DOKEZO Waliofanya Uandikishaji Vitambulivyo vya NIDA, Nsololo - Uyui hawajakamilisha kazi, bado watu wengi hawajakamilisha mchakato

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.


Your browser is not able to display this video.
Zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambalo limefanyika kwa siku mbili katika Wilaya ya Uyui hapa Tabora lilipokelewa vizuri na Wananchi na inawezekana mwitikio umekuwa mkubwa kuliko walivyotegemea.

Watu walikuwa wengi kiasi cha kusababisha changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na ufinyu wa muda, hali hiyo ilichangia pia kuonekana kuna uhaba wa vifaa pamoja na watoa huduma kuwa wachache.

Zoezi hilo lililofanyika Februari 24 na 25, 2025 lilisababisha msuguano wa hapa na pale na kukosekana kwa wenye mahitaji maalum kutopewa vipaumbele kama vile walemavu, wazee, wajawazito na kina mama wenye watoto wadogo.

Tumeshuhudia fujo kadhaa zikifanyika kutokana na foleni kuwa kubwa mpaka ngumi zikichapwa katika vituo vya kutolea huduma.

Kibaya zaidi ni kuwa baadhi ya watu walifikia hatua wakawa wanauziwa fomu licha ya kuwa zinatakiwa kutolewa bure, ambapo waliuziwa Tsh. 200 kama gharama ya kutoa nakala (photocopy).

Changamoto hizo zimejitokeza katika Kata ya Nsololo, tunajiuliza kwanini Mamlaka inayohusika isingefanya zoezi hili kwa mpangilio wa vijiji, kwani kilichofanyika ,chakato umekamilika lakini kuna watu wengi hawajakamilisha mchakato.

Ni kama wameenda kutiki boksi tu lakini kazi haijakamilika, kuna Watu wengi hawajakamilisha mchakato wa kuboresha taarifa zao.





Pia soma
~
Mwitikio wa wanaojiandikisha NIDA Wilaya ya Uyui ni mkubwa lakini Watendaji na Vifaa havitoshi
~ NIDA yatoa majibu ya changamoto zinazolalamikiwa katika Uandikishaji Vitambulisho vya NIDA Wilayani Uyui Mkoani Tabora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…