Uda
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 811
- 623
Tanzania imekumbwa na wimbi la wageni kutoka nje ambao huja na ulaghai kwa viongozi wa vijiji na vitongoji na kujimilikisha ardhi kilaghai.
Wengi wa wageni hasa kutoka magharibi wanakuja na gia ya kujenga shule au zahanati au mradi wa maji katika sehemu ndogo ya ardhi inayoombwa kwa vijiji. baadae huanzisha miradi yao mingine kama hoteli za kitalii,viwanda n.k kwa nia ya kujipatia fedha tena bila kulipa kodi.
Maeneo mengi ambayo ni strategic kama vile hifadhi za Taifa,maeneo yenye madini n.k ndio sehemu wanazoenda kuzishika na kuestablish himaya zao kwa kuwanunua wazee wa kimila ,viongozi wa vijiji na watendaji wa Serikali. Ukitazama maeneo mengi yenye migogoro ya ardhi nyuma yake yupo muwekezaji flani kutoka ughaibuni.
Yapo maeneo nimewahi kutembelea unakuta kuna vibao vingi vya muwekezaji kuliko vibao vinavyoashiria uwepo wa Serikali...hii ni fedheha na ukoloni mamboleo.
Wizara ya ardhi mambo ya ndani fungueni macho na kuchukua hatua.