mawili Dar ambayo msimamizi wa uchaguzi ni mtumishi tukuka ndani ya Chadema. Mbona safari hii mnalo. Nyie wanaccm mumeachwa huku mitandanoni pigeni makelele wee ila mpo mfukoni kama simu zetu. Tunawatoa huko tunawaperuzi then tunawarusisheni humo. Keshokutwa Lissu pia hamtamuona Kisutu na mtatulia tuliiiii!
Unajifariji.
 
MaCCM akili zenu azina akili kabisa, mnahangaika mno na Mbowe.
Yaani hapo jamaa kawatoa na pesa kisa tu alikua mlinzi wa Mbowe. Mmekwama MATAGA, mnashindwa hata kuelewa kua ulizi ni kazi tu ya mkataba.
 
Mkuu, mm sikuchangia kishabiki, ila nilichangia mada kwa kina na kwa mapana yake, Nina hakika kabisa hukutafakiri kwa kina kabla ya kuandika hii post yako, ulichokiandika hapa hakina logic, je akina kubenea ambao Wameondoka juzi tu na mwenyewe alikuwa mwajiriwa??
Mlinzi si mwanachama ni mwajiriwa hana kadi ya uanachama vinginevyo asingekuwa analipwa mshahara. Mchezaji mpira wa klabu si mwanachama ni mwajiriwa.
Uwezo wetu wa kifikiri ni mdogo kwa sababu tunajikita kwenye ushabiki wa kijimga.
 
Mkuu, mm sikuchangia kishabiki, ila nilichangia mada kwa kina na kwa mapana yake, Nina hakika kabisa hukutafakiri kwa kina kabla ya kuandika hii post yako, ulichokiandika hapa hakina logic, je akina kubenea ambao Wameondoka juzi tu na mwenyewe alikuwa mwajiriwa??
Samahani sikujua kuwa wakina Kubenea walikuwa walinzi wa Mbowe, kumbe wabunge wote wa Chadema ni walinzi! And this is JF of GT's!
 
Nafukua Kaburi.. Kuna walinzi waliotekwa Usiku hotelini. Kisha Kuna kina Lingwenya na Adamoo waliotekwa Rau mchana. Halafu Kuna Hawa waliohania CCM Mara baada ya wenzao Kutekwa!
 
Uzi kama huu unaonesha ni namna gani walinzi wa Mbowe au watu wake wa karibu wanavyofuatiliwa kwa nia ovu na kundi la wahuni wa CCM.
 
Ccm bhana! Yaani hawaoni kazi kutumia kiasi chochote kile cha fedha kwa lengo moja tu la kuendelea kubakia madarakani.
 
Back
Top Bottom