Waliodukua na kubadili hotuba ya Spika Ndugai wasakwe na kukamatwa maana huo ni uzandiki wa kumchonganisha na mkuu wa nchi

Hakuna mtu aliyedukua hotuba. Hata leo hajabadilisha kauli ya ukubwa wa madeni na hatari iliyo mbele yetu ya nchi kupigwa mnada
 
ndugai na jopo lake ni watu wazima, hapo kaomba radhi kuwapoteza maboya, kukosoa mkopo wala si kauli ya kwanza alianzia kwenye sheria mbovu zinazotungwa na mawaziri na makatibu wao zinazopitishwa kihuni bungeni , kisha alitoa kauli ya kupinga katazo la serikali la twishweni wakati wa likizo, hawa watu wanamipango yao na ifikapo wakati sahihi ndo watatoka hadharani.
 
Mama kama ana akili ( na anaonekana anazo) inabidi awe makini na haya mapoyoyo ambayo mara baada ya JPM kumaliza safari yake iliyotukuka hapa duniani yalimgeuka na kuanza kumtukana. Haya maakina Ndugai, Nape, na wengineo. Wanafiki hawanaga misingi watakugeuka na kukung'ata tu pale wanapoona inafaa.
 
Tuanzie hapa kwanza.

Your browser is not able to display this video.
 
kiukweli spika hana kosa kuishauri selikali ndio wajibu wake na ilitakiwa iwe ivyo tangu mwanzo.sasa hoja iko hapa wenzako waliosema uliwaita kwenye kamati ya maadili.sasa huu uzalendo kautoa wapi ghafula?
 
.
 
Wewe unahangaikaga sana kutetea visivyowezekana kutetewa...!!! Si unakumbuka ulivyokuwa unaanzisha nyuzi za kumtetea SABAYA..!? Leo kiko wapi? Huyo unayetaka kumtetea sasa hivi hajadukuliwa..
 
Huenda ni mbowe
 
Amelazimishwa ni mnafiki sn huyu mzee
Unafikiria kwa huo msamaha wa kinafiki, mama atakuwa amemsahau"nimekusamehe lakini sitokusahau"kwani matamshi yake yalikuwa wazi kabisa hakuna kusema kuwa amelishwa maneno!!hapo lichopunguza ni matusi tu kutoka kwa wana ccm wenzake, lakini heshima tayari imeshapotea!!
 
Wewe unahangaikaga sana kutetea visivyowezekana kutetewa...!!! Si unakumbuka ulivyokuwa unaanzisha nyuzi za kumtetea SABAYA..!? Leo kiko wapi? Huyo unayetaka kumtetea sasa hivi hajadukuliwa..
Jamaa halielewi hata maana ya kudukuliwa!!yaani mtu yuko ukumbini ana hutubia, clip yake inatoka unasema kadukuliwa!!ila mama ameshapata sura halisi ya Ndugai!!
 
Je Ndugai alikuwa na hoja ama hakuwa na hoja?
 
Wewe unahangaikaga sana kutetea visivyowezekana kutetewa...!!! Si unakumbuka ulivyokuwa unaanzisha nyuzi za kumtetea SABAYA..!? Leo kiko wapi? Huyo unayetaka kumtetea sasa hivi hajadukuliwa..
Wewe unajua nini kuhusu kesi na justice system?
 
Wewe unajua nini kuhusu kesi na justice system?
Sijui chochote zaidi ya kwamba SABAYA kala mvua 30 ... Wewe unayedhani unajua makorokocho hayo, maneno yako hayajabadilisha ukweli kwamba aliyotuhumiwa nayo yamethibitishwa na mahakama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…