Waliochaguliwa kuandaa mpango wa maendeleo 2050 wote wanaishi Mbezi Beach au Masaki, wanalishwa kwa kodi za umma miaka yote, wana umri zaidi ya 50 yrs

Waliochaguliwa kuandaa mpango wa maendeleo 2050 wote wanaishi Mbezi Beach au Masaki, wanalishwa kwa kodi za umma miaka yote, wana umri zaidi ya 50 yrs

1. Mbona hawa wamo au hujamuona Rais wa Tanzania Startup association. Pia yumo Dk Neema Mduma ndio ali design mifumo ya machine learning kubashiri mabinti kuacha shule kisa ujauzito!!. So watu wa technology ni wengi humo. Pia wapo wajasiriamali mfano hapo Mgetta she's an entrepreneur pia board member Tantrade.

2. Why academicians? Dunia nzima kazi za consultancy na strategic plans hakuna watu better kuziandaa kuliko Academicians. Hawa laymen/wafanyabiashara wataitwa tu watoe maoni ila wanaoandaa draft zile have to be academicians maana wamebobea kwenye hizo mambo kwa miaka mingi.

Ambacho labda hakijakaa sawa kama ulivyosema ni balance ya wasomi vs kada zingine. Sema mpango wa taifa ni framework tu mfano watasema Huduma za afya kupitia bima ya wote. Sasa mpango wa miaka mitano mitano ndio utaeleza KIVIPI hiyo vision inatekelezeka.

4. Ila miaka yote tatizo sio uandaaji mpango ila utekelezaji. Mfano mpango wa 2015-2020 ulisema Tanzania nchi ya viwanda alafu wa 2021-25 unasema tumeshavuka kuwa nchi ya viwanda eti sasa tunafanya value addition ili kuuza nje na sio kuuza raw material kama zamani. Ni maneno ya karatasi tu ila hakuna hata kiwanda kimoja cha kueleweka hapa nchini mfano say magari, ndege, kuchenjua dhahabu n.k
Hii ni paper work kama zilizopita, hakuna jipya mkuu. Time will tell.
 
Unamjua Dr Mduma? Umaarufu kaupata kwa tafiti anazofanya huko duniani tena ni practical. Nimekueleza kaandaa hadi mfumo wa kubashiri wajawazito mashuleni kutumia takwimu ili kupunguza school dropouts. From machine learning to Artificial Intelligence anatuwakilisha huko duniani na umri wake ni less than 40 unampuuzaje mtu wa hivyo!!

Kabudi na Osoro walifanya kazi bila uhuru mfano Rais ameshasema tunaibiwa madini wasingeweza kuonyesha hatujaibiwa!! Na hii ni shida ya taasisi kufanya kazi bila uhuru. Ila watu wakipewa uhuru kama alivyosema Leo Mama Samia obvious watajimwaga wanavyoweza. Nadhani it's clear Mama Samia ni pragmatic kuliko JPM ndio maana licha ya kupinga katiba mpya ila bado kikosi kazi kikashauri katiba mpya ni lazima. Hayo yasingewezekana chini ya JPM otherwise angehukumu wanyongwe kwenye Live TV.
Utakuwa mpumbavu hohe hahe ukiamini suala la mimba na school drop outs ni kati ya matatizo yanayofanya nchi isipige hatua za maendeleo..si kila kipya anacholeta mtu kina umuhimu, vingine ni vitu vidogo na havina impact kwa jamii..na hicho alichofanya huyo dokta wako ni mojawapo.
 
Kama kuna ambaye anayo tathmini au matokeo ya zile INVESTMENT GUIDE kwa kila mkoa zilizoandikwa na ESRF/UNDP ikionyesha badiliko lolote chanya la uwekezaji ktk mkoa husika tofauti na hali ilivyokuwa awali..nitamshukuru sana.
 
Sasa Kitila na Degrees zake za sociology anajua nini!!!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Kuna mtu juzi kaniambia, huenda 2050,Mikoa iliyo vizuri kiuchumi ikarudi nyuma kama Singida. Nilimwuliza ni kwa nini, akanjibu anayepanga [ Waziri wa Mipango] anatoka Singida. Na anayetoa fedhs za Mipango hiyo[ Waziri wa Fedha] naye anatoka Singida. Tena wote ni Wanyira. Niliishia kucheka.
 
Hii ndio gharama ya kukosa upinzani,wanaamua tu lolote linalo furahisha nafsi zao mwafrika. ni mtu hatari Sana,Angalia mtaala mpya eye "ETI WAMEWEKA UFUGAJI WA NYUKI"
umeona mawazo ya Hawa wazee wa CCM,katika Karne ambao watu wanapaa kwenda sayari nyingine wewe unafundisha kufuga NYUKI,hii ni laana,Hawa wazee wamelaamiwa
 
Mhe. Waziri Kitila Mkumbo ametoa majina ya watu alioteua kutengeneza mpango wa 2050. Wote walioteuliwa wana miaka 50 kwenda mbele, ni wake au watoto wa viongozi wa CCM, ni wanazuoni waliofundisha na kusoma naye chuo...........hizi siyo zama za giza ni zama za technology. Hakuna namna hawa wazee wanaweza kuweka projection za nchi kuendana na technology badala yake watakwenda kutuletea nadharia kwenye vitabu

Tulitegemea kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMa na watu wenye mafanikio kwenye jamii wakiwa Sehemu ya timu . Academia wangebaki kwenye technical team ya waandishi siyo wachakata hoja.

Tunaanza kufeli kupanga kama Ishara ya kufeli kufanikiwa...........nchi haiwezi ikapangiwa kila kitu na wakaazi wa mbezi beach inahitaji watu wa namtumbo, Kaperamsenga na Kipandaule washiriki pia.

Hawa watu wa masaki na Mbezi Beach wanawekwa kwenye mipango ya nchi ndio wanaotengeneza propaganda za utajiri kwenye umaskini. Mtu kazaliwa hadi anazeeka yupo analishwa na serikali kwa kodi za wananchi anawezaje kujua matatizo ya wananchi? Ndio hawa badala ya kuripoti uhalisia wao wanaripoti uongo na uzandiki walioandika kwenye vitabu vyao.
Ni kweli. bado kuna jamii zinaishi maisha ya miaka ya kijima , hao wanajua hilo? Zinatakiwa tafiti kwenye jamii za namna hii na kufikiri jambo gani lifanywe. Mipango imekuja ns kuondoka lakini bado tuko nyuma tu. Watu wanaoishi kwenye marimari hawawezi kuwapangia maendeleo wanaoishi kwenye matembe!
 
Utakuwa mpumbavu hohe hahe ukiamini suala la mimba na school drop outs ni kati ya matatizo yanayofanya nchi isipige hatua za maendeleo..si kila kipya anacholeta mtu kina umuhimu, vingine ni vitu vidogo na havina impact kwa jamii..na hicho alichofanya huyo dokta wako ni mojawapo.
Nimekupa mfano tu wa mambo aliyofanya, ila huyo ni mtaalamu wa machine learning, Computer engineering, computer science, artificial intelligence. Na wana miradi kibao tu ya kuendeleza sayansi mashuleni na kwa wanawake, kuunda mifumo ya kupredict ubora wa mazao.

Pitia twitter page yake ndio utapata picha alivyo mtu wa muhimu. So inclusion yake is well deserved.
 
Sema makada wengi sana kwenye hiyo kamati.
 
Of course huwa ni makaratasi tu ila utekelezaji ni zero. Nashagaa concern ya watu ni timu inayoandaa chapisho instead of kuhoji utekelezaji huwa unakwama wapi?
unakwama hapa, Kinachoandikwa ni nadharia zisizotekelezeka..
 
Nimekupa mfano tu wa mambo aliyofanya, ila huyo ni mtaalamu wa machine learning, Computer engineering, computer science, artificial intelligence. Na wana miradi kibao tu ya kuendeleza sayansi mashuleni na kwa wanawake, kuunda mifumo ya kupredict ubora wa mazao.

Pitia twitter page yake ndio utapata picha alivyo mtu wa muhimu. So inclusion yake is well deserved.
Unajua vyuo vyetu kwa nini vimepoteza ile credibility viliyokuwa nayo awali..ni kuruhusu vitu vidogo vidogo km hivi anavyofanya huyu Madam vifanyike kwa jina la chuo, vimiradi vidogo vidogo vyenye lengo la kupata hela hata km ni ndogo, na wazungu ndio wanataka hivyo, sababu kwao ni signal kwamba sisi hatuwezi mambo makubwa yenye athari kubwa zaidi.. ni km vile una matatizo 10 umeorodhesha kwa uzito na kipaumbele, sasa wewe unaacha yale 9 ya mwanzo unakwenda kushughulikia tatizo la 10 ambalo ni la mwisho kwa umuhimu halafu unaweka mabango utambuliwe wewe ni bingwa..sidhani km trend ya namna hii imekaa sawa! Ok muulize huyo Dr. ana hata kitabu au makala yoyote ya eneo la ubobezi wake?
 
Kama kuna ambaye anayo tathmini au matokeo ya zile INVESTMENT GUIDE kwa kila mkoa zilizoandikwa na ESRF/UNDP ikionyesha badiliko lolote chanya la uwekezaji ktk mkoa husika tofauti na hali ilivyokuwa awali..nitamshukuru sana.
Bado iko kwenye mchakato...[emoji16]
 
Kuna mtu juzi kaniambia, huenda 2050,Mikoa iliyo vizuri kiuchumi ikarudi nyuma kama Singida. Nilimwuliza ni kwa nini, akanjibu anayepanga [ Waziri wa Mipango] anatoka Singida. Na anayetoa fedhs za Mipango hiyo[ Waziri wa Fedha] naye anatoka Singida. Tena wote ni Wanyira. Niliishia kucheka.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom