Walinzi wa rais wetu fitness yao vipi?

Amenena vyema ila hajajibu swali langu la ubora wa walinzi wetu
Mkuu Ubora wa kitu chochote unapimwa kutokana na vitu vitatu

1 Performance
2 Stability
3 Nature

Kazi ya TISS ni ulinzi wa viongozi je nikuulize swali ulishawai kusikia kiongozi ambaye yuko under TISS protection amepata madhara ?
kama ujawai kusikia kwanini upate wasiwasi na weledi wa kazi wanazofanya??

Ngamanya Kitangalala
 
Anauliza ile ya mzee mwinyi alivyonyukwa kibao
 
Ufafanuzi wako ni mzuri sana, ni somo tosha. Hata hivyo katika uandishi wako inaonekana umeathiriwa sana na lugha ya mama, KIHAYA. Inapunguza utamu wa andiko lako.
 
Tuelezee kidogo hizo performance, stability and nature mkuu. Ila Walinzi wetu unadhani wanaelimu ya chuo na hizo 3.5 GPA??
 
Anauliza ile ya mzee mwinyi alivyonyukwa kibao
Kuna kitu kinaitwa Protection Clearance level (PCL) na ndani ya PCL kuna vitu viwili au Clearance level 2

1 Presidential Proctection (PP)
2 Executive protection (EP)

PP na EP refers to security measures taken to ensure the safety of VIPs

Presidential Proctection Clearance level nimesema zipo 5 na zinatumika kutokana na mazingira mfano rais anapokuwa ndani ya Ikulu je ulinzi wake ni sawa kama anavyokuwa nje ya ikulu?

Executive protection ni ulinzi wanaopewa watu au viongozi wa kitaifa na wastaafu ulinzi huu ni tofauti na Presidential Proctection ambao mara nying ni kwa ajili ya Rais tena ambaye yuko madarakani

Leo Obama msafara wake ni wa gari tatu moja yake mbili za walinzi so ulinzi wake umepungua si sawa kama alivyokuwa ni rais wa US

Kingine tafuta video ya Mzee Mwinyi then angalia vizuri utagundua kitu kuwa yule jamaa alikuja si kwa kuvamia au kufanya kitu alikuja kama ni mmoja wa Crew member wa ile shuguli kumbuka ilikuwa ni shuguli ya kidini na alikuja kama ni fundi mitambo na alikuja kama anarekebisha mike ndio akafanya tukio lile ambalo naimani hakuna mtu aliyetarajia kwa tukio lile kufanyika kwenye shuguli kama zile hasa za mambo ya kiimani
 
Mzee Mwinyi aliposhambuliwa alikuwa analindwa na watu gani? Kinachowasaidia viongozi wetu ni utulivu na nidhamu ya Watanzania.
Lkn natabiri, kwa matendo ya viongozi wetu wa leo, siku zinakuja tutaanza kuona wakishambuliwa...
 
Si ujaribu kupenya kwa nguvu mkuu kama hujapasuliwa kichwa.Thread zingine huwa hazina maana kufunguliwa
 
Jaribu siku moja kumvamia Rais akiwa kwenye ziara au mkutano wowote hapo ndipo utakapopata jawabu la swali lako.
 
Kwa mantiki hiyo huyo nae n mmoja wamo ya walinzi wake au watalaam wa mafunzo ya ulinzi kama n MTU baki s angekurupuka na kwenda kumvamia nakumbuka mh bush aliwah rushiwa kiatu na hii huwa wanajiandae walinzi wa viongozi wetu?
 
Kwa mantiki hiyo huyo nae n mmoja wamo ya walinzi wake au watalaam wa mafunzo ya ulinzi kama n MTU baki s angekurupuka na kwenda kumvamia nakumbuka mh bush aliwah rushiwa kiatu na hii huwa wanajiandae walinzi wa viongozi wetu?
 
Raisi analindwa Na Team Kubwa asilimia kubwa ya walinzi hao ni invisible hawaonekani Ambao huonekana ni Detail Leader na mpambe ambae ni Aided de Camp (ADC)
 
Usije ukapma uwezo wa mtu kwa kumwangalia Ndugu Yangu utakuja kupgwa ngumi moja mpka uanze kuoza saiyo iyo
 
Walinzi wa Tanzanian kwasababu hawajawahi kukutana na mikimikiki. wakati wanamlinda raisi kwahiyo hatuwezi kujua uimara wao
 

Aiseee,

Mleta Uzi nakuona tayari uko kwenye ule mstatiri wenye kona nne katika jeneza tukiimba haka kawaimbo haka ka kanisa za kuletwa na wazungu kanaitwa Aaaagh nimekasahau tena oooh, kanaitwa *tuonane mbinguni, wanaongezea tuonane bandarini kule* ila sina uhakika sana kama ndiyo hako kawimbo.

Labda, niseme, hivi kwa kifupi, hao jamaa zali likitokea au wewe mleta huu uzi ukijaribu sumu kwa kuilamba ndiyo utaelewa majibu yake na kisha utatuletea mrejesho kamili usio kuwa na chenga wala maswali.

Pia, niongezee tu kuwa hao jamaa wako vizuri mno kuliko unavyofikilia au kuwaona kwa macho.

Mwisho, ulinzi wa viongozi Wakubwa wa nchi yetu kuna ngazi nyingi sana zaidi ya ngazi tano , kwa hiyo hao wanaoonekana wako jambo ile sana pia wako wanyama makundi tano ambao hawaonekani hapo nao wako vizuri sana mno.

Kwa hiyo, nikushauri kuwa hebu jaribu uuone mziki wake kisha utaleta muendelezo wa huu uzi wako kama mrejesho ,

Japo , ninauhakika kuwa hutarudi maana tutakuwa tayari tunapiga pambio la makaburini!

Kwa hiyo mrejesho, itakuwa ni makaburini au mabepwande huku ukiwa umeisha ny'ofolewa moyo , figo na maini hadi na ulimi bila ganzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…