BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Watu walikuwa wengi kiasi cha kusababisha changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na ufinyu wa muda, hali hiyo ilichangia pia kuonekana kuna uhaba wa vifaa pamoja na watoa huduma kuwa wachache.
Zoezi hilo lililofanyika Februari 24 na 25, 2025 lilisababisha msuguano wa hapa na pale na kukosekana kwa wenye mahitaji maalum kutopewa vipaumbele kama vile walemavu, wazee, wajawazito na kina mama wenye watoto wadogo.
Tumeshuhudia fujo kadhaa zikifanyika kutokana na foleni kuwa kubwa mpaka ngumi zikichapwa katika vituo vya kutolea huduma.
Kibaya zaidi ni kuwa baadhi ya watu walifikia hatua wakawa wanauziwa fomu licha ya kuwa zinatakiwa kutolewa bure, ambapo waliuziwa Tsh. 200 kama gharama ya kutoa nakala (photocopy).
Changamoto hizo zimejitokeza katika Kata ya Nsololo, tunajiuliza kwanini Mamlaka inayohusika isingefanya zoezi hili kwa mpangilio wa vijiji, kwani kilichofanyika ,chakato umekamilika lakini kuna watu wengi hawajakamilisha mchakato.
Ni kama wameenda kutiki boksi tu lakini kazi haijakamilika, kuna Watu wengi hawajakamilisha mchakato wa kuboresha taarifa zao.
Pia soma
~ Mwitikio wa wanaojiandikisha NIDA Wilaya ya Uyui ni mkubwa lakini Watendaji na Vifaa havitoshi
~ NIDA yatoa majibu ya changamoto zinazolalamikiwa katika Uandikishaji Vitambulisho vya NIDA Wilayani Uyui Mkoani Tabora