Walinzi wa rais wetu fitness yao vipi?

four eyes

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2017
Posts
905
Reaction score
1,408
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia Kwa umakini muonekano wa walinzi wa rais wetu mpendwa ukilinganisha na walinzi wa Marais wengine

Katika kufatilia huko nimegundua kuwa muonekano wa walinzi wa Marais wengine ni wa kikakamavu sana ukilinganisha na walinzi wa Marais wetu hapa tanzania ambao ni watu wazima hv wenye vitambi vyao ambao wananipa shaka kama wanaweza kukurukakara za kukabiliana na mtu mkakamavu au mbio za kukimbizana na mhalifu anayetoroka,nimejaribu kuweka picha za walinzi wa Marais mbalimbali na hawa wa kwetu mjinee.

Karibuni wadau mchangie mnauonaje monekano wa walinzi wetu wa rais na kama unakidhi mahitaji ya unyeti wa kazi yao.
 
Tatizo lako mbona dogo sana mkuu. Jaribu kukatisha uende kuchukua kiatu chako pale kwa mng'arishaji uone. Waona hata kuleee mbali kwenye magari waliokaa kibwege bwege?? Wote walinzi wale. Sasa sijui unataka ulinzi wa wakimbiaji?? Ingelikuwa hivyo wangeli tafuta wamasai wezi wa mifugo tu
 
mlinzi ana kitambi?? hii ni bongo tu
 
Halafu kuna hili la askari polisi hao wapya wanaorandaranda mitaani na kuongoza magari, mbona wana miili kidogo sana maumbo yao ni madogo mno , sidhani kama wataweza kumdhibiti mtu mwenye kilo tisini wale, sijui kwa nini wale maaskari polisi wa miaka ile ya themanini na mwanzoni mwa tisini kama watakuwepo tena, hawa wa sasa niliwaona huko TZ, mpaka wanangu wakawa wanawashangaa eti ndio askari wetu mbona wadogo hivyo.
 
Hao wakikudaka hawana maneno mengi mkuu pamoja na kusema wana miili midogo'Ukibanwa praizi kwenye pumbu na kupigwa rungu za ugoko utawaheshimu tu mkuu.'Utake usitake mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…