KERO Walinzi wa viwanja vya Mnazi Mmoja wamekuwa kero

KERO Walinzi wa viwanja vya Mnazi Mmoja wamekuwa kero

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Siku moja natoka kazini (4 June 2025) nikakutana na mpenzi wangu maeneo ya mnazi mmoja hospital, kutokana na kelele zilizokuwepo pale nje ikabidi tusogee uwanjani kwakuwa kuna mwanga na usalama zaidi.

Kitendo cha kufika pale, walikuja vijana wawili ambao wamevaa kiraia, walifika kwa matusi na vitisho na kujitambulisha kama maaskari walinzi wa uwanja huo na kwamba muda wa kuwa kwenye uwanja huo ushapita.

Wakatuburuza mimi na mpenzi wangu tukawekwa chumba fulan palepale, mimi sikutoa ushirikiano mpaka alipofika askari aliyevaa sare na alikuwa na kitambulisho pamoja na silaha.

Walituambia tutoe laki moja tuachiwe ila nilipokataa wakampigia mkubwa wao wa kazi ambaye sikujua jina lake. Yule mkubwa wao alisema kosa la kukaa pale faini yake ni laki tatu😢.

Kilichoniumiza kipindi nafika pale nilipewa ruhusa ya kukaa pale na mtu mmoja ambaye sikujua kama ni askari ila huyo huyo ndo alitugeuka na kutupiga hela yote hiyo.

Kero yangu:

Je, Haturuhusiwi kwenda Mnazi Mmoja uwanjani mpaka liwe tamasha?

Muda wa kukaa pale mwisho ni saa ngapi? Na ikiwa nimekaa zaid ya muda huo ni adhabu gani napata?

Na je.! Askari yeyote ambaye hana sare, hana kitambulisho wala silaha anaruhusiwa kukamata? Kama kuna utaratibu maalum naomba utolewe maana kuna dhuruma inafanyika Sana na marafik wa maaskari ambao hawana taaluma ya uaskari.

Endapo kama kuna namna naweza kutoa ushuhuda wangu, niko tayari kushirikiana na mamlaka kutokomeza hii tabia.

Tunaumia jamani kwenye hili
 
Na je.! Askari yeyote ambaye hana sare, hana kitambulisho wala silaha anaruhusiwa kukamata? Kama kuna utaratibu maalum naomba utolewe maana kuna dhuruma inafanyika Sana na marafik wa maaskari ambao hawana taaluma ya uaskari.

Endapo kama kuna namna naweza kutoa ushuhuda wangu, niko tayari kushirikiana na mamlaka kutokomeza hii tabia.💪🏿🙏🏿
 
Serikali ya CCM ndio inawapa nguvu watu km hao maana wanajua hkn ppt utapata HAKI Yako zaidi Zaid ukisema ulishupaliee utapotezaa pesa na muda wako......ss ungana uku tuwafanye jambo tutokomezee uozo huo
FB_IMG_1749139137988.jpg
 
Pole mkuu ila pale sio eneo sahihi la kukaa, usalama ni mdogo wahuni kibao.

Jana nimekatiza uwanjani mishale ya saa 4 usiku kuna wadau wakaniongelesha ila kama kawaida yangu mtu yeyote ambae simjui akiniongelesha barabarani huwa simzingatii na simjibu kwa faida ya usalama wangu.

Huwa wanakamata sana wahuni hapo, kuna siku mchana walikamata wahuni kama 20 hivi kwahiyo sio eneo zuri la kukaa kama hakuna mechi au event yeyote.
 
Daah kwahiyo mwanangu walikuvua 100k kimasikhara kabisa.??
 
Back
Top Bottom