Mtikila alikomaa hadi akapata usajili wa kudumu.
Subira na uvumilivu na ari ya kupambana ndizo zilipeleke D. P kusajiliwa.
Hawa viongozi wa C . C. J waliojitoa, sidhani kama wana nia ya kudhati ya kuleta upinzani hapa nchini kwetu.
Hawa ni waganga njaa, wenye uchu na uroho wa madaraka.
Tuwakatae popote watakapoenda.
Tuwachukulie kwamba wanajua sana maana ya siasa za Bongo. Unadhani kama ungekuwa wewe mkuu ungefanyaje, kama Mtikila? Lengo la ccj labda halikuwa kupata publicity kama Mtikila? Mtikila ameachieve alichotaka - umaarufu. CCJ walitaka kuleta upinzani wa kweli wa kisayansi ambao ulishaona CCM walichanganyikiwa kuona wanazidiwa kete, wakatumia nguvu waliyonayo kuzima progress za CCJ ambao walikwishajizolea ufahamu wa watu kibao wa kuwapo kwao na matumaini ya kisiasa.
Mwenyekiti wa Chadema alisema openly kwamba siasa ni opportunistic game, hata ukiwa angani unaweza kubadili gear ili kuhakikisha kinaeleweka. Nakubaliana naye. Kama tungekuwa na siasa za kistaarabu ambazo kila mtu anapewa fulsa sawa na mizengwe inadhibitiwa kwa aliyemo na asiyekuwamo, siasa unazotaka tuzing'ang'anie zingefaa. Wamewasoma chadema wakaona angalau kuna lugha wanayoweza kuelewana, wasingeweza kuingia moja kwa moja kwa sababu ya tofauti zao fulani, lakini baada ya kuona wamewekewa nondo wasipite wanakloenda wakaona bora kupitia dirishani kama mlango umezibwa. Huko mbele unajuaje, labda wataendelea na harakati zao?
SIasa za Afrika ni ngumu sana kwa sababu aliyepata hataki kutoka kwa nguvu zozote hata ikibidi kuua. Hiyo ndiyo Afrika yetu. Siwalaumu CCJ waliojiunga chadema, sijui wangejiunga wapi, maana kwa Tanzania bara chadema ndio angalau wanakubalika zaidi na ushiriki wao. CUF sawa, lakini Visiwani kwanza. UDP kanda ya ziwa kwanza, NCCR bado longolongo nyingi, Jogoo ni chama cha mtu mmoja mmoja, akisema mwenyekiti ni kwisha maneno. Ndio demokrasia yao.
Ajabu iko wapi kwa walichofanya ccj kutafuta uwakilishi bungeni zaidi kupitia chadema ghafla ghafla? Mbona kina Mtemvu walitoka cuf wakanyaka post ccm chap chap? unamsikia siku hizi mwanasheria machachari aliyekuwa chadema akaingia ccm na kuwa mlinzi wao mara moja? sikumbuki jina - matatizo? Mashaka sielewi. Wengi tu walipohamia ccm walipewa ukuu wa wilaya, vyeo kibao..... Kwa nini isiwe vinginevyo kwa wengine?
Mimi sina chama chochote kichwani wala mwilini mwangu, navichukulia vyama vyote ikiwemo ccm kwamba ni vyama vya kugangia njaa kwa kila anayeipiga vizuri hesabu ya kuingilia huko. Najua kwa hakika kwamba chama chochote kingekuwa madarakani kingedhibiti wengine wasizoe madaraka kama wafanyavyo ccm. Nyanya zote ni sawa tu, tofauti ni aliyezibeba.
Siasa is not really a profession, it is a rough way of life ambayo ukiweza kuwadhibiti watu na akili zao basi wewe umewini. Kama mchezo wa kuigiza vile, ukijua watu wanataka kusikia nini ukakisema hicho umewapata. Ukiwaambia ukweli watu hao usitegemee kuwapata. Mwongo ndiye mtaalam wa siasa za kubadili maneno kila saa kufuatana na upepo.
Mwanaume mkweli sana ni vigumu kupendwa na watu wengi, hata wengine wanashindwa kupata mke. Waongo wengi wanafanikiwa sana kwenye maeneo yoyote yale - kibiashara, kimaisha, nk. Let CCJ members maximize this opportunity of trial and error in their endevor to achieve their dreams. Nimependa walivyo sharp kufikiri. Kumwiga Mtikila maana yake wangeendelea kuzozana na Tendwa ambaye kashika mpini na nyuma yake kukiwako na dola zito lililoko tayari kummeza yeyote aliye kinyume nao. Vita anayeshinda ni yule mjanja. Retreating doesn't mean a surrender.