Waliochaguliwa kuandaa mpango wa maendeleo 2050 wote wanaishi Mbezi Beach au Masaki, wanalishwa kwa kodi za umma miaka yote, wana umri zaidi ya 50 yrs

Hii ni paper work kama zilizopita, hakuna jipya mkuu. Time will tell.
 
Utakuwa mpumbavu hohe hahe ukiamini suala la mimba na school drop outs ni kati ya matatizo yanayofanya nchi isipige hatua za maendeleo..si kila kipya anacholeta mtu kina umuhimu, vingine ni vitu vidogo na havina impact kwa jamii..na hicho alichofanya huyo dokta wako ni mojawapo.
 
Kama kuna ambaye anayo tathmini au matokeo ya zile INVESTMENT GUIDE kwa kila mkoa zilizoandikwa na ESRF/UNDP ikionyesha badiliko lolote chanya la uwekezaji ktk mkoa husika tofauti na hali ilivyokuwa awali..nitamshukuru sana.
 
Sasa Kitila na Degrees zake za sociology anajua nini!!!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Kuna mtu juzi kaniambia, huenda 2050,Mikoa iliyo vizuri kiuchumi ikarudi nyuma kama Singida. Nilimwuliza ni kwa nini, akanjibu anayepanga [ Waziri wa Mipango] anatoka Singida. Na anayetoa fedhs za Mipango hiyo[ Waziri wa Fedha] naye anatoka Singida. Tena wote ni Wanyira. Niliishia kucheka.
 
Hii ndio gharama ya kukosa upinzani,wanaamua tu lolote linalo furahisha nafsi zao mwafrika. ni mtu hatari Sana,Angalia mtaala mpya eye "ETI WAMEWEKA UFUGAJI WA NYUKI"
umeona mawazo ya Hawa wazee wa CCM,katika Karne ambao watu wanapaa kwenda sayari nyingine wewe unafundisha kufuga NYUKI,hii ni laana,Hawa wazee wamelaamiwa
 
Ni kweli. bado kuna jamii zinaishi maisha ya miaka ya kijima , hao wanajua hilo? Zinatakiwa tafiti kwenye jamii za namna hii na kufikiri jambo gani lifanywe. Mipango imekuja ns kuondoka lakini bado tuko nyuma tu. Watu wanaoishi kwenye marimari hawawezi kuwapangia maendeleo wanaoishi kwenye matembe!
 
Nimekupa mfano tu wa mambo aliyofanya, ila huyo ni mtaalamu wa machine learning, Computer engineering, computer science, artificial intelligence. Na wana miradi kibao tu ya kuendeleza sayansi mashuleni na kwa wanawake, kuunda mifumo ya kupredict ubora wa mazao.

Pitia twitter page yake ndio utapata picha alivyo mtu wa muhimu. So inclusion yake is well deserved.
 
Sema makada wengi sana kwenye hiyo kamati.
 
Of course huwa ni makaratasi tu ila utekelezaji ni zero. Nashagaa concern ya watu ni timu inayoandaa chapisho instead of kuhoji utekelezaji huwa unakwama wapi?
unakwama hapa, Kinachoandikwa ni nadharia zisizotekelezeka..
 
Unajua vyuo vyetu kwa nini vimepoteza ile credibility viliyokuwa nayo awali..ni kuruhusu vitu vidogo vidogo km hivi anavyofanya huyu Madam vifanyike kwa jina la chuo, vimiradi vidogo vidogo vyenye lengo la kupata hela hata km ni ndogo, na wazungu ndio wanataka hivyo, sababu kwao ni signal kwamba sisi hatuwezi mambo makubwa yenye athari kubwa zaidi.. ni km vile una matatizo 10 umeorodhesha kwa uzito na kipaumbele, sasa wewe unaacha yale 9 ya mwanzo unakwenda kushughulikia tatizo la 10 ambalo ni la mwisho kwa umuhimu halafu unaweka mabango utambuliwe wewe ni bingwa..sidhani km trend ya namna hii imekaa sawa! Ok muulize huyo Dr. ana hata kitabu au makala yoyote ya eneo la ubobezi wake?
 
Kama kuna ambaye anayo tathmini au matokeo ya zile INVESTMENT GUIDE kwa kila mkoa zilizoandikwa na ESRF/UNDP ikionyesha badiliko lolote chanya la uwekezaji ktk mkoa husika tofauti na hali ilivyokuwa awali..nitamshukuru sana.
Bado iko kwenye mchakato...[emoji16]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…